Mwandishi;
ULY CLINIC
Mhariri;
7 Aprili 2020 16:45:43
Kirusi cha UKIMWI
Kirusi cha UKIMWI ni kirusi ambacho kitiba kinaitwa Humman Immunodeficiency Virus au HIV kama watu wengi wanavyo fahamu na kwa lugha ya kiswahili huitwa Virusi Vya UKIMWI, kifupisho chake VVU au HVI1/2.
Magonjwa yanayosababishwa na HIV
Kirusi hiki husababisha ugonjwa wa Upungufu wa KInga MWIlini au UKIMWI. UKIMWI ni moja ya ugonjwa wa mlipuko wenye kuteketeza watu Zaidi ukilinganisha na magonjwa mengine yaliyorekodiwa duniani. Kwa mara ya kwanza UKIMWI uligunduliwa Los Angeles mwaka 1981, kwa Tanzania mgonjwa wa kwanza aligundulika mwaka 1983.
Familia ya kirusi cha HIV
HIV ni kirusi kimojawapo kwenye familia ya retrovirus, virusi katika familia hii hufahamika kwa;
Kinga za mwili kuwa na mwitikio hafifu dhidi yao
Kujificha kwa muda ndani ya mwili wa binadamu
Kukaa kwa muda mrefu kwenye damu
Kusababisha maambukizi kwenye mfumo wa fahamu wa kati Familia ya retrovirus ikiwa pamoja na HIV huwa na ukuta unaofunika RNA, DNA yao hutegemea RNA ili kuzalishwa.
Sifa za kirusi
Huwa na umbo la duara na kipenyo cha nautiko maili 120
Huwa na kuta tatu za kipekee
Jinomu ya kirusi huwa ni tata ukilinganisha na virusi wengine kwenye familia ya retrovirus
Kujizalisha kwake hufanana na virusi wengine wa kwenye familia ,hutegemea CD4 ya binadamu ili kuzaliana
Maambukizi kwa binadamu kupelekea mfumo wa kinga kuathiriwa hivyo kinga ya mwili kushuka
Huweza kubadilisha jinomu yake ya RNA na kuwa DNA kwenye seli za binadamu
Kirusi huyu hana dawa ya kumuua bali kuna dawa ya kupunguza makali yake
Kirusi huyu hawezi kustahimili katika nyuzi joto za 68 Fahrenheit
Kirusi huweza ishi vizuri kwenye PH ya 7 hadi 8
Kipindi cha kumwambukiza binadamu na kuleta ugonjwa wa UKIMWI inakadiliwa kuwa miaka 10 kwa vijana wadogo.
Virusi vingine kwenye familia ya retrovirus
Baadhi ya virusi vingine kwenye familia ya retrovirus ni;
Caulimoviridae
Pseudoviridae
Metaviridae
Belpaoviridae
Aina za virusi vya UKIMWI (VVU)
Kuna aina mbili za virusi vya Ukimwi ambavyo ni;
HIV aina ya 1 (HIV1 au VVU1)
HIV aina ya 2 (HIV2 au VVU2)
Magonjwa yanayosababishwa na VVU
Kirusi cha UKIMWI huweza kusabababisha magonjwa yafuatayo;
UKIMWI (AIDS)
Magonjwa nyemelezi mfano homa ya Mapafu, Kaposis Sakoma na magonjwa ya ngozi kama Molluscum Contagiusum
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi huyu huweza kutunzwa na binadamu pamoja na sokwe
Uenezaji wa kirusi cha UKIMWI
Uenezaji wa kirusi huyu kumegawanyika katika makundi makuu matatu;
Kwa njia ya ngono isiyo salama
Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Kugusana na majimaji ya damu yanayotoka kwa mtu mwenye HIV
HIV haienezwi kwa njia zifuatazo;
Kupeana mikono
Kukumbatiana
Kwa njia ya chakula
Kwa njia ya hewa kama kukohoa au kupiga chafya
Kushiriki choo pamoja na mtu mwenye Maambukizi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya VVU
Sababu za kitabia kama kushiriki pamoja vitu vya ncha kali na mwenye maambukizi kama sindano na viwembe, kufanya ngono zisizo salama bila kutumia kondomu ,kuwa na wapenzi wengi
Sababu za kijamii kama kuwa maskini ,kazi za utotoni ,kukosa maarifa juu ya njia za kujikinga na HIV na migogoro
Sababu za kibailojia kama kutotahiriwa, kuwepo kwa ugonjwa wa zinaa mwingine, mtu asiye na maambukizi anayeishi na mwenza mwenye maambukizi
Kinachoweza kuamsha Maambukizi ya virusi waliolala ni msongo wa mawazo, kutokupata vyakula vinavyoongeza kinga ya mwili na kuwa na wasiwasi na mawazo mengi
Uzalianaji wa VVU
VVU huingia kwa kujishikiza kwenye seli nyeupe za ulinzi wa binadamu kwa kutumia protini yake inayoitwa glycoprotein baada ya kuingia huachia jinomu yake ya RNA kwenye seli hiyo na hutumia kimeng'enya chake Reverse Transcriptase kutengeneza kopi ya jinomu ya DNA ya kirusi kutoka kwenye RNA baada ya hapo huweza kutengeneza DNA ya kirusi.
Baada ya DNA kutengenezwa, hufuatia utengenezwaji wa protini za kirusi. Protini hizi na DNA hujiunganisha na kuwa kirusi kingine kisha kuvamia chembe chembe nyingine za ulinzi dhidi ya magonjwa.
Chembe nyeupe zina [povamia na kirusi huharibiwa hivyo kinga ya mwili hushuka sana endapo havidhibitiwi.
Vipimo
Maambukizi ya UKIMWI hupimwa maabara kwa vipimo mbalimbali, ikiwa pamoja na kipimo cha haraka kwa kutumia kipimo cha HIV1 na 2 HIV Bioline na Endapo kitasoma una maambukizi kipimo kingine cha kutumia Uni gold kitafanyika
Matibabu
Kirusi huyu hana tiba ila zipo dawa ambazo hutolewa kwa mchanganyiko wa dawa zaidi ya moja ambazo hutumika kuzuia uzalianaji kirusi huyu mwilini au kumkinga mtu kupata maambukizi.
Je kuna chanjo ya kirusi cha UKIMWI
Mpaka sasa hakuna chanjo inayofahamika kufanya kazi, wanasayansi bado wanafanya tafiti mbalimbali ili kutengeneza chanjo ya kirusi huyu. Huenda mbeleni ikapatikana chanjo ya kirusi cha UKIMWI.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
Rejea zamada hii;
United republic of Tanzania.. Countryprofile. Https://www.who.int/hiv/HIVCP_TZA.pdf. Imechukuliwa 06.04.2020
Epidemiology of Disease Progression in HIV.http://hivinsite.ucsf.edu/insite?Page=kb-03-01-04#S2X. Imechukuliwa 6.04.2020 3.Hiv.
Mayoclinic. Https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/hiv-aids/diagnosis-treatment/drc-20373531.Imechukuliwa 6/4/2020
Webmdhiv. Https://www.webmd.com/hiv-aids/hiv-aids-screening.Imechukuliwa 6/4/2020
Medscapehiv. Https://www.medscape.com/viewarticle/893367.Imechukuliwa 6/4/2020
Healthlinehiv. Https://www.healthline.com/health/hiv-aids .Imechukuliwa 6/4/2020
Warren Revinson. Human Immunodeficiency Virus. Chapisho la 14, kurasa 566-568 ISBN 978-0-07-184574-8
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:15:36