Mwandishi;
Dkt. Mercy M, CO
Mhariri;
Dkt. Mangwella S, MD
16 Septemba 2021, 11:27:01
Kirusi zika
nyingi huwa hasababishi ugonjwa mkali na dalili zake kuu ni homa, maumivu ya kichwa, misuli, maungio ya mwili na macho mekundu.
Kirusi husababisha nini?
Kirusi zika husababisha homa ya wastani na wakati mwingine homa kali inayoambatana na upele mwilini hasa maeneo ya kifua uso, viganja na miguu.
Msambazaji wa kirusi
Kirusi cha ziko husambazwa na mbu jike aina ya Aedes hasa Anopheles Aegyptindiye.
Kirusi cha zika kilianza mwaka gani
Tafiti zinaonesha kuwa kirusi cha zika kilianza kuonekana kwa mara ya kwanza kwa nyani mwaka1947 huko Uganda na mwaka 1948 virusi hawa walionekana kwa mbu aina ya Aedes na ripoti ya kwanza kwa binadamu ilionekana mwaka 1952 uganda na Tanzania. Milipuko mingine ya kirusi zika imewahi ripotiwa baada ya miaka hiyo kwenye nchi zingine za Afrika, Americas, Asia na bahari ya pasifiki.
Familia ya kirusi
Kirusi cha zika ni kimoja wapo kwenye familia ya Flaviviridae, Virusi katika familia hii hufahamika kwa kusababisha Homa kali.
Sifa za kirusi
Kirusi Zika ni ni aina ya kirusi chenye RNA moja katika familia ya virusi vya Flaviviridae yenye sifa zifuatazo;
Hupatikana kwenye wadudu jamii ya arthropodi
Huwa na umbile la uzi
Ukuta wake umefungwa
Huwa warefu
Wana RNA moja
Virusi vya familia flaviviridae
Baadhi ya virusi vingine kwenye familia ya Flaviviridae ni;
Kirusi cha homa ya njano
Kirusi Tick-borne encephalitis
Kirusi West Nile
Kirusi dengue
Kirusi chikungunya
Mtunzaji wa kirusi
Kirusi cha Zika hutunzwa na binadamu, m'bu jike aina ya Aedes na nyani.
Uenezaji w akirusi
Kirusi cha Zika kinaenezwa kwa njia zifuatazo;
Kung’atwa na mbu jike aliyebeba virusi kutoka kwa mgonjwa wa zika
Kujamiana bila kinga (virusi hawa wameonekana kwenye shahawa za mwanaume)
Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Kwa kuongezewa damu
Dalili za ugonjwa wa Zika
Kipindi cha kuatema cha kirusi zika ni kati ya siku 3 hadi 14. Mtu hawezi kusambaza ugonjwa mpaka pale dalili zitakapoonekana. Dalili za ugonjwa zake huwa pamoja na;
Homa kali
Uchovu
Maumivu ya kichwa
Kukosa hamu ya kula
Upele mwilini hasa kifuani, usoni, viganja na miguu
Dalili zingine ni;
Hisia za maumivu nyuma ya macho
Kuvimba mitoki
Kuharisha
Kuvimba miguu na mikono
Kuumizwa na mwanga
Kikohozi
Uchovu
Maumivu ya mgongo
Vidonda vya aphthous
Kutokwa na jasho
Magonjwa linganifu
Magonjwa yanayofanana dalili na ugonjwa wa zika ni pamoja na;
Malaria
Ebola
Homa ya njano
Homa ya chikungunya
Influenza
Measles
Rubella
Ugonjwa wa Corona virus diseases
Maambukizi ya Streptococcal kundi A
Vipimo tambuzi
Picha nzima ya damu
Kipimo cha PCR ya kirusi Zika
Kipimo cha Immunoglobulin M (1gM)
Kipimo cha Immunoglobulin G (1gM)
Kipimo cha Nucleic Acid Amplification (NAATs)
Kuotesha kirusi
Matibabu
Hakuna dawa maalumu inayotumika kutibu maambukizi ya kirusi Zika na hivyo tiba hulenga kupunguza au kuondoa dalili zinazojitokeza na huhusisaha;
Kupata muda mwingi wa kupumzika
Kunywa maji ya kutosha
Kutumia dawa za maumivu kama Acetaminophen(paracetamol) kwa kuzuia homa na maumivu
Matumizi ya dawa jamii ya antihistamine kwa ajiri ya vipele na muwasho
Kinga na chanjo
Ili kujikinga na maambukizi ya kirusi zika, fanya yafuatayo;
Dhibiti vimelea wanaoeneza kirusi zika kama vile mbu kwa;
Kupuliza ndai au kupaka dawa ya kuua mbu wakati wa jioni
Punguza au acha safari zisizo za lazima katika maeneo yenye hali ya juu ya maambukizi
Vaa nguo ndefu zinazofunika sehemu zote za mwili, tumia pia kofia na soksi ndefu
Usiache milango na madirisha wazi isipokuwa kama kuna wavu katika dilisha ambapo unaweza acha madirisha wazi
Tumia kinga wakati wa kujamiana.
Je kuna chanjo ya kirusi cha zika?
Hapana! mpaka sasa bado hakuna chanjo iliyogunduliwa kwa kwa ajili ya kirusi zika.
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii
​
Rejea zamada hii;
WHO. Zika virus. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/zika-virus. Imechukuliwa 13/09/2021Â
MEDSCAPE. Zika virus. https://emedicine.medscape.com/article/2500035-guidelines. Imechukuliwa 13/09/2021Â
CDC. Zika. https://www.cdc.gov/zika/about/index.html. Imechukuliwa 13/09/2021 A.D.T. Barrett, S.C. Arboviruses: alphaviruses, flaviviruses and bunyaviruses .https://www.sciencedirect.com/topics/neuroscience/zika-virus. Imechukuliwa 13/09/2021Â
CDC. About Zika. https://www.cdc.gov/zika/about/index.html. Imechukuliwa 13/09/2021Â
K Gorshkov, et al. Zika Virus: Origins, Pathological Action, and Treatment. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6330993/. Imechukuliwa 13/09/2021Â
Syeda Sidra Kazmi, et al. A review on Zika virus outbreak, epidemiology, transmission and infection dynamics. https://jbiolres.biomedcentral.com/articles/10.1186/s40709-020-00115-4. Imechukuliwa 13/09/2021
Imeboreshwa;
27 Septemba 2021, 12:11:46