top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

10 Juni 2020 14:28:14

Aina za shinikizo la damu la juu (Haipatenshen)
Aina za shinikizo la damu la juu (Haipatenshen)

Aina za shinikizo la damu la juu (Haipatenshen)

Tatizo la Haipatenshen limegawanywa katika makundi tofauti kulingana na mahitaji ya kitiba, Kundi la kwanza limetokana na visababishi, katika kundi hili kuna aina mbili yaani haipatenshen ya awali na haipatenshen ya sekondari.


Makundi ya haipatenshen kutokana na visababishi

Haipatenshen ya awali


Haipatenshen ya awali ni aina ya shinikizo la juu la damu, kisababishi mara nyingi huwa hakifahamika. Huchangia kwa asilimia 90 - 95 ya ugonjwa wa haipatensheni haswa watu wazima wenye umri wa miaka 35 na kuendelea.

Haipatensheni ya awali huhusianishwa na sababu za kimazingira au za kiasilia kama ifuatavyo;

  • Kurithi- inaonekana kwamba watu wengi wenye shinikizo la damu baadhi huwa na historia hii kwenye familia zao lakini urithishwaji huu bado haueleweki vizuri. Kuna utafiti umefanyika na kuonesha watoto mapacha wanaozaliwa wote wanaweza kupata shinikizo la damu la juu kwa asilimia 33-57%

  • Uzito mkubwa kupita kiasi (ugonjwa wa obeziti)

  • Ugonjwa wa kisukari

  • Magonjwa ya moyo


Haipatenshen ya sekondari


Haipatenshen ya sekondari huchangiakwa asilimia 5-10 ya shinikizo la juu la damu. Zipo sababu za moja kwa moja zinazofahamika kusababisha haipatensheni hii. Watu wanaopata shinikizo hili la damu wengi huonekana kuwa na umri chini ya miaka 35.


Makundi mengine ya shinikizo la juu la damu


Shinikizo la juu la damu linalozidi la 180/120 linaweza kugawanywa tena katika makundi mawili ambayo ni;

Shinikizo la damu la juu linalohitaji matibabu ya haraka

Shinikizo hili haliambatani na ishara ya madhara ya shinikizo kwenye ogani ndani ya mwili, mgonjwa huenda hospitali akiwa anajihisi vibaya na anapopimwa anakuwa na shinikizo la damu la juu sana. Matibabu ya shinikizo hili huchukua siku 2 hadi 3 na dawa za kumeza hutumika mgonjwa akiwa amelazwa wodini, au nyumbani chini ya usimamizi wa daktari.


Shinikizo la damu linalohitaji matibabu ya dharura

Aina hii inajitokeza na dalili za uhalibifu wa organi mbalimbali mwilini kama vile macho(kushindwa kuona vema), ubongo( mabadiliko ya kiakili/tabia ya mtu), figo (kutokukojoa au kukojoa mkojo kidogo sana), mapafu(maumivu ya kifua) na moyo(maumivu ya moyo ya ghafla na maumivu ya kifua), mapafu (maji kwenye mapafu) na ujauzito( kifafa cha mimba), ubongo( damu kuvia kwenye ubongo) na moyo (mshituko wa moyo na kifo).


Mgonjwa anahitaji matibabu ya dharura kwenye chumba cha watu mahututi yani ICU na matibabu yake yanahusisha kushusha shinikizo hili ndani ya saa 1 hadi 2nadawa za zinazotumika ni za kuchoma kwenye mishipa ili kuepuka madhara makubwa zaidi yanayoweza kutokea na kuokoa maisha

Imeboreshwa,

6 Oktoba 2021 10:45:33

ULY Clinic inakushauri siku zote usichukue hatua yoyote ile inayoathiri afya yako bila kuwasiliana na daktari wako. 

Wasiliana na daktari wa ULY CLinic kwa kubonyeza 'Pata Tiba' au kutumia namba za simu chini ya tovuti hii kwa elimu suhauri na Tiba

Rejea za mada hii,

​

  1. Beckett  NS, Peters  R, Fletcher  AE,  et al; HYVET Study Group.  Treatment of hypertension in patients 80 years of age or older.  N Engl J Med. 2008;358(18):1887-1898.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020

  2. SHEP Cooperative Research Group.  Prevention of stroke by antihypertensive drug treatment in older persons with isolated systolic hypertension: final results of the Systolic Hypertension in the Elderly Program (SHEP).  JAMA. 1991;265(24):3255-3264. ArticlePubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020

  3. Institute of Medicine.  Clinical Practice Guidelines We Can Trust. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Clinical-Practice-Guidelines-We-Can-Trust.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020

  4. Staessen  JA, Fagard  R, Thijs  L,  et al; The Systolic Hypertension in Europe (Syst-Eur) Trial Investigators.  Randomised double-blind comparison of placebo and active treatment for older patients with isolated systolic hypertension.  Lancet. 1997;350(9080):757-764.PubMedGoogle ScholarCrossref. Imechukuliwa 09.06.2020

  5. Hsu  CC, Sandford  BA.  The Delphi technique: making sense of consensus.  Pract Assess Res Eval. 2007;12(10). http://pareonline.net/pdf/v12n10.pdf. Accessed October 28, 2013.Google Scholar. Imechukuliwa 09.06.2020

  6. Institute of Medicine.  Finding What Works in Health Care: Standards for Systematic Reviews. Washington, DC: National Academies Press; 2011. http://www.iom.edu/Reports/2011/Finding-What-Works-in-Health-Care-Standards-for-systematic-Reviews.aspx. Imechukuliwa 09.06.2020

  7. https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-in-adults-beyond-the-basics?topicRef=4415&source=see_link. Imechukuliwa 10.06.2020

  8. https://www.uptodate.com/contents/high-blood-pressure-diet-and-weight-beyond-the-basics.Imechukuliwa 10.06.2020

  9. Hypertension. https://jamanetwork.com/journals/jama/fullarticle/1791497. Imechukuliwa 11.06.2020

  10. Dash Diet- 365 Days of Low Salt, Dash Diet Recipes For Lower Cholesterol, Lower Blood Pressure and Fat Loss Without Medication ( PDFDrive.com )

bottom of page