Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Benjamin L, MD
16 Septemba 2021, 09:09:46
Kirusi chikungunya
Kirusi chikungunya ni kirusi anayesababisha homa ya homa ya chikungunya, moja kati ya magonjwa ya mlipuko yanayotokea sana kwenye ukanda wa sana kwenye ukanda wa tropiki kama Afrika na kusini mashariki mwa Asia pamoja na India.
Kirusi husababisha nini?
Kirusi hiki husababisha homa kali ya chikungunya.
Ugonjwa wa Homa ya chikungunya umeanza mwaka gani?
Kulingana na WHO, ugonjwa wa homa ya chikungunya ligundulika kwa mara ya kwanza Tanzania mwaka 1953 katika kijiji cha Swahili wilaya ya Newala. Ugonjwa huu ulianza kusambaa sehemu nyingine duniani na kwa sasa unapatikana karibia nchi 60 duniani kama vile Asia, Afrika, Ulaya na Amerika.
Genus na familia ya kirusi
Kirusi cha chikungunya ni kimoja wapo kwenye genus ya Alphavirus na familia ya Togaviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kuwa na strendi moja ya RNA.
Sifa za kirusi
Chikungunya ni kirusi chenye strendi moja ya RNA na kipo familia ya Togaviridae yenye sifa zifuatazo;
Wana strendi moja ya RNA
Wana umbile lenye pande 20 (ikosahedro)
Ganda lake la nje la seli limejifunga
Wana kipenyo cha urefu wa 70nm
Virusi kundi moja na Chikungunya
Virusi wengine walio kundi moja na kirusi chikungunya ni;
Kirusi cha Eastern Equine encephalitis
Kirusi cha Western equine encephalitis
Kirusi cha Venezudan equine encephalitis
Mtunzaji wa kirusi
Kirusi cha chikungunya hutunzwa na binadamu, nyani na mbu.
Uenezwaji wa kieusi
Kirusi cha chikungunya kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Mbu anapomng’ata mgonjwa wa homa ya chikungunya, hubeba kirusi huyu kwenye matumbo yake na mara anapomng'ata mtu mwingine humwachia kirusi huyu
Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ( huchangia kwa asilimia ndogo sana)
Kuongezewa damu ya mtu mwenye maambukizi ya kirusi chikungunya (huchangia kwa asilimia ndogo sana)
Dalili za maambukizi
Muda wa kuatema wa kirusi chikungunya ni huanzia siku tatu mpaka saba. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine pale tu dalili zinapoanza kuonekana ambazo ni;
Homa kali (102°f-105°f)
Uchovu
Kutetemeka
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya koo
Maumivu ya viungio vya mwili
Maumivu ya tumbo
Haja kubwa ngumu
Vipimo tambuzi
Vipimo vya kirusi cha chikungunya;
Picha nzima ya damu
RT-PCR
Kuotesha virusi
Kipimo cha Seroloji
Magonjwa mfanano
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na ugonjwa wa Homa ya chikungunya ni pamoja na;
Homa ya Dengue
Homa ya West nile
Maambukizi ya Kirusi Adenovirus
Homa ya Ebola
Homa ya Ross river
Homa ya Sindbis
Rubela
Mumps
Hepatitis B
Homa ya Lassa
Falciparum malaria
Matibabu
Hakuna matibabu rasmi kwa ajiri ya ugonjwa unaotokana na maambukizi ya kirusi chikungunya, hata hivyo ili kumsaidia mgonjwa anaweza fanyiwa mambo yafuatayo kutibu dalili;
Kuongezewa maji kwa njia ya mishipa au
Kunywa kama atakuwa kapungukiwa maji mwilini
Dawa za kutuliza
Mazoezi ya viungo vya mwili
Dawa zinazozuia au kupunguza michomo kinga
Kinga
Fanya yafuatayo ili uweze kujikinga na virusi vya chikungunya;
Dhibiti wa viumbe wanaoeneza kirusi chikunguka kama vile mbu.
Tumia dawa ya kuua mbu
Punguza au acha safari zisizo na lazima katika ukanda wa kitropiko au maeneo yenye hali ya juu ya maambukizi
Vaa nguo ndefu zinazofunika sehemu zote za mwili pia kofia na soksi
Funga milango na madirisha wakati wa jioni kuzuia mbu kuingia ndani
Je kuna chanjo ya kirusi mumps?
Chanjo kwa ajiri ya kirusi chikungunya haijatengenezwampaka sasa.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea zamada hii;
CDC. Chikungunya Virus. https://www.cdc.gov/chikungunya/transmission/index.html. Imechukuliwa 11/09/2021
MAYO CLINIC. Chikungunya virus. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/infectious-diseases/expert-answers/what-is-chikungunya-fever/faq-20109686. Imechukuliwa 11/09/2021
NCBI. Chikungunya Virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3085104/. Imechukuliwa 11/09/2021
MEDSCAPE. Chikungunya Virus. https://emedicine.medscape.com/article/2225687-treatment#d1. Imechukuliwa 11/09/2021
WHO. Chikungunya. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/chikungunya. Imechukuliwa 11/09/2021
Dubrulle M, et al. Chikungunya virus and Aedes mosquitoes: Saliva is infectious as soon as two days after oral infection. PLOS ONE, 2009. 4(6): p. e5895.
Silva M.M.O, et al. Concomitant Transmission of Dengue, Chikungunya, and Zika Viruses in Brazil: Clinical and Epidemiological Findings From Surveillance for Acute Febrile Illness. Clinical Infectious Diseases, 2018.
Goyal M, et al. Recent development in the strategies projected for chikungunya vaccine in humans. Drug Design Development and Therapy, 2018. 12: p. 4195-4206.
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021, 12:12:17