top of page

Uzazi wa mpango

Bangiri ya uzazi wa mpango

Bangiri ya Uzazi wa Mpango

Ni njia yenye ufanisi mkubwa ya kuzuia mimba kwa kutoa homoni zinazozuia ovulesheni na kubadilisha mazingira ya mfumo wa uzazi. Tofauti na vidonge vinavyohitaji matumizi ya kila siku, bangiri hutoa urahisi wa matumizi kwa kubadilishwa kwa ratiba maalumu, lakini hailindi dhidi ya magonjwa ya zinaa hivyo kondomu bado ni muhimu kwa kinga hiyo. Kutumika kwa usahihi na kuchaguliwa kulingana na hali ya afya ya mwanamke huongeza ufanisi na kupunguza hatari ya madhara.

Kitanzi cha madini shaba

Kitanzi chenye madini ya shaba

Kitanzi chenye madini shaba kimeonekana kufanya kazi vizuri sana ya kuzuia mimba kwa kipindi cha takribani miaka 12 na kikitolewa mwanamke huweza kushika mimba kwa haraka.

Kiwambo cha uzazi wa mpango

Kiwambo cha Uzazi wa Mpango

Kimetengenezwa kwa raba laini na huwa na umbo la pia(dome), kizuizi kikiwekwa kwenye mlango wa kuingilia kwenye shingo ya kizazi huzuia mbegu kuingiakwenye mfuko wa uzazi wakati wa tendo la kujamiiana, wakati mwingine vizuizi huwa na kemikali za kuua mbegu za kiume.

Kondomu kama njia ya uzazi wa mpango

Kondom ya kike

Kondomu ya kike ni njia salama ya kuzuia mimba na kupunguza hatari ya VVU na magonjwa mengi ya zinaa inapowekwa na kutumiwa kwa usahihi kila tendo. Kwa kinga bora, tumia kondomu mpya kila tendo, usitumie kondomu ya kike na ya kiume kwa pamoja, na chagua kilainishi kinachofaa kulingana na aina ya kondomu.

Kondomu ya kiume

Kondomu ya kiume

Ni njia rahisi na yenye ufanisi ya kuzuia mimba na kupunguza hatari ya VVU pamoja na magonjwa mengi ya zinaa inapovaliwa kwa usahihi kabla ya tendo na kutumiwa hadi mwisho wa tendo. Kwa kinga bora, tumia kondomu mpya kila tendo, chagua inayokufaa, tumia kilainishi cha maji au silikoni inapohitajika, na epuka mafuta kwenye kondomu za lateksi kwa sababu yanaweza kuifanya ipasuke.

bottom of page