Imeandikwa na ULY CLINIC
Ulimi kunaswa/kushikwa
Utangulizi
Ulimi kushikwa (kwa jina jingine hufahamika kama ulimi uliofungwa, ulimi wenye kamba au ankailoglosia) ni hali inayotambuliwa wakati mtotot anazaliwa, hali hii hupelekea ulimi wa mtoto kukosa uhuru wa miendo inayotakiwa kama binadamu wa kawaida
Mtoto mwenye Ulimi ulioshikwa huwa na utando ama ukuta mpana ulio chini ya ulimi na unashikamanisha ulimi kwenye sakafu ya kinywa. Mtu mwenye tatiazo la ulimu kifungoni huwa na tatizo la kutoweza kutoa ulimi nje yam domo, pia huathiri ulaji wa mtoto.
Wakati mwingine tatizo la ulimi kushikwa halisababishi tatizo llote lile, tatizo hili huhitaji matibabu ya upasuaji ili kuuweka ulimu kuwa huru
Dalili
Dalili za ulimi ulioshikwai ni ;
-
Ugumu katika tendo la kuinua ulimi kutoka katika sakafu ya kinywa
-
Kushindwa kutoa ulimi nje ya kinywa
-
Ulimi kuonekana una umbo la moyo ama umegawanyika kama ukitolewa nje
Wakati gani umwone daktari
Mwone daktari endapo;
-
Mtoto anadalili za ulimi kushikwa na anapata matatizo kama, kushindwa kunyonya vema
-
Kama mtoto anaonekana kuathiliwa uongeaji wake
-
Mtoto wako mkubwa analalamika ulimi wake umeshikwa na anashindwa kula, kuongea
-
Mtoto anakereka na tatizo hilo
Visababishi
Kwa kawaida utando unaoshika ulimi hukatika kabla ya kuzaliwa, na kuruhusu ulimi uwe na uhuru wa kujongea miendo yote. Ulimi ukiwa umeshikwa inamaana utando uitwao lingual frenulum umebaki bila kukatika na hivo huunga ulimi na sakafu ya kinywa. Kwanini hali hii hutokea? Hazijulikani sababu moaka sasa ingawa baadhi ya mambo yanayoambatana na ulimi kushikwa yanajulikana kama vile sababu za kijeni
Vihatarishi
Ingawa ulimi kushikwa unaweza kuathiliwa mtu yeyote Yule, hutokea sana kwa wanaume kulika kwa wanawake.
Wakati mwingine tatizo hili hutembea kwenye familia Fulani tu.
Madhara ya ulimi kushikwa
Ulimi kushikwa huweza kuathiri ukuaji wa kinywa cha mtoto pamoja na kuchangia katika matatizo ya kula, kuongea na kumeza.
Mfano wa matatizo yanayoweza tokea ni kama;
-
Matatizo ya kunyonya. Mtoto akiwa ananyonya hutakiwa kutuliza ulimi chini ya sakafu yam domoakishindwa kufanya hivi huweza kusababisha kutafuna badala ya kunyonya na hivo kusababisha maumivu kwenye ziwa/chuchu za mama. Hili hupelekea mama kushindwa kumnyonyesha mtoto na kuacha unyonyeshaji. Madhara ya kuacha unyonyeshaji husababisha mtoto kutokua vema.
-
Kushindwa kuongea. Huweza kuathiri utamkaji wa herufi kadhaa kama "t," "d," "z," "s," "th" and "l." huweza kupata tatizo la kuongea r pia
-
Hali duni ya usafi wa kinywa. Mtoto aliyekuwa, ulimi kushikwa unaweza kusababisha ulimi kutoosha mabaki ya chakula haswa yale yaliyo kwenye meno. Hili huweza kusababisha magonjwa ya meno na kinywa, ama meno kuoza
-
Kutofanya kazi zingine za ulimi. Hushindwa kunyonya barafu, kulamba midomo, kubusu, ama kupuliza kifaa cha mziki kama fluti
Vipimo na utambuzi
-
Ulimi kushikwa hutambuliwa wakati wa uchunguzi wa kinywa cha mtoto.
Matibabu
-
Matibabu ya ulimi kushikwa kwa watoto hutegemea mambo mbalimbali. Baadhi ya wataalamu wanashauri kutibiwa mara baada ya kuzaliwa ama tatizo linapoonekana hata kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbanii baada ya kujifungua. Hawa ni wataalamu wa kunyonyesha na madaktari.
-
Utando unaoshika ulimi unaweza kulegea muda unavyokwenda na kusababisha tatizo kuisha. Na wakati mwingine tatizo linaweza lisiishe na hivyo kufanya matibabu mengine yafanyike
-
Matibabu ya upasuaji huhusisha upasuaji wa kukata ute tu, au kukata ute( frenotomi ) na kuunga ulimi endapo tatizo lilikuwa kubwa yaani frenuloplasti
Wakati gani wa matibabu?
Matibabu ya ulimi kushikwa kwa watoto hutegemea na wataalamu uliokutana nao. Baadhi ya wataalamu wanashauri kutibiwa mara baada ya kuzaliwa ama tatizo linapoonekana hata kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbanii, na wengine wanashauri kukaa kwa muda Fulani kabla ya matibabu. Hawa ni wataalamu wa kunyonyesha na madaktari.
Utando unaoshika ulimi unaweza kulegea muda unavyokwenda na kusababisha tatizo kuisha. Na wakati mwingine tatizo linaweza lisiishe na hivyo kufanya matibabu mengine yafanyike
Kwa maana nyingine ukiona dalili hizi mwone daktari:
-
Mtoto ana dalili za ulimi kushikwa na anapata matatizo kama, kushindwa kunyonya vema
-
Kama mtoto anaonekana kuathiliwa uongeaji wake
-
Mtoto wako mkubwa analalamika ulimi wake umeshikwa na anashindwa kula, kuongea
-
Mtoto anakereka na tatizo hilo
Imeboreshwa, 22.09.2021
ULY CLinic inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kiafya baada ya kusoma makala hii;
Unaweza wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri zaidi na tiba kupitia kitufe cha wasiliana nasi au pata tiba chini ya tovuti hii.
Soma matatizo mengine ya ulimi kwa kubofya hapa
Nenda kwenye orodha kuu ya mada za afya kwa kubofya hapa
Rejea za mada hii,
-
NCBI. tongue tie and its managemenet https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3200025/. Imechukuliwa 07.08.2020
-
Tongue-tie (ankyloglossia). American Academy of Otolaryngology-Head and Neck Surgery. http://www.entnet.org/content/tongue-tie-ankyloglossia. Imechukuliwa 07.08.2020
-
Isaacson GC. Ankyloglossia (tongue-tie) in infants and children. https://www.uptodate.com/contents/search. AImechukuliwa 07.08.2020
-
O'Shea JE, et al. Frenotomy for tongue-tie in newborn infants. Cochrane Database of Systemic Reviews. http://onlinelibrary.wiley.com/doi/10.1002/14651858.CD011065.pub2/abstract. Imechukuliwa 07.08.2020