top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY Clinic

​

Maumivu ya titi (mastalgia)

​

Utangulizi

​

Maumivu ya titi(ziwa) ni dalili inayotokea mara kwa mara kwa wanawake, Dalili hii huweza kuwa na sifa ya, maumivu ya chuchu zikishikwa, maumivu ya kuchoma au kuunguza au kubana kwenye tishu zinazotengeneza titi.

​

Maumivu  huweza kuwa makali au ya kawaida na huweza kutokea

​

  • Siku chache za mwezi, siku mbili au tatu kabla ya kuanza hedhi yako ya mwezi. Kutokea kwa maumivu wakati huu ni kawaida, maumivu huwa kidogo au ya wastani na huweza husisha matiti yote mawili

  • Kwa wiki au zaidi katika mwezi, huanza kabla ya kuona hedhi yako,na wakati mwingine huendelea katika kipindi chote cha hedhi. Maumivu huwa ya wastani au makali sana na huathiri matiti yote mawili

  • Maumivu yanayoedelea mwezi mzima au Zaidi, maumivu haya hayana mahusiano na mzunguko wa hedhi.

​

Wanawake wanaokaribia komahedhi wakati mwingine hupata maumivu ya matiti, hata hivyo maumivu ya matiti hutokea sana kwa wanawake vijana ambao bado hawajafikia kwenye komahedhi.

​

Mara nyingi maumivu ya chuchu huwa hayasababishwi na saratani na huwa haya maanishii una saratani. Licha ya hayo, maumivu ya matiti ambayo yanaendelea hata baada ya komahedhi au yasiyoisha baada ya mzunguko 1 au 2 ya hedhi huhitaji kufanyiwa uchuguzi wa ndani ili kujua visababishi.

​

​

Visababishi

​

Wakati mwingine si rahisi kujua kisababishi cha maumivu ya matiti. Mambo yanayochangia kupata maumivu ya titi ni pamoja na;

​

Mabadiliko ya Homoni za uzazi

​

  • Tafiti na ushahidi wa kisayansi huonesha maumivu ya chuchu huhusiana na mabadiliko ya kiwango cha homoni za uzazi(estrogen na progesterone) zinazotofautiana kiwango katika kipindi cha mzunguko mzima wa hedhi.

 

Maumivu ya titi ya kujirudia katika mwezi hupotea endapo mtu anatapa mimba au hedi itakoma

​

Umbo la titi

​

  • Maumivu ya titi yasiyohusiana na mzunguko wa hedhi hutokea kutokana na mabadiliko yanayotokea katika maumbile ya tezi na mirija inayopitisha maziwa katika titi. Mabadiliko haya yanaweza kusababisha kutokea kwa vifuko vya maji kwenye chuchu.

 

Visababishi vingine ni

​

  • Majeraha au kupigwa kwenye chuchu 

  • Kuwa na titi kubwa pia husababisha maumivu ya titi kutokana na uzito

  • Kufanyiwa upasuaji wa titi

  • Matumizi ya dawa jamii ya antidepresant na baadhi ya dawa asilia kama vile dawa zenye tangawizi

  • Msongo wa mawazo na shauku iliyopitiliza

​

Hata hivyo maumivu ya titi huweza kuanzia nje ya titi mfano kifuani, kwenye misuli, maungio ya mifupa na kisha kuelekea kwenye chuchu.

​

Sifa za maumivu ya titi

​

Maumivuya titi yanayojirudia rudia kila mwezi

​

  • Uhusiana na mzunguko wa hedhi

  • Huwa si makali, kuuma na kuhisi uzito

  • Huambatana na kuvimba kwa titi au kuhisi uvimbe ndani

  • Hudhuru matiti yote, haswa sehemu ya juu na maumivu huelekea kwenye kwapa

  • Huwa makali zaidi wiki mbili kabla ya kuona damu ya mwezi, baada ya hapo hupungua

  • Hudhuru wanawake walio katika umri wa kupata watoto, pia kwa wanawake wamiaka 40 wanaoelekea kwenye komahedhi

 

Maumivu  ya titi yasiyojirudia

​

  • Hayahusiani na siku za mzunguko wa hedhi

  • Huwa ya kubana, kuunguza au kama kidona kinavyouma

  • Maumivu huwa yapo mda wote au kuja na kuondoka

  • Hudhuru titi moja mara nyingi na sehemu moja tu, wakati mwingine titi zima linaweza kuwa linauma

  • Hudhuru wanawake kipindi baada ya komahedhi

​

​

ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.

​

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa Elimu ,ushauri na Tiba kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

​

Imeboreshwa 6.12.2020

​

Rejea za mada hii

​

  1. Golshan M, et al. Breast pain. https://www.uptodate.com/contents/search.Imechukuliwa 6.12.2020

  2. Breast pain(mastalgia). https://www.breastcancer.org/symptoms/benign/mastalgia. Imechukuliwa 6.12.2020

  3. Jokich PM, et al. ACR Appropriateness Criteria breast pain. American College of Radiology (ACR). https://acsearch.acr.org/docs/3091546/Narrative/. Imechukuliwa 18.04.2020

  4. Rapkin AJ, et al. Premenstrual syndrome. First consult. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 6.12.2020

  5. Balleyguiera C, et al. Breast pain and imaging. Diagnostic and Interventional Imaging. 2015;96:1009.

  6. Mastalgia (breast pain). Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/breast-disorders/mastalgia-breast-pain. Imechukuliwa 6.12.2020

  7. Rikers A.Breast Disease:Comprehensive Management. New York, N.Y.: Springer; 2015: 79.

  8. Vitamin E fact sheet for consumers. National Institutes of Health. https://ods.od.nih.gov/factsheets/VitaminE-Consumer/. Imechukuliwa 6.12.2020

  9. Breast pain. https://breastcancernow.org/information-support/have-i-got-breast-cancer/benign-breast-conditions/breast-pain#. Imechukuliwa 6.12.2020

bottom of page