Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Benjamin L, MD
16 Septemba 2021 07:50:05
Kirusi Measles
Kirusi measles au kirusi cha surua ni moja ya kirusi kwenye familia ya Paramyxoviridae kinachosababisha ugonjwa wa surua. Surua ni moja kati ya magonjwa ya kuambukizwa, asilimia 90 ya maambukizi hutokea kama mtu ana magonjwa mengine au kinga yake ya mwili imeshuka.
Magonjwa ya kirusi
Kirusi measles husababisha homa kali na vipele vidogo vidogo mwilini yenye jina la surua kwa jina jingine 'ugonjwa wa measle'
Historia ya surua
Tafiti za kwanza kuhusiana na ugonjwa wa surua ziliandika karne ya 19 na mwaka 1757 francis home alilipoti kwamba surua ni ugonjwa wa kuambukizwa unaopatikana kwenye damu na mwaka 1990 ugonjwa wa surua ulilipotiwa Tanzania.
Familia ya kirusi measles
Kirusi cha surua ni kimoja wapo kwenye familia ya Paramyxoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na stranded RNA hasi pia husababisha homa kali na vipele vidogovidogo.
Sifa za kirusi
Kirusi Measles ni kirusi chenye strendi moja ya RNA hasi katika familia ya virusi vya paramyxoviridae yenye sifa zifuatazo;
Wana RNA moja
Huwana strendi moja ya RNA hasi
Ganda lake la njee la seli limejifunga
Wana kipenyo chenye urefu wa 150-300nm
Virusi wengine katika familia ya paramyxoviridae
Virusi wengine katika familia ya paramyxoviridae ni;
Kirusi Para influenza
Kirusi Mumps
Kirusi Respiratory syncytial
Kirusi hutunzwa na nani?
Kirusi measles hutunzwa na binadamu.
Kirusi measles kinaenezwa kwa njia gani?
Kirusi cha surua kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Kirusi husambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia matone ya chafya, kukohoa au ya pumzi
Wakati mwingine watu huambukizwa kiruzi measles kwa kugusana na vitu au sehemu yenye virusi kisha kujigusa puani au mdomoni.
Vihatarishi vya maambukizi
Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi measles ni;
Kutopata chanjo ya surua
Kuwa na kinga kidogo ya mwili( watoto)
Kutembelea ukanda wenye mlipuko
Kula lishe duni
Kuwa mjamzito
Kuwa na upungufu vitamin A
Dalili za maambukizi ya kirusi measles
Muda wa kuatema ni ndani ya siku saba hadi kumi na nne. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana. Dalili za ugonjwa wa surua ni;
Kuota vipele
Homa kali (nyuzi joto 40°c)
Mwili kudhoofika
Kukosa hamu ya kula
Macho kuwa mekundu na kuwasha
Macho kuvimba
Kikohozi
Kushindwa kuona vizuri
Vipimo
Asilimia kubwa ya vipimo hufanyika kutokana na hali ya ugonjwa, vinaweza kuwa;
Kipimo cha immunoglobulin G (1g G)
Kipimo cha immunoglobulin M (1g M)
RT-PCR
Kuotesha virusi
Picha nzima ya damu
Kipimo cha ufanyaji kazi wa ini
Magonjwa linganifu
Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na maambukizi ya measles ( ugonjwa wa surua) ni pamoja na;
Homa ya Dengue
Ugonjwa wa Kawasaki
Ugonjwa wa Serum
Sindromu ya mshitiko wa sumu
Rubella
Sepsis
Konjanctivatiz kali
Kuota upele wa dawa
Erythema infectiosum
Maambukizi ya kirusi Epstein-Barr
Homa ya uti wa mgongo
Matibabu
Matibabu hulenga dalili na madhara yanayoweza kujitokeza kama vile;
Mgonjwa anaweza kupata matibabu kwa kutibu dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa
Mgonjwa atapatiwa dawa kutibu au kinga maambukizi ya bakteria
Vitamin A
Kuongezewa maji
Je kuna chanjo ya kirusi cha Surua?
Chanjo ya kirusi measles ipo.na hutolewa kwa watoto wanapofikisha miezi tisa baada ya kuzaliwa na kisha anapofikisha miezi kumi na nne baada ya kuzaliwa.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
Rejea zamada hii;
CDC. Measles virus. https://www.cdc.gov/measles/cases-outbreaks.html. Imechukuliwa 13/09/2021
WHO. Measles virus. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/measles. Imechukuliwa 13/09/2021
NCBI. Measles virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK8461/. Imechukuliwa 13/09/2021
MEDSCAPE. measles virus. https://emedicine.medscape.com/article/966220-questions-and-answers. Imechukuliwa 13/09/2021
Measles Virus R. Cattaneo, et al. In Encyclopedia of Virology (Third Edition), 2008. https://www.sciencedirect.com/topics/neuroscience/measles-virus. Imechukuliwa 13/09/2021
Alison Margaret Kesson. Measles. Netter’s Infectious Diseases, 2012. https://www.sciencedirect.com/topics/neuroscience/measles. Imechukuliwa 13/09/2021
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:12:44