top of page

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

​

Imeandikwa 04.12.2020

​

Amenorrhea (Amenorea)

​

Amenorea ni tatizo la kutoona damu ya mwezi au kukatika kwa damu ya hedhi kwa mwanamke aliyekwishavunja ungo. Tatizo hili husababishwa na sababu mbalimbali za mabadiliko ya homoni au magonjwa ndani ya mwili. Kuna sababu za kifiziolojia ya kawaida zinazoweza kuleta amenorea mfano kupata ujauzito, kunyonyesha baada ya kujifungua na kuwa kwenye kipinid komahedhi.

​

Magonjwa yanayoweza kusababisha kutoona damu ya hedhi ni,

  • Matatizo ya maumbile ya mfumo wa kizazi

  • Magonjwa ya tezi za endokrini, (haipothalamas, pituitari, adreno, thairoidi, na tezi zingine)

  • Ugonjwa sirosisi

  • Kuferi kwa ovari

  • Kurithi madhaifu ya kijeni

​

Amenorea inaweza kuwa ya kuzaliwa au ya inayotokea baada ya kuzaliwa, amenorea ya kuzaliwa ni pale ambapo mwanamke hajavunja ungo kwa kuona damu ya mwezi mpaka kufikia umri wa miaka 16 na amenorea baada ya kuzaliwa ni ile ambayo hutokea endapo mwanamke aliyekuwa anaona hedhi hajapata hedhi ya mwezi kwa muda angalau miezi mitatu na kuendelea.

​

Endelea kusoma zaidi kwa kubonyeza hapa

​

Muulize daktari wako endapo una dalili hii kwa ushauri, uchunguzi na tiba

​

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri vipimo na tiba bonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii

​

Imeboreshwa, 5.8.2022

​

Rejea za mada hii

​

  1. Ulyclinic maswali na majibu kwa wateja

  2. Amenorrhea. Pubmed. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/5885258/. Imechukuliwa 04.12.2020

  3. Welt CK, et al. Etiology, diagnosis and treatment of secondary amenorrhea. http://www.uptodate.com/home.Imechukuliwa 04.12.2020

  4. Welt CK, et al. Etiology, diagnosis and treatment of primary amenorrhea. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 04.12.2020

  5. Bope ET, et al. Conn's Current Therapy. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2013. http://www.clinicalkey.com.Imechukuliwa 04.12.2020

  6. DeCherney AH, et al. Current Diagnosis & Treatment Obstetrics & Gynecology.11th ed. New York, N.Y. http://www.accessmedicine.com/resourceTOC.aspx?resourceID=788. Imechukuliwa 04.12.2020

  7. Goldman L, et al. Goldman's Cecil Medicine. 24th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2012. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 04.12.2020

bottom of page