top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

1 Machi 2021 08:34:33

Ishara ya macho ya mdori

Ishara ya macho ya mdori

Ishara ya macho ya mdori kwa lugha tiba 'Doll's eye sign, ni ishara inayomaanisha kuwepo kwa tatizo kwenye mfumo wa fahamu wa kati.


Ishara hii hutabulika endapo mtu akigeuzwa kichwa kuelekea kushoto au kulia, macho yake hayatafuata uelekeo wa kichwa na hivyo yatakuwa yameangalia pembeni. Angalia picha kwa uelewa zaidi.


Ishara hii hutumika kupima ufanyaji kazi wa mshipa wa fahamu inayoanzia kwenye ubongo yenye jina la cranial nerve nambari 3, 6, na 8, kupima reflex arc na kazi za shina la ubongo kwa ujumla.


Visababisha


  • Matumizi ya baadhi ya dawa

  • Kufa kwa sehemu ya ubongo kutokana na kukosa damu au virutubisho

  • Uvimbe katika mfumo wa kati wa fahamu

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

7 Februari 2022 19:31:48

Rejea za mada hii

1)Evan Dishion et al. Doll's Eyes. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK551716/. Imechukuliwa 01.03.2021

2)Tarek Sharshar, et al. Brainstem responses can predict death and delirium in sedated patients in intensive care unit https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/21532477/. Imechukuliwa 01.03.2021

3)Moshe Snir, et al. Suppression of the oculocephalic reflex (doll's eyes phenomenon) in normal full-term babies. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/20450249/. Imechukuliwa 01.03.2021

4)R V Wong, et al. Using the oculocephalic reflex to assess effective retrobulbar anesthesia. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/8515952/. Imechukuliwa 01.03.2021

bottom of page