top of page

Huduma za matibabu mtandaoni kwa wateja wa VIP na wasio VIP

"Kama umeletwa kwenye ukurasa huu baada ya kujaza fomu (dodoso) ya kutoa taarifa za ugonjwa wako ili daktari aweze kuelewa hali yako, basi umefika hapa makusudi ili kuendelea na hatua inayofuata ya kupata huduma kutoka kwetu. â€‹Tafadhali kamilisha hatua hii ili uweze kuendelea na mchakato wa kuwasiliana na daktari, kupata ushauri wa kitaalamu, pamoja na mapendekezo ya dawa au matibabu yanayofaa kwa hali yako."

​

​Huduma hizi zinakupa ushauri wa kitabibu na kuandikiwa dawa mtandaoni mara moja, kwa kuzingatia viwango vya kimatibabu na maadili ya kitaaluma.

​

Neno “mara moja” katika maelezo haya linamaanisha kuwa utapatiwa huduma wakati huu uliofika tu. Ikiwa utahitaji huduma tena wakati mwingine, utahitajika kujiunga upya ili kupata ushauri na huduma nyingine.

​

1.0. Huduma za mara moja tu

​​

1.1. HUDUMA KWA WASIO VIP – Tsh 30,000/=(Ongezeko la asilimia 50)

 

Madaktari wanaopatikana

Unaweza kupata huduma kutoka kwa madaktari wa:

  • Ngozi

  • Mifupa

  • Mionzi

  • Watoto

  • Magonjwa ya wanawake

  • Magonjwa ya wazee

  • Magonjwa ya akili

  • Meno

  • Masikio, pua na koo

  • Upasuaji

  • Magonjwa ya kawaida

  • Lishe

  • Macho

​

Huduma unazopata mara moja kwa tatizo:

  • Ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa daktari

  • Maelezo ya tatizo lako kulingana na historia na dalili

  • Kupendekezewa vipimo vinavyohitajika

  • Usomaji wa vipimo na kuandikiwa dawa kwa walioandikiwa vipimo wakati wa huduma ya kwanza

  • Kuandikiwa cheti cha dawa (prescription)

  • Maelekezo sahihi ya matumizi ya dawa

  • Ufafanuzi wa majibu ya vipimo (maabara/mionzi)

  • Ushauri wa dawa sahihi kwa tatizo lako

  • Vidokezo muhimu vya kiafya kulingana na hali yako

 

Mambo yasiyojumuishwa kwa Huduma hii:

  • Kupewa dawa

  • Kufanyiwa vipimo

  • Kufanyiwa upasuaji

  • Kupigiwa simu

  • Kutembelewa na daktari/mhudumu

  • Kulazwa

​

Malipo

Lipa Tsh 20,000 kupitia MPESA namba
📞 +255 752 954 281

 

Baada ya malipo:
Jaza fomu iliyo chini ya ukurasa → Tuma → Kisha wasiliana na whatsapp namba  +255 621 122 578  kwa matibabu.

​

Muda wa Huduma (Si kwa VIP)

🕒 Saa 12:30 mchana – 09:00 jioni (1230–1530hrs)
📅 Kila siku isipokuwa Jumapili (mapumziko)

​

Iwapo Huna uwezo wa kulipa

Wasiliana nasi kupitia namba zetu. Utaulizwa maswali ya uthibitisho na ukithibitika kuwa unahitaji msaada, utapewa utaratibu maalumu wa huduma. Pia unaweza kusoma kupitia kurasa ya utaratibu wa huduma zetu kwa maelezo zaidi ya namna ya kupta huduma hii

​

1.2. HUDUMA ZA VIP – Tsh 55,000/=(Ongezeko la asilimia 37.5)

Huduma za VIP hukupa upendeleo wa muda, majibu ya haraka, na muda mrefu zaidi wa kuwa na mtaalamu wa Afya.

 

Madaktari Wanaopatikana

(Orodha ni ile ile kama ya wasio VIP)

​

Huduma unazopata mara moja kwa tatizo:

  • Ushauri wa moja kwa moja na daktari

  • Utambuzi wa tatizo kulingana na dalili na historia

  • Ushauri wa vipimo vinavyohitajika

  • Usomaji wa vipimo na kuandikiwa dawa kwa walioandikiwa vipimo wakati wa huduma ya kwanza

  • Kuandikiwa cheti cha dawa (prescription)

  • Ufafanuzi wa vipimo (maabara/mionzi)

  • Maelekezo ya matumizi ya dawa

  • Vidokezo vya kiafya kulingana na hali yako

​

Huduma zisizojumuishwa kwenye kifurushi hiki:

  • Kupewa dawa

  • Kufanyiwa vipimo

  • Kufanyiwa upasuaji

  • Kupigiwa simu

  • Kutembelewa na mhudumu

  • Kulazwa

​

Malipo

Lipa Tsh 50,000 kupitia MPESA namba:
📞 +255 752 954 281

 

Baada ya malipo: Jaza fomu iliyo chini ya ukurasa → Tuma → Kisha wasiliana na whatsapp namba  +255 621 122 578  kwa matibabu.

 

Muda wa Huduma za VIP

  • 🕒 Jumatatu – Ijumaa: 2:00 asubuhi – 5:00 usiku (0800–1400hrs)

  • 🕒 Jumamosi: 3:00 asubuhi – 5:00 usiku (09:00–23:00)

  • Jumapili: Mapumziko

​

1.3. HUDUMA ZA SAA 24 – Tsh 80,000/=(Ongezeko la asilimia 60)

Huduma hii imeandaliwa kwa watu wanaohitaji ushauri wa kitabibu na huduma ya daktari muda wowote, bila kufungwa na ratiba maalumu ya huduma za kawaida au VIP. Huduma hii hukupa kipaumbele cha kupata huduma nje ya muda wa kawaida wa kazi, kulingana na upatikanaji wa daktari.

​

Madaktari Wanaopatikana

(Orodha ni ile ile kama ya huduma za kawaida na VIP)

​

Huduma unazopata mara moja kwa tatizo:

  • Ushauri wa moja kwa moja na daktari

  • Utambuzi wa tatizo kulingana na dalili na historia

  • Ushauri wa vipimo vinavyohitajika

  • Usomaji wa vipimo na kuandikiwa dawa pale inapofaa

  • Kuandikiwa cheti cha dawa

  • Ufafanuzi wa vipimo vya maabara au mionzi

  • Maelekezo sahihi ya matumizi ya dawa

  • Vidokezo muhimu vya kiafya kulingana na hali yako

 

Huduma zisizojumuishwa kwenye kifurushi hiki:

  • Kupewa dawa

  • Kufanyiwa vipimo

  • Kufanyiwa upasuaji

  • Kutembelewa na daktari au mhudumu

  • Gharama nyingine za matibabu zinazoweza kuhitajika

  • Kulazwa

​

Malipo

Lipa Tsh 80,000/= kupitia MPESA namba:

📞 +255 752 954 281

Baada ya malipo: Jaza fomu iliyo chini ya ukurasa → Tuma → Kisha wasiliana na WhatsApp namba +255 621 122 578 kwa huduma ya kitabibu.

​

Muda wa Huduma

🕒 Muda wowote – Saa 24

Huduma hii haina ratiba maalumu ya siku au saa. Unaweza kuomba huduma wakati wowote, ikiwemo nje ya muda wa kawaida wa huduma, usiku, wikendi na siku za mapumziko. Huduma hutolewa kulingana na upatikanaji wa daktari wakati wa kuomba huduma.

​

Muhimu

Huduma hii ni kwa ajili ya ushauri na huduma ya kitabibu mtandaoni na si huduma ya dharura. Ikiwa una hali inayohitaji matibabu ya haraka au inayohatarisha maisha, tafadhali nenda hospitali au kituo cha afya chenye huduma za dharura mara moja.

​

2.0. Huduma za mwaka mmoja – mara 10 tu kwa mwaka

Huduma hizi zimeandaliwa kwa mtu anayehitaji kupata ushauri na matibabu mtandaoni mara nyingi katika kipindi cha mwaka.

​

Kwa kulipa ada ya mwaka, unaweza kupata huduma za kitabibu mara 10 tu ndani ya mwaka mmoja(miezi 12), kulingana na aina ya kifurushi unachochagua.

​

Muhimu: Kila kifurushi cha mwaka ni cha mtu mmoja tu aliyesajiliwa. Hakiwezi kutumiwa, kugawanywa au kuhamishwa kwa mtu mwingine.

​

2. 1. WASIO VIP – Tsh 120,000/= kwa mwaka (ni punguzo la asilimia 60)

  • Huduma ni mara 10tu  kwa mwaka

  • Muda wa huduma ni ule ule wa huduma za kawaida za wasio VIP

  • Huduma na aina za madaktari ni kama zilivyoelezwa kwenye kifurushi cha wasio VIP hapo juu

  • Kifurushi ni cha mtu mmoja tu

​

2. 2. VIP – Tsh 220,000/= kwa mwaka (ni punguzo la asilimia 60)

  • Huduma ni mara 10 tu kwa mwaka

  • Kipaumbele na muda wa huduma ni kama ilivyo kwenye kifurushi cha VIP hapo juu

  • Huduma na aina za madaktari ni kama zilivyoelezwa kwenye kifurushi cha VIP

  • Kifurushi ni cha mtu mmoja tu

 

2. 3. HUDUMA ZA SAA 24 – Tsh 320,000/= kwa mwaka (ni punguzo la asilimia 60)

  • Huduma ni mara 10 tu kwa mwaka

  • Upatikanaji wa huduma saa 24 ni kama ilivyoelezwa kwenye kifurushi cha huduma za saa 24 hapo juu

  • Huduma na aina za madaktari ni kama zilivyoelezwa kwenye kifurushi cha saa 24

  • Kifurushi ni cha mtu mmoja tu

​

Muhimu

Huduma za mwaka hazijumuishi gharama za kupewa dawa, kufanyiwa vipimo, kufanyiwa upasuaji, kulazwa hospitalini, matibabu ya ana kwa ana au huduma nyingine ambazo tayari zimeelezwa kuwa hazijumuishwi kwenye vifurushi husika.

 

Huduma hizi ni za mwanachama aliyesajiliwa pekee. Malipo ya mwaka hayaruhusu ndugu, rafiki, mwenza au mtu mwingine kutumia huduma kwa jina la mwanachama.​

​​​

Usiri na Ubora wa Huduma

ULY Clinic inafuata miiko, maadili, na viwango vya kitabibu.

 

Taarifa zako zote ni siri kati yako na daktari. Kwa kujaza fomu hii unathibitisha kukubaliana na Vigezo na Masharti ya huduma.

​

Kurasa ya Fomu(Dodoso) za huduma

Baada ya kulipia huduma bofya hapa kwenda kwenye kurasa ya fomu za kupata huduma kama

Jina lako kamili

Mkoa ulipo

Namba ya simu uliyofanyia malipo

Nambari ya muamala wa malipo

bottom of page