top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY-Clinic

 

Maana ya Chunusi

 

Chunusi ni tatizo la ngozi linalotokea endapo vitundu katika ngozi vimezibwa  kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa. Chunusi mara nyingi huonekana usoni, shingoni, kifuani na kwenye mabega. Ingawa matibabu mazuri yapo, chunusi huweza kuwa sugu na kuendelea kutokea. Chunusi hutokea na kupotea na mara inapopotea huota  sehemu nyingine ya ngozi.

 

Chunusi hutokea sana kwa vijana wenye umri wa miaka kumi na ushehe, asilimia 70 hadi 87 ya vijana wa umri huu hupata chunusi. Kwa sasa vijana wadogo zaidi hupata chunusi na idadi inaongezeka zaidi.

Ikitegemea ukubwa wa tatizo, chunusi humsababisha mtu ajihisi kuwa na mwonekano na kisaikolojia na pia huacha mkovu kwenye ngozi. Endapo chunusi itatibiwa mapema utaepuka hali ya kisaikolojia na kuharibika kwa ngozi yako.

 

ULY clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kiafya pekeyako.

Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa ushauri na tiba kwa kupiga namba za simu au bonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

 

Soma makala ingine kuhusu chunusi kwa kubonyeza hapa

au endelea kusoma makala hii kwa kubonyeza hapa

bottom of page