top of page

Mwandishi:

Dkt. Mercy M, CO

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

25 Septemba 2021 08:25:50

kirusi mumps-ulyclinic

Kirusi human parainfluenza

Kirusi human parainfluenza ni kirusi kinachosababisha maambukizi katika mfumo wa upumuaji hasa kwa watoto. Maambukizi hayo ni kama mafua yenye homa, laryngotracheobronchitis , bronkolaitiz na nimonia.


Kirusi husababisha nini?


Kirusi hiki husababisha maambukizi kwenye mfumo wa upumuji.


Kirusi human parainfluenza kimeanza mwaka gani?


Tafiti za kwanza kuhusiana na kirusi Human parainfluenza kilionekana mwaka 1950.


Kirusi Human parainfluenza kipo katika Familia gani?


Kirusi Human parainfluenza ni kimoja wapo kwenye genus ya Respirovirus na familia ya Paramyxoviridae. Virusi katika familia hii hufahamika kwa kuwa na strendi moja ya RNA hasi pia husababisha maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.


Sifa za kirusi


Human parainfluenza ni kirusi cha strendi moja ya RNA hasi. Kirusi hiki ni familia ya virusi vya paramyxoviridae.Familia hii ina sifa zifuatazo;


 • Wana strendi moja ya RNA

 • RNA yake ni hasi

 • Ukuta wake wa njee ya seli umejifunga

 • Wana kipenyo cha 150-300nm

 • Wana mwili ambao haujajigawanya


Virusi wengine katika familia ya paramyxoviridae


 • Measles virus (surua)

 • Mumps virus

 • Kirusi respiratory syncytial


Genera za kirusi


Kirusi Human parainfluenza kimegawanyika katika genera mbili ambazo ni;


 • Respirovirus

 • Rubulavirus


Mtunzaji w akirusi


Kirusi hutunzwa na nani?


Kirusi Human parainfluenza hutunzwa na binadamu.


Uenezwaji wa kirusi


Kirusi Human parainfluenza kinaenezwa kwa njia gani?


Kirusi Human parainfluenza kinaenezwa kwa njia zifuatazo;


 • Kusambaa kutoka mtu mmoja kwenda mtu mwingine kupitia matone ya chafya, makohozi au hewa

 • Kugusa vitu au sehemu yenye virusi na kujigusa puani au mdomoni

 • Kuwa karibu na mtu mwenye maambukizi ya kirusi human parainfluenza


Vihatarishi


Vihatarishi vya kupata maambukizi ya kirusi Human parainfluenza ni;


 • Watoto wenye lishe duni.

 • Mkusanyiko mkubwa wa watu.

 • Mtoto anayekosa maziwa ya mama

 • Wenye upungufu vitamin A

 • Mazingira

Dalili


Muda wa kuatema ni ndani ya siku moja hadi saba. Mtu mwenye ugonjwa huu huweza kumuambukiza mwingine pale tuu dalili zinapoanza kuonekana. Dalili za kirusi human parainfluenza ni;


 • Joto kali la mwili (Homa)

 • Kikohozi

 • Coryza

 • Stridor

 • Retraction

 • Kupumua harakaharaka

 • Irritability


Vipimo vya utambuzi


 • Immunoglobulin G (1g G)

 • Immunoglobulin M (1g M)

 • Kuotesha virusi

 • Picha nzima ya damu

 • Picha ya shingo na kifua


Magonjwa yanayofanana


Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na kirusi Human parainfluenza ni pamoja na;


 • Bronkaitiz

 • Kiusi Corona

 • Kupaliwa

 • Nimonia

 • Kirusi Respiratory syncytial

 • Adenovirus

 • Influenza

 • Nimonia ya Chlamydial

 • Coxsackieviruses

 • Maambukizi ya mycoplasma

 • Pediatric epiglotaitiz

 • Usaha kwenye retrofalinjo


Matibabu ya kirusi Human parainfluenza


Matibabu hulenga dalili zile zinazoonekana kwa mgonjwa yanayohusisha

 • Dawa kwa ajiri ya maambukizi ya bakteria

 • Vitamin A Suppliment

 • Maji ya kutosha kwa njia ya kunywa au mishipa

 • Dawa za kushusha homa (Panadol)

 • Dawa jamii ya corticosteroid na nebulizer kwa ajiri ya kupunguza michomo kinga na uvimbe kwenye mfumo wa hewa kama imeshukiwa

 • Oxygen kama kiwango chake cha oxygen chini ya kawaida

 • Kutolewa nguo kwa mtoto ili apate hewa ya kutosha


Kinga


Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi


 • Ukiwa umeugua, usitoke nyumbani, isipokuwa pale unapohitaji huduma ya matibabu.

 • Funika mdomo na pua kwa kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya au fanya hivyo ndani ya kiwiko chako na ukioshe baadaye.

 • Tupa kifaa kilichotumika kwenye takataka.

 • Nawa mikono yako mara kwa mara

 • Epuka msongamano wa watu


Je kuna chanjo ya kirusi Human parainfluenza ?


Mpaka sasa hakuna chanjo ya kirusi Human parainfluenza .

Imeboreshwa,

25 Septemba 2021 08:25:50

ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktrari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii;

Kupata ushauri zaidi na tiba wasiliana na daktari wa ULY CLINIC bofya mawasiliano yetu chini ya tovuti hii au kwa kubofya pata tiba.

Rejea za mada hii;

 1. CDC. Human parainfluenza  virus. https://www.cdc.gov/human parainfluenza /index.html. Imechukuliwa 23/09/2021.

 2. NCBI. Human parainfluenza  virus. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7171724/. Imechukuliwa 23/09/2021.

 3. Medscape. Human parainfluenza  virus. https://emedicine.medscape.com/article/224708-overview. Imechukuliwa 23/09/2021.

bottom of page