top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Dkt. Mangwella S, MD

19 Novemba 2021 18:29:15

Vidonge vyenye vichocheo viwili

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

Tarehe mwezi na mwaka na saa

ULY clinic inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia mawasiliano yetu.

Rejea za mada hii;

  1. Baird DT, et al. Hormonal contraception. N Engl J Med. 1993 May 27;328(21):1543-9.

  2. Maguire K, et al. The state of hormonal contraception today: established and emerging noncontraceptive health benefits. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S4-8.

  3. Committee on Gynecologic Practice. ACOG Committee Opinion Number 540: Risk of venous thromboembolism among users of drospirenone-containing oral contraceptive pills. Obstet Gynecol. 2012 Nov;120(5):1239-42.

  4. Shulman LP. The state of hormonal contraception today: benefits and risks of hormonal contraceptives: combined estrogen and progestin contraceptives. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S9-13.

  5. ACOG Practice Bulletin No. 110: noncontraceptive uses of hormonal contraceptives. Obstet Gynecol. 2010 Jan;115(1):206-218.

  6. Cooper DB, et al. Oral Contraceptive Pills. 2021 Aug 25. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing; 2021 Jan–. PMID: 28613632.

Vidonge vya uzazi wa pango vyenye vichocheo viwili ni nini?

Ni vidonge vyenye kiasi kidogo ya vichocheo vya kutengeneza vya aina mbili projestini na estrojeni ambavyo vinafanana na vichocheo vinavyozalishwa mwilini.


Vidonge vyenye vichocheo viwili pia vinajulikana kama “combined pills”


Vidonge hivi hufanyaje kazi?


Hufanya kazi hasa kwa kuzuia kuachiwa kwa mayai kutoka kwenye ovari (uovuleshaji)



Vinafanya Kazi kwa Ufanisi Kiasi Gani?


Ufanisi unategemea mtumiaji:


Hatari ya kupata mimba ni kubwa wakati mwanamke anapoanza pakiti mpya ya vidonge akiwa amechelewa siku 3 au zaidi, au akiacha kumeza vidonge vitatu au zaidi karibu na mwanzo au mwisho wa pakiti ya vidonge.

Inafahamika kuwa wanawake 8 kati ya 100 watapata mimba kama wakitumia njia hii ipasavyo katika mwaka wa kwanza.


Iwapo kutatokea makosa ya kusahau kumeza vidonge, kutakuwa na mimba 1 kwa wanawake 100 wanaotumia vidonge vyenye vichocheo viwili kwa mwaka wa kwanza


Je unaweza kupata mimba kirahisi baada ya kuacha vidonge?


Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wanaotumia vidonge hivi mara wanapoacha kuvitumia, uwezo wao wa kupata hurejea mara moja.


Vidonge hivi vinakinga dhidi ya magonjwa ya zinaa?


Hapana!


Vidoge vya uzazi wa mpango vyenye vichocheo viwili havizuii magonjwa ya zinaa. Unatakiwa kutumia njia zingine kujikinga na magonjwa ya zinaa.



Maudhi ya vidonge vya uzazi wa mpango vyenye vichocheo viwili



Baadhi ya watumiaji wameripoti yafuatayo:


  • Mabadiliko ya tabia ya hedhi

  • Hedhi kidogo na siku chache za hedhi

  • Hedhi isiyotabirika

  • Hedhi ya mara chache

  • Hawakupata hedhi

  • Maumivu ya kichwa

  • Kizunguzungu

  • Kichefuchefu

  • Maumivu ya Matiti

  • Mabadiliko ya uzito

  • Mabadiliko ya mhemko

  • Chunusi (zinaweza kupungua au kuongezeka, lakini kawaida hupungua)


Maudhi mengine mwilini


  • Husababisha damu kuganda ndani ya mishipa ya miguu au mapafu

  • Kiharusi

  • Shinikizo la damu la juu


Kwanini wanawake wengi wanapenda kutumia vidonge vya uzazi wa mpango vyeney vichocheo viwili?


Asilimia 25 hadi 44 ya wanawake hupenda kutumia dawa yenye vichocheo viwili kutokana na;


  • Kumudiwa na wanawake

  • Vinaweza kuacha kutumiwa wakati wowote bila msaada wa mtoa huduma

  • Haviathiri tendo la ngono


Faida za Kiafya Zinazojulikana


Husaidia kukinga dhidi ya:


  • Hatari ya kupata mimba

  • Saratani ya kizazi

  • Saratani ya ovari

  • Dalili za ugonjwa wa uvimbe wa pelvisi

  • Uvimbe wa ovari


Vidonge vyenye vichocheo viwili hupunguza:


  • Maumivu makali wakati wa hedhi

  • Matatizo ya kutokwa damu za hedhi

  • Maumivu wakati wa uovuleshaji

  • Nywele nyingi usoni na mwilini

  • Dalili za ugonjwa wa polycystic ovar- ian syndrome (hedhi isiyotabirika, chu- nusi, nywele nyingi usoni na mwilini)

  • Dalili za endometriosisi (maumivu ya nyonga, hedhi isiyotabirika)


Vidokezo muhimu kuhusu vidonge vya uzazi wa mpango vyenye vichocheo viwili


Meza kidonge kimoja kila siku

Ili kupata mafanikio makubwa mwanamke lazima ameze vidonge kila siku na kuanza pakiti mpya ya dawa kwa wakati.


Kubadilika kwa hedhi hutokea kwa watumiaji lakini hakuna madhara

Kwa kawaida hupata hedhi isiyotabirika kwa miezi michache ya kwanza na kisha hupungua na baadaye kupata hedhi ya kawaida.


Meza kidonge ulichosahau kumeza haraka iwezekanavyo

Kusahau kumeza kidonge huongeza hatari ya kupata mimba na huweza ongeza maudhi ya dawa.


Vinaweza kutolewa wakati wowote na kutumiwa baadae

Kama unahitaji tumia vidonge vya uzazi wa mpango vyenye vichocheo viwili lakini huna uhakika kuwa una mimba au la, unaweza kupewa vidonge hivi ili uanze kutumia mara utakapoanza kuona damu ya hedhi. Havipaswi kutumika ukiwa na mimba.

bottom of page