Maambukizi ya Rubella kwa Watoto
Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
Maambukizi ya rubella kwa watoto yamepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa uelewa juu ya umuhimu wa matibabu na chanjo zinazotolewa kwa kina mama na watoto. Hata hivyo maambukizi haya kwa mtoto mdogo baada ya kuzaliwa huwa hayaleti madhara makubwa ukilinganisha na madhara anayoweza kupata mama endapo atamwambukiza mtoto akiwa tumboni, yakiwepo ufanyikaji mbovu wa organi mbalimbali za mtoto kama moyo n.k
Kirusi aina ya rubella anayesafilishwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mwathilika, mara baada ya kumpata mtu mwingine huvamia koo na mitoki ya kooni na hivyo hujizalia na kuongezeka. Baadhi ya virusi hawa huweza kuingia katika mfumo wa damu na baadae wanaweza kusambaa kwenye ngozi, kwenye maji ya mfumo wa fahamu, uteute wa magoti na kondo la nyuma hivyo kwa njia hii mama huweza kumwambukiza mwanae akiwa bado tumboni
Kabla ya chanjo dhidi ya rubella kutambuliwa mwaka 1969, ugonjwa huu ulikuwa ukitokea kwa mlipuko katika nchi moja au sehemu fulani ya nchi moja kila baada ya miaka 6-9 na kutokea kwa mlipuko uliodhuru nchi nyingi kila baada ya miaka 10-20. Mwaka 1977-1981, watoto 20,395 walilipotiwa kuwa na ugonjwa huu kutokana na rekodi za statistical handbook on rubella za huko USA na kutoke hapo mpaka sasa ugonjwa huu umekuwa ukipungua.Katika mwaka 1990 watoto 1124 waliathiliwa, mwaka 1999 watoto 267 na toka hapo kipindi hicho watoto chini ya kumi wanaathiliwa na ugonjwa huu na watoto wanaoathiliwa mpaka sasa wakiwa wanapata maambukizi haya kw mama ni chini ya 10. Rekodi za tafiti katika nchi za afrika hazipatikani sana kutokana na kutoandika taarifa hospitali au tafiti kutofanyika.
Kimataifa ugonjwa huu wa rubella kwa watoto wakiwa bado tumboni umeonekana kusababisha asilimia 15 ya matatizo ya kuzaliwa kwa watoto
Dalili za ugonjwa wa rubella ni zipi?
Kirusi huyu anapoingia mwilini hukaa siku 14 hadi 23 kabla mtu hajaanza kuonyesha dalili. Na kama mtoto ameathirika na kirusi huyu huonyesha dalili zifuatazo;
-
Mwili kuchoka
-
Homa
-
Kukosa hamu ya kula
-
Maumivu ya kichwa
-
Maambukizi kwenye macho(macho kuuma)
-
Kutokwa na mafua
-
Mtoto anapata vipele ndani ya siku 1-5 baada ya dalili za hapo juu kuanza, vipele huanzia usoni na mbele ya kichwa na kusambaa kuelekea miguuni ukiathiri tumbo na miguu, vipele hivyo hutoweka kwa mtililiko huohuo kama vilipoanza
-
Vipele vinaweza kuwasha, lakini hutoweka ndani ya siku tatu bila mabaki yoyote. Vipele huwa na rangi ya pinki na huwa vimeinuka au kama mabaka
Mtoto anaweza kuvimba mitoki sasa sana usoni ,nyuma ya shingo na kichwani. Vipele hivyo huwa na
Madhara ya ugonjwa huu ni yapi?
Maambukizi kwa watoto waliozaliwa na wana afya njema huwa ya kujizuia na hayaleti madhara makubwa
Madhara makubwa yoweza kuyapata watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu ni;
-
Kuzaliwa na matatizo ya vidole,kiwiko cha mkono na magoti yanayoweza kuendelea kwa muda wa mwaka mmoja au zaidia madhara haya hutokea maranyingi
-
Upungufu wa chembe za kugandisha damu kitaalamu thrombocytopenia na watoto wanaweza kuwa na mivirio ya damu au kutokwa na damu, hili hutokea kwa nadra
-
Matatizo ya kuzaliwa nayo ni kama kutofanyika vyema au matatizo katika organi mbalimbali mwilini kama mfumo wa fahamu, macho na mifupa. Kichanga mwenye ugonjwa huu toka tumboni huweza kushambuliwa na magonjwa yatokanayo na kinga ya mwili kushambulia chembe hai za mwili kitaalamu autoimmune disease na upungufu wa utengenezwaji wa kinga mwilini aina ya antibodies (dysgammagloburinemia) ukubwani
-
Uhalibifu kwa mtoto unatokea sana endapo mama alikuwa na maambukizi haya miezi miwili ya kwanza ,tena kuna hatari ya kupata madhara hayo mama akiwa na miezi 5.
