Mwandishi;
ULY CLINIC
Mhariri;
Dkt. Lugonda B, MD
2 Aprili 2020 18:44:40
Rino (Rhinovirus)
Kirusi Rino au rhinovirus, ni kirusi chenye RNA kutoka kwenye familia ya Picornaviridae. Kirusi huyu huongoza kusababisha homa ya baridi kwa binadamu kwa kuathiri sana pua na koo. Anapoingia mwilini Kirusi huyu huathiri sana pua na koo kwa kwa kuwa huzaliana sana kwenye maeneo hayo Kirusi Rino kinauwezo wa kuzaliana vizuri kwenye nyuzi joto la sentigrade 33kuliko nyuzi joto 37, hii ndio sababu kwanini huzaliana sana kwenye pua koo na konjaktiva ya macho kulio mfumo wa chini wa njia ya hewa. Kwa sababu pia kirusi huyu huwa hawapatani na tindikali, huuliwa na tindikali ya tumboni kama vikimezwa ukilinganisha na virusi vya enterovirus. Mwanzo ilifahamika kuwa kirusi huyu huambukizwa kwa njia ya hewa tu, kwa sasa inaongezewa kuwa kirusi huweza kuambukizwa kwa majimaji ya chafya au kikohozi yanayoanguka kwenye meza au vitu vingine ambavyo mtu akishika na kuweka mikono machoni au puani hupata maambukizi hayo.
Aina za kirusi Rino
Kuna zaidi ya aina 100 za kirusi huyu kutokana na seloroji, wingi huu unaelezea kwa nini kirusi huyu huongoza kusababisha homa ya mafua.
Mtunzaji wa kirusi Rino
Mtunzaji wa kirusi huyu ni binadamu na sokwe mtu.
Uambukizaji wa kirusi Rino
Kirusi rhinovirus kwa binadamu huambukiza zaidi wakati wa vuli na kwenye msimu wa baridi. Virusi huweza kubaki hadi masaa 3 nje ya mwili wa binadamu. Mara baada ya kirusi kuambukizwa, mtu huambukiza zaidi ndani ya siku 3 za kwanza. Hata hivyo kirusi rino huzaliana sana kwenye joto dogo.
Sifa za kirusi rhinovirus
Ni moja ya kirusi kidogo
Wana kipenyo cha 30 nautical miles hivi
Dalili za kuambukizwa na kirusi rhinovirus kwa watu wazima
Homa ya nyuzi joto Zaidi ya 38.5 degreeza sentigredi
Homa isiyoisha Zaidi ya siku mbili
Kuishiwa pumzi
Kutoa sauti za miruzi wakati wa kupumua
Koo kukauka na kuuma
Maumivu ya sinasi
Kuwashwa kwenye koo
Kutoka maji ya mafua kwenye pua au kuziba kwa pua
Kupiga chafya
Kikohozi
Maumivu ya kichwa
Dalili kwa Watoto wadogo
Homa nyuzi joto za sentigredi Zaidi ya 38
Homa inayopanda Zaidi ya siku mbili
Dalili ambazo zinakuwa kali au kutoisha
Kutoa sauti za miruzi akiwa anapumua
Maumivu ya masikio
Kuchoka sana
Kukosa hamu ya kula
Dalili zingine
Wakati mwingine dalili ya kirusi rhinovirus huweza kuambatana na;
Maumivu ya misuli
Uchovu
Mwili kulegea
Maumivu ya kichwa
Udhaifu wa misuli
Kupoteza hamu ya kula
Matibabu
Hakuna matibabu ya moja kwa moja ya kirusi huyu, chanjo haina mashiko kwa sababu kuna aina nyingi sana za serotaipu ya kirusi huyu.
Tafiti zinaonyesha asidi iliyochanganywa na sodiamu sulfate hukiua kirusi huyu. Hivyo matumizi ya sanitaiza na kupaka mikononi huzuia kueneza au kupata maambukizi kwa njia ya kushika vitu. Matumizi ya vitamini C yanazuia kwa kiasi homa ya baridi, dawa ya zinki glukonate hutumika kwenye matibabu ya homa hii lakini ufanisi wake haujulikani vizuri.
Kina nani wapo hatarini kwa maambukizi?
Waathirika zaidi na kirusi rhinovirus ni watoto wachanga, wazee, na watu wenye magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili.
Namna ya kujikinga na mamabukizi ya kirusi rino
Kuzuia huu uenezwaji wa kirusi rhinovirus kama vile kunawa mikono kwa nguvu na sabuni na maji kunaweza kusaidia kuzuia kuambukizwa. Kuepuka kugusa mdomo, macho na pua, zinaweza pia kusaidia katika kuzuia.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
Rejea zamada hii;
American Journal of Respiratory and Critical Care Medicine. Rhinovirus Infections More Than a Common Cold. https://www.atsjournals.org/doi/full/10.1164/rccm.200609-1387ED. Imepitiwa 1.04.2020
Warren levinson . Review of Medical microbiology and immunology chapisho la 14 pg 334, 348-349 3.Sexton DJ, et al. The common cold in adults: Diagnosis and clinical features. https://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 1.03.2020 4.Pappas DE, et al. The common cold in children: Clinical features and diagnosis. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 1.03.2020 5.Common colds: Protect yourself and others. Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/features/rhinoviruses/. Imechukuliwa 1.03.2020
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021 12:17:07