top of page

Mwandishi;

ULY CLINIC

Mhariri;

Dkt. Mangwella S, MD

17 Aprili 2020 16:10:56

Kirusi Varicella Zosta

Kirusi Varicella Zosta

Kirusi Varicella Zosta-VZV ni kirusi ambaye husababisha magonjwa ya tetekuwanga na mkanda jeshi, kirusi huyu yupo kwenye Familia ya virusi inayoitwa Herpes Viridae.


Familia ya herpesi viridae


Familia ya herpesi viridae ina virusi vingine ambao ni;


  • Kirusi Hepezi Simpeksi

  • Kirusi Cytomegalovirus

  • Kirusi Epstain Bar

  • Kirusi human hepezi

  • Kirusi kaposis Sakoma hepezi


Utunzaji wa kirusi


Kirusi huyu huwezwa kutunzwa na binadamu


Sifa za kirusi VZV


  • Anayo kapsidi ya nuklia inayozunguka kiini cha ndani

  • Huwa na strend mbili za jinomu ya DNA

  • Anayo jalada la protini ambalo hutenganisha kapsidi kutoka kwenye lipidi

  • Hustahimili kwa sana kwenye maeneo ya joto

  • Hutoa immunoglobulin G (IgG), IgM, na IgA ambayo hujishikiza kwenye protini ya kirusi


Ugonjwa unaosababishwa na VZV


Kirusi huyu huweza kupelekea magonjwa ya tetekuwanga na mkanda jeshi


Dalili kwa mgonjwa wa tetekuwanga


Kuotwa vipele vinavyowasha na kuuma kuanzia siku ya 10 hadi 21 baada ya kupata Maambukizi na baadae huisha baada ya siku 10 Kabla ya vipele dalili zifuatazo huonekana;


  • Homa

  • Kukosa hamu ya kula

  • Maumivu ya Kichwa

  • Uchovu wa mwili


Jinsi kirusi anavyoenezwa;


Huenezwa kwa njia ya kugusana na mtu aliyeathirika au kuvuta hewa yenye matone kutoka kwa mtu aliyekohoa na mwenye Maambukizi.


Dalili za mgonjwa mwenye mkanda wa jeshi (Hepezii Zosta au shingozi)


Mkanda wa jeshi huathiri upande mmoja wa sehemu ya mwili, huambatana na;


  • Maumivu

  • Vipele ambavyo huuma na kuchoma

  • Vinahisika kwa haraka ukivigusa

  • Vipele vyekundu ambavyo huanza siku chache baada ya maumivu

  • Kuwashwa


Baadhi ya watu pia huweza kupata;


Homa

Maumivu ya kichwa

Kuchoka


Kundi hatarishi kupata mkanda jeshi


  • Watu wenye umri mkubwa zaidi ya miaka 50

  • Watu wenye kinga ya mwili ndogo kama wenye Maambukizi ya HIV

  • Wagonjwa wanaotumia dawa za kansa


Jinsi ya kujikinga na kirusi VZV


Kujikinga na tetekuwanga watoto wanahitaji kupewa chanjo baada ya kuzaliwa, hata hivyo chanjo haimaanishi kuwa hautapata bali hupunguza makali pale utakapopata.

Vipimo vya VZV


Vipimo vikuu vinavyofanyika ni;


Polymerase chain reaction (PCR) kutambua vimelea kwenye (Malenge, magamba na, upele)


Matibabu ya VZV


Dawa zifuatazo hutumika kutibu


  • Acyclovir

  • Valacyclovir


ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

Orodha kuu


Rejea zamada hii;

  1. Medscape.VaricellaZosterVirus.https://emedicine.medscape.com/article/231927-overview. Imechukuliwa 17/4/2020 

  2. NCBI.VaricellaZosterVirus.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2919834/. Imechukuliwa 17/4/2020

  3. WebMd.VarivellaZosterVirus.https://www.webmd.com/skin-problems-and-treatments/shingles/qa/what-is-varicella-zoster. Imechukuliwa 17/4/2020

  4. CDC.ChickenPox.https://www.cdc.gov/chickenpox/hcp/index.html. Imechukuliwa 17/4/2020

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 12:14:35

bottom of page