Vyakula vinavyoongeza uzalishaji wa maziwa ya mama
Imeandikwa na madaktari wa uly clinic
Uzalishaji wa maziwa ya mama hutegemea vitu vingi ikiwa pamoja na namba ya idadi unavyonyonyesha ama kukamua maziwa, na kiasi cha chakula unachokula na saikolojia ya mama kwa wakati huo. Ingawa wamama wengi huzalisha kiwango cha maziwa cha kutosha lakini hakuna kipimo kinachoonyesha maziwa yako yanatoka kwa wingi kiasi cha kumtosha mtoto.
Kuna baadhi ya vyakula vya asili kama pilipili manga n.k vinaweza kuongeza uzalishaji wa maziwa endapo vikitumiwa kwa wingi. Pilipili manga ni mojawapo ya kiungo kinachoongeza uzalishaji wa maziwa.
Vyakula vingiene
Baadhi ya vyakula huongeza uzalishaji wa maziwa, hivyo huwa na faida wakati na kipindi cha kunyonyesha .
-
Viazi vitamu,
-
Tangawizi,
-
Pilipili manga,
-
Mboga za majani-kama spinachi, kabeji,sukuma wiki
Radha ya maziwa yanayozalishwa huwa haibadiliki sana, hata hivyo hutegemea aina ya chakula wakati mwingine, mfano umekula chakula chenye pilipili manga, maziwa yanaweza kuwana na radha kama unayopata kutokana na kula pilipili manga
Soma hapa wakati gani baada ya kujifungua utarajie mwili kutoa maziwa kwa ajili ya kichanga. Kwa ushauri na tiba ongea na daktari wako au tutafute kwenye namba zilizo chini ya tovuti hii
Toleo la 3
Imeboreshwa 8/1/2019