top of page

ULY CLINIC

22 Machi 2025, 14:41:31

Edema ya ghafla ya mapafu

Edema ya ghafla ya mapafu

Dalili za edema ya mapafu ni zipi?


Katika edema ya mapafu ya ghafla, mgonjwa huonyesha matumizi makubwa ya misuli ya ziada kwa kupumua, pamoja na kupumua kwa shida, kupumua haraka, na kutoweza kulala bila kuinua kichwa.


Dalili na ishara zinazohusiana ni:

  • Sauti za mpasuko mapafuni (krepitation krako) na miruzi,

  • Kikohozi chenye makohozi ya rangi ya waridi na yenye povu,

  • Kutotulia na wasiwasi,

  • Mapigo ya moyo haraka na sauti ya moyo ya ziada (sauti ya Galop kwenye ventriko),

  • Ngozi baridi, yenye unyevunyevu, na rangi ya bluu kwenye ngozi kutokana na ukosefu wa oksijeni

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

22 Machi 2025, 14:41:31

Rejea za mada hii

ULY CLINIC

bottom of page