Komahedhi
​
Imeandaliwa na daktari wa ULY-clinic
​
​
Komahedhi ni ishara au neno limalomaanisha hedhi kuisha, maelezo ya kitaalamu humaanisha pale mwanamke anapoacha kuona damu ya mwezi kwa miezi 12 mfululizo.
​
Kutokwa damu baada ya hedhi kukoma hua sio jambo la kawaida na inapaswa kufanyiwa uchunguzi wa kitaalamu endapo mwanamke amepata hali hii.
Kwa mafano, kutokwa damu ukeni baada ya komahedhi kunaweza kusababishwa na matatizo kama haya yalioorodheshwa hapo chini;
-
Saratani ya mfuko wa kizazi, ikiwa pamoja na saratani ya kuta za ndani ya kizazi, saratani ya misuli ya kizazi, saratani ya shingo ya kizazi
-
Kusia kwa kuta za uke au kusinya kwa kuta za ndani ya kizazi.
-
Fibroid ndani ya kizazi
-
Vinyama ndani ya kuta za uzazi
-
Maambukizi ndani ya mfuko wa kizazi
-
Matumizi ya madawa kama homoni au dawa inayoitwa tamoxifen
-
Majeraha kwenye uzazi
-
Kutokwa damu kutoka kwenye mfumo wa mkojo, au njia ya haja kubwa
-
Kukua kupitiliza kwa seli ndani ya mfuko wa kizazi
Sababu zinazosababisha kutokwa na damu baada ya komahedhi zinaweza kuwa si za kudhuru, ingawa kuona damu baada ya komahedhi kunaweza kusabaishwa na tatizo kubwa ndani ya mwili, hivyo ni muhimu kuonana na daktari ili kupata uchunguzi na matibabu sahihi.
​
Soma zaidi kuhusu komahedhi kwa kubonyeza hapa
​
​
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ili dhidi ya afya yako.
​
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa elimu na ushauri kupitia namba za simu au kubonyeza Pata Tiba chini ya tovuti hii.
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 25 .04.2020
​
-
Web.Md.Menopause.https://www.webmd.com/menopause/guide/menopause-symptoms-types. Imechukuliwa 10/4/2020
-
Health.Line.Today.Menopause.https://www.healthline.com/health/menopause.Imechukuliwa 10/4/2020
-
Menopause. National Institute on Aging. http://www.nia.nih.gov/health/publication/menopause. Imechukuliwa 10.04.2020
-
Casper RF, et al. Clinical manifestations and diagnosis of menopause. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020
-
Longo DL, et al., eds. Menopause and postmenopausal hormone therapy. In: Harrison's Principles of Internal Medicine. 19th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education; 2015. http://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 10.04.2020
-
Nelson LM, et al. Clinical manifestation and evaluation of spontaneous primary ovarian insufficiency (premature ovarian failure). https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 10.04.2020
-
Menopausal symptoms and complementary health practices. National Center for Complementary and Alternative Medicine. http://nccam.nih.gov/health/menopause/menopausesymptoms. Imechukuliwa 10.04.2020
-
Medical.New.Today.Menopause.https://www.medicalnewstoday.com/articles/155651.Imechukuliwa 10/4/2020
-
Dc Dutta Textbook Gynaecology ISBN 978-93-5152-068-9 written by Hiralal Konar Ukurasa wa 57-60