top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

Shinikizo la damu la juu (HAIPATENSHENI)

Shinikizo la damu la juu ni hali inayotokea endapo presha ndani ya mishipa ya damu imezidi kiwango cha kawaida kinachofanhamika kiafya. Kuzidi kwa presha hii kunaweza kusababishwa na hali na magonjwa mbalimbali. Ili tuweze kujua kuhusu shinikizo la damu la juu ni vema kwanza kujua aina za shinikizo la damu la juu. Kwenye maka hii na tovuti hii neno shinikizo la damu la juu linatumika kwa jina jingine kama haipatensheni.

mgonjwa huitwa ana shinikizo la damu la juu(haipatensheni) endapo presha yake imezidi 139/79mmHg.

Tatizo la Hapatensheni limegawanyika katika makundi makuu mawili. Haipatensheni ya awali na haipatensheni ya sekondari.

Haipatensheni ya awali kisababishi mara nyingi huwa hakifahamika na huchangia kwa asilimia 90 hadi 95 ya ugonjwa wa haipatensheni kwa binadamu haswa watu wazima wenye umri kati ya miaka 35 na kuendelea.

 

Haipatensheni ya awali huhusianishwa na sababu za kimazingira au za kiasilia kama ifuatavyo;

 

 • Kurithi- inaonekana kwamba watu wengi wenye shinikizo la damu baadhi huwa na historia hii kwenye familia zao lakini  urithishwaji huu bado haueleweki vizuri. Kuna utafiti umefanyika na kuonesha watoto mapacha wanaozaliwa wote wanaweza kupata shinikizo la damu la juu kwa asilimia 33-57%

 • Uzito mkubwa kupita kiasi(obeziti)

 • Ugonjwa wa kisukari

 • Magonjwa ya moyo

 

Haipatensheni ya sekondari linachangia kwa asilimia 5-10 kusababisha shinikizo la juu la damu. Zipo sababu za moja kwa moja zinazofahamika kusababisha haipatensheni hii. Watu wanaopata shinikizo hili la damu wengi huonekana kuwa na umri chini ya miaka 35.

Shinikizo la juu la damu linalozidi la  180/120 linaweza kugawanywa tena katika makundi mawili ambayo ni;

 

 • Hypertensive urgency (Shinikizo la damu la juu linalohitaji matibabu ya haraka)

  • Shinikizo hili haliambatani na ishara ya kuharibika kwa ogani ndani , mgonjwa huenda hospitali akiwa anajihisi vibaya na anapopimwa anakuwa na shinikizo la juu sana. Matibabu ya shinikizo hili huchukua siku mbili hadi tatu kwa matumizi ya dawa za kumeza mgonjwa akiwa amelazwa wodini, au nyumbani chini ya usimamizi wa daktari.

 • Hypertensive emergency (Shinikizo la damu linalohitaji matibabu ya dharura)

  • Aina hii huwa inajitokeza na dalili za uhalibifu wa organi mbalimbali mwilini kama vile macho(kushindwa kuona vema), ubongo( mabadiliko ya kiakili/tabia ya mtu), figo (kutokukojoa au kukojoa mkojo kidogo sana), mapafu(maumivu ya kifua) na moyo(maumivu ya moyo ya ghafla na maumivu ya kifua), mapafu (maji kwenye mapafu) na ujauzito( kifafa cha mimba), ubongo( damu kuvia kwenye ubongo) na moyo (mshituko wa moyo na kifo)

  • Mgonjwa anahitaji matibabu ya dharura kwenye chumba cha watu mahutui yani ICU na matibabu yake yanahusisha kushusha shinikizo hili ndani ya saa 1 au 2 kwa dawa za mishipa ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea na kuokoa maisha.

Je kunamahusiano ya vyakula na mfumo wa maisha na kutibu shinikizo la damu la juu?

 

Ndio kuna mahusiano makubwa ya shinikizo la damu na chakula. Pengine mtu mwenye dalili za kuanza kupata shinikizo au mwenye shinikizo anashauriwa kubadili mfumo wa maisha yake kama ifuatavyo;

 • Punguza kula vyakula vya mafuta kwa wingi hasa vyenye kolestro mbaya  ili kuzuia magonjwa ya moyo

 • Tumia chumvi kiasi kinachoshauriwa kiafya kulingana na hali yako.

 • Ongeza kula vyakula vya matunda na mboga mboga

 • Kula vyakula vyenye madini ya kalisiamu kwa wingi kama viazi vitamu, ndizi n.k

 • Acha kuvuta sigara

 • Fanya mazoezi kwa angalau  dakika 30 kila siku utazuia ongezeko la uzito na magonjwa ya moyo

 • Puguza uzito

 • Punguza msongo wa mawazo

 • Kuwa na tabia ya kupima shinikizo la damu kila mwezi ili kujua shinikizo lako la damu. Itakusaidia kutambua mapema kama likibadilika

 • Tumia dawa kila siku endapo umeanzishiwa dawa za kushusha shinikizo la damu ili kuepuka madhara yake.

 • Mwone dakitara mara unapopata tatizo lolote ambalo hulielewi

Soma hapa kuhusu kushusha shinikizo la damu pasipo kutumia dawa

Endelea kusoma kuhusu Hatua, Aina , Visababishi, Vipimo na matibabu na ushauri wa daktari kwa kubonyeza hapa

Ili kuendelea kusoma makala hii unahitaji uwe na email tu

 

Wasiliana na daktari wako endapo umeona una dalili yoyote ile katika maelezo haya kwa ushauri na tiba

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba zaidi kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa

Imeboreshwa 09.12.2020

bottom of page