top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya miezi nane

Mimba ya miezi nane

Mimba ya miezi nane ni sawa na mimba ya wiki 29 hadi 32, katika kipindi hiki mabadiliko mbalimbali hutokea mwilini katika kila wiki. Makala hii imeelezea kuhusu mabadiliko yanayotokea katika lila wiki ya mimba ya miezi nane.


Mimba ya wiki ishirini na tisa (29)

Mtoto hukua na kucheza zaidi kwa kuwa nafasi huwa kubwa katika mji wa uzazi na uzito wa mama huongezeka zaidi.


Nini hutokea kwa mtoto
 • Huwa na urefu wa takribani sentimeta 37 na uzito wa gramu 1000

 • Mabadiliko makubwa hutokea katika ubongo wake ili kufanania ubongo wa mtu mzima

 • Huanza kupata ndoto, kukapua macho na kuonesha hisia tofauti tofauti kama vile tabasamu nk

 • Huanza kugeuka, asilimia kubwa ya vichanga hutanguliza kichwa


Nini hutokea kwa mama

Pamoja na mabadiliko ambayo huanza wiki ya 27, kitu cha pekee ambacho huanza kuonekana katika wiki hii ni kuhisi maumivu ambayo hutaka kufanana na uchungu (braxton-Hicks contractions), nenda kwenye makala ya uchungu kusoma zaidi kuhusu dalili za uchungu


Hali hii husababishwa na kutanuka na kusinyaa kwa misuli ya mji wa uzazi ambako huchukua muda wa sekunde 30 hadi dakika 2. Maumivu haya huwa hayana muendelezo na huwa ya kawaida japo huwa makali leba inapokaribia.


Mimba ya wiki thelathini (30)


Huanza kuona na kutofautisha vitu vinavyomzunguka, japo muda mwingi huwa amefumba macho


Nini hutokea kwa mtoto
 • Mtoto huwa na uzito wa takribani gramu 1300

 • Huanza kuona na kutofautisha vitu vinavyomzunguka, japo muda mwingi huwa amefumba macho


Nini hutokea kwa mama
 • Kuchoka sana

 • Maumivu ya mgongo na kiuno

 • Kukojoa mara kwa mara nk


Mimba ya wiki thalathini na moja (31)

Kichwa cha moto huanza kuwa na mweonekano mzuri na nywele laini zilizofunika mwili huanza kupotea.


Nini hutokea kwa mtoto
 • Nywele laini ambazo zilikuwa zimefunika sehemu kubwa ya mwili wake katika wiki za awali huanza kupotea

 • Huanza kuwa na muonekano mzuri wa kichanga

 • Huwa mwenye nguvu zaidi na hivyo hucheza sana hali inayoweza kupelekea mama kukosa usingizi


Nini hutokea kwa mama
 • Mji wa uzazi hutanuka sana na kuanza kugandamiza diaframu hivyo kupelekea kushindwa kupumua vizuri, mgandamizo huu huwa na maudhi makali kuliko wiki za awali

 • Pia mgandamizo katika kibofu cha mkojo huongezeka na kusababisha kutokwa na mkojo bila hiari wakati wa kupiga chafya au kucheka kwa nguvu, pamoja na kukojoa mara kwa mara

 • Matiti huanza kutoa maziwa ya awali (dang’a) ambayo ni mazito yenye rangi ya njano, hata hivyo huweza kutokea mapema zaidi au karibia na wiki za kujifungua na wakati mwingine baada ya kujifungua


Nini cha kufanya

Fanya mazoezi ya kuimarisha sakafu ya nyonga (mazoezi ya kegeli) ili kuzuia hali ya kutokwa na mkojo bila hiari kuendelea baada ya ujauzito, japokuwa kwa asilimia kubwa ya wanawake hali hii huisha baada ya kujifungua (kusoma zaidi kuhusu mazoezi ya kegeli tembelea.


Mimba ya wiki ya thalathini na mbili (32)

Uwezo wa kupumua kwa kuvita majimaji ya amniotiki huongezeka licha ya upumuaji halisi kuanza mara tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto.


Nini hutokea kwa mtoto
 • Mifumo na ogani nyingi huwa zipo katika hatua za mwisho za ukuaji ili kumuwezesha mtoto kuishi nje ya tumbo la uzazi

 • Uwezo wa kupumua na kutumia misuli ya upumuaji kwa kuyavuta maji ya amniotiki nje na ndani huimarika (huanza kati ya wiki 10-12),na ikumbukwe kuwa kupumua halisi huanza mara tu anapozaliwa. Hivyo anapokuwa tumboni hupata oksijeni na kutoa hewa ya kabonmonoksaidi kupitia kondo la nyuma.


Nini hutokea kwa mama

Huendelea kupata maudhi ya kipindi cha tatu cha ujauzito ambayo huongezeka siku kwa siku.

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 20:32:02 UTC

Rejea za mada hii:

 1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

 2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

 3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

 4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

 5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

 6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

 7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

 8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

 9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page