top of page

Imeandikwa na madaktari wa uly clinic

Kupunguza uzito kwa njia ya chakula

Utangulizi

Chakula chenye wanga kidogo ni kile kinachodhibiti matumizi ya wanga unaopatikana kwenye nafaka, mboga za majani na matunda yenye wanga. Vyakula hivyo hutilia mkazo matumizi ya vyakula vyenye protini kwa wingi na mafuta. Zipo aina kadhaa za vyakula vyenye wanga kidogo, aina hizo ni lazima hutumika kulingana na ushauri wa daktari na afya ya mtu.

Madhumuni ya matumizi ya chakula chenye wanga kidogo

Matumizi ya chakula chenye wanga kidogo malengo yake makuu ni kupunguza uzito. Baadhi ya aina ya vyakula vyenye wanga kidogo huwa na faida zingine za kiafya mbali na kupunguza uzito ikiwa pamoja na kukuondoka katika kihatarishi cha kupata kisukari aina ya 2 na magonjwa mengine ya kimetabolik

Maelezo ya ziada kuhusu chakula chenye wanga kidogo

Kama jina linavyosema, chakula chenye wanga kidogo humdhibiti mtu kula wanga kwa wingi, wanga ni kirutubisho kinachotoa nishati. Wanga hupatikana kwenye vyakula vingi na vinywaji kama sukari, maziwa, matunda, unga, na mbegu za mimea pamoja na maharagwe na mboga za majani

Watengenezaji wa vyakula visivyo asili hutumia wanga katika vyakula wanavyotengeneza ulio kwenye mfumo wa sukari au unga. Mfano wa vyakula vyenye wanga ni mkate, chapati, keki, glukosi, soda na vinywaji vingi.

Mwili hutumia wanga kama chanzo kikuu cha nishati, wanga huvunywa vunjwa tumboni na kuwa sukari kisha hufyonzwa na kuingia kwenye mishipa ya damu ili kutumika kwenye chembe hai za mwili. Vyakula halisi vya wanga mfano unga wa mahindi usiokobolewa n.k humeng”enywa taratibu kwenye utumbo wa binadamu hivyo huchangia sukari kiasi kidogo kwenye mfumo wa damu kuliko vyakula ambavyo si halisi, mfano glukos, keki, soda n.k. hata hivyo vyakula halisi huwa na faida nyingi mbali na ile ya kukupa sukari kidogo, kwa kuwa huwa na virutubisho na madini.

Sukari inapofyonzwa na kuingia kwenye mfumo wa damu husababisha kongosho kuzalisha homoni ya insulin kwa wingi, homoni hii hufanya kazi ya kuwezesha chembe hai za mwili zitumie sukari kutoa nishati, nishati hii husaidia chembe hai kuweza kufanya kazi zake mfano, moyo uendelee kusukuma damu, ubongo uendelee kufikiria, misuli ikusababishie uweze kutembea au kukimbia n.k. kiwango cha sukari iliyozidi mahitaji ya mwili katika damu hubadilishwa na homoni hii kuwa mafuta na kuhifadhiwa katika ngozi maeneo ya tumbo, makalio na mapaja, kifuani n.k

Malengo ya kutumia vyakula vyenye wanga kidogo ni kuwezesha kongosho isizalishe homoni hii kwa wingi, matokeo yake,  mwili huanza kutumia mafuta yaliyohifadhiwa katika tumbon.k  kuzalisha nishati na mwishowe mtu kupungua uzito endapo atatumia chakula chenye wanga kidogo au kisicho na wanga.

Faida zingine za kutumia vyakula vyenye wanga kidogo ni nini?

Mbali na kupunguza uzito vyakula vyenye wanga kidogo vinaweza  kuleta faida zifuatazo;

Huweza kuimarisha au kukinga mwili dhidi ya magonjwa ya kimetaboliki, kisukari, presha(shinikizo la juu la damu) na magonjwa ya moyo. Bila shaka kila aina ya chakula kinachokufanya usile wanga kwa wingi hukukinga dhidi ya magonjwa ya moyo na kisukari.

Vyakula vyenye protini kwa wingi na ikiwa protini hii imetoka kwenye samaki, wanyama jamii ya ndege, kuku, mimea jamii ya kunde na vyakula ambavyo kobolewa/havijachakatuliwa mfano kunde, mboga za majani, matunda halisi, vyakula vya mbegu maziwa yasiyo na mafuta mengi, hushauliwa kutumika na huleta afya njema kwa binadamu.

Maudhi/Madhara ya kutumia vyakula vyenye wanga kidogo

Kama ukiacha ghafla kula vyakula vyenye wanga unaweza kupata madhara yafuatayo yanayodumu kwa muda mfupi

  • Maumivu ya kichwa

  • Harufu mbaya kinywani

  • Udhaifu wa mwili

  • Maumivu ya misuli

  • Mwili kuchoka

  • Harara kwenye ngozi

  • Choo kigumu au kuharisha.

Hata hivyo baadhi ya vyakula vinavyo dhibiti kabisa kutumia wanga  au kutumia kwa kiasi kidogo sana, huweza pelekea mtu kukosa madini na vitamin muhimu na madhara yake ya muda mrefu huwa ni kupungukiwa madini na vitamin, kupoteza uimara wa mifupa, matatizo ya tumbo na  uwezekano wa kuwa na magonjwa sugu.

Nani hashauriwi kutumia chakula hiki?

Chakula chenye wanga kidogo hakishauriwi kwa watoto wadogo ambao wapo chini ya umri wa miaka 13 kwa sababu vyakula hivi hukosa madini na vitamin muhimu kwa ajili ya ukuaji wao. Kumbuka watoto hawa bado wanakuwa na hawajakomaa hivyo wanahitaji kula vyakula hivi ili wakue vizuri.

Kwa ushauri ongea na daktari wako au tutafute kupitia namba za simu zilizo chini ya tovuti yetu au kwa kupitia email zetu.

Endapo utazuia kiwango cha wanga kuwa chini ya miligramu 20 kwa siku basi mtu anaweza kuingia kwenye kipindi kinaitwa ketoacidosis kilicho elezewa kwenye Makala hii kwa undani Zaidi.

Unaanzaje kuuambia mwili wako upunguze uzito kuchoma mafuta yaliyo kwenye mwili?

Acha kula au punguza vyakula vya wanga

Je madhara ya kuacha kula wanga ni nini?

Madharaya kuacha kula wanga kabisa ni Kupanda kwa kemikali ya ketone kwenye damu, Ketone huwa haina madhara kwenye mwili

Watu wengi wanaojaribu kupunguza uzito, hujaribu kufanya mambo mengi kama mazoezi, kutokula baadhi ya vyakula nakadhalika. Baadhi ya njia huwasaidia kupunguza uzito lakini baadae hujirudia kwa na huwa zaidi ya uzito wa awali. Hii ni kwa sababu wanachokifanya huwa ni cha muda tu, kinachohitajika hapa ni mabadiliko ya maisha ya kufanya muda wote. Bila shaka mabadiliko haya yanahusisha mtu kuendelea kula vyakula halisi na asilia.

Hata hivyo kula vyakula asilia kama vyakula visivyokobolewa, vyakula vyenye mafuta kwa wingi, vyakula vyenye sukari kwa wingi n.k  inaweza isisaidie kupunguza uzito hata kidogo endapo unakula vyakula hivyo kwa wingi kwa siku.

Endapo mwili wako unatunza mafuta kwa kawaida, mtu huongezeka uzito kiasi, endapo kuna tatizo kwenye mchakato wa kutunza mafuta basi mtu huweza kuongezeka uzito kupita kiasi.

Kwa kawaida mwili huwa na kumbukumbu la agizo la kiasi gani cha mafuta kitunzwe kwa ajili ya matumizi yake. Endapo kuna mabadiliko yanataka kutokea kwenye kiasi hii, mwili huanza kupambana ili kufanya kiasi hiko kisipungue. Hi indo maana kama ukifanya mazoezi sana unapata njaa sana na endapo utakula chakula chenye nishati kidogo mwili utarekebisha uchakatuaji wa kazi zake ili kuendana na nishati iliyopo.

 

Kwanini kujali kuhusu agizo la kiasi cha mafuta ya kutunzwa?

Matatizo mengi ya uzito kupita kiasi hutokanana kuharibika kwa agizo hili. Endapo mwili utakaidi agizo hili basi utunzwaji wa mafuta unaweza kuongezeka na kuwa mkubwa na hivyo kuleta uzito uliopitiliza. Kwa maana nyingine uzito kupita kiasi unatokana na kukiukwa kwa agizo la kiasi cha mafuta kinachotakiw akutuzwa, na kila mbinu ya kupunguza uzito ambayo itakuwa endelevu inatakiwa kufanya agizo hili litimizwe.

Tunafahamu kwamba mtu huongezeka uzito kwa sababu anakula sana vyakula vyenye nishati nyingi, kwanini mtu anakula sana? Jibu ni kwa sababu mfumo unaotimiza agizo la mafuta yahifadhiwe kiasi mwili unahitaji hupokea agizo la kuhifadhi mafuta mengi yanayozidi kiasi kinachohitajika na mwili.

Ili kupunguza uzito, unahitaji kurudisha mfumo huu uendano la agizo la awali la mwili kutunza mafuta kulingana na agizo la asili la kiasi gani cha mafuta kitunzwe. Hili haliwezekani tu kwa njia ya mazoezi na kula vyakula vyenye nishati kidogo, kwa sababu mwili utapambana iwezekanavyo ili kupinga mafuta kupungua mwilini, pia ni vigumu kupingana na njaa kwa kuwa mwili utakufanya uhisi njaa na ule, matokeo yake ni kuongezeka uzito

Namna gani utarekebisha na kuendana na agizo la awali la kiwango cha mafuta kinachotakiwa kutunzwa? Na Namna gani ya kuufunza mwili wako uanze kuunguza mafuta?

Njia muhimu ya kufanya ni kuufanya mwili kupandisha kiwango cha kenone kwenye damu

Ketone ni kemikali inayozalishwa mwili unapounguza mafuta(kutumia mafuta kwa ajili ya kuzalisha nishati. Kama ukila kiwango kikubwa cha wanga hutawahi kuingia kwenye kipindi cha kuwa na ketone kwa wingi kwenye damu. Kwa maana nyingine mwili utatumia sukari iliyo kwenye wanga kama chanzo cha nishati.

Je kuwa na kiwango cha ketone nyingi kwenye damu ni hatari?

Kuwa na kiwago kikubwa cha ketone kwenye damu si hatari endapo unakula vyakula vyenye nishati nawenye virutubisho muhimu. Ketone huzalishwa endapo mtu atafunga kula chakula, katika kipindi hiki cha mfungo mwili hubadilisha mafuta kuwa ketone ili utumie kama nishati kuupa mwili nguvu, ketone huwa haidhuru misuli. Wataalamu wengi huchanganya kati ya ketogenesisi(uzalishaji wa ketone kutokana na kufunga kula chakula na) ketoacidosis ambapo mwili hupata ketone na asidi kwa wingi kwenye damu, hali hii ni hatari sana kwa binadamu. Endapo unapata ketone kwa ajili ya kufunga kula chakula huna haja ya kuogopa endapo unakula wanga kidogo sana na mboga za majani na matunda.

Mwisho, kula vyakula vinavyosababisha ktone mwilini vimekuwa vikipingwa na wataalamu wa afya na umuhimu wake katika kupunguza uzito unafahamuka. Vyakula hivi huwa na wanga kidogo sana na husababisha mwili uanze kutumia mafuta yaliyotunzwa kama nishati.

Binadamu hajaumbiwa kutumia nishati kutoka kwenye wanga tu bali anaweza kupata nishati kutoka kwenye ketone na ndo maana baadhi ya maandiko matakatifu yanataka watu wafunge kwa maombi, sio tu kwa ajili ya kupata Baraka bali kuupa mwili afya njema kwa kufanya mwili uweze kutumia nishati mfumo wa ketone ambayo hutoka kwenye mafuta. Vyakula vyenye kusababisha ketone kutumika kwa wingi ni vile vyenye wanga kidogo sana kama

Endapo mwili wako unapata kiwango cha wanga kidogo mfano miligramu 50 hadi 80 kwa siku,ketone zitaanza kuzalishwa kwa wingi. Hali hii ikifanyika kwa wakati kadhaa mwili unazoea na kuendana na hali hii ya kutumia ketone. Kiwango hiki cha wanga kinatosha na pia unaweza kuongeza madini(madini kalisi-magadi) na virutubisho vingine kama mboga za majani na matunda.

Utakapofika katika uzito unaohitaji kuwa nao, na kutohitaji kupungua zaidi, unaweza kuongeza kiwango cha wanga na kufika miligramu 100 hadi 150 kwa siku na kuendelea, hii itakusaidia kufanya mwili upate agizo jipya kuhusu kiwango cha mafuta kinachotakiwa kutunzwa.

Huhitaji kupima kiwango cha chakula au nishati unachotumia, bila shaka unaweza kufanya hivi, achana na vyakula vya mbegu, sukari na matunda matamu. Ukipata hamu ya kula vyakula hivyo basi kula vyakula vyenye mafuta safi(saturated fat) kama mafuta ya nazi, mafuta kutoka ngozi ya wanyama, siagi, na mafuta ya nguruwe.

Mafuta haya yamekuwa yakipingwa vibaya kutumika kwamba yanaongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo lakini tafiti za hivi karibuni zimeonyesha mchango wa mafuta haya kwamba hulinda moyo na faida zingine nyingi

Mara baada ya kufikia uzito unaohitaji, jipe wakati wa kula matunda matamu kama embe chungwa n,k na vyakula vya mbegu zilizoandaliwa vema, mizizi, na vyakula jamii ya kunde.

Ukiwa kipindi hiki cha kuendelea na uzito unaotaka, utajikuta kwamba unakula vyakula vya asili na visivyosindikwa, vyakula vyenye mafuta ya asili, vyakula vilivyochachishwa kwa njia ya asili na vyakula vibichi(fresh) vyakula visivyo na sukari. Kiasi halisi cha nyama, mboga za majani na mafuta unachohitaji hutegemea mahitajiyako na uchaguzi wako, lakini kumbuka hutakiwi kurudi kuwa na uzito uliokuwa nao awali.

Bonyeza hapa kusoma kuhusu mfano wa mpango wa chakula unaoweza kukupunguza uzito kwa kukupatia nishati unayotakiwa kupata kwa siku

Imeboreshwa mara ya mwisho 18.06.2020

utangulizi
madhumuni
faida wanga kidogo
madhara wanga kidogo
ufunze mwili
ketoni/ketoacidosis
bottom of page