Imeandikwa na ULY CLINIC
1 Machi 2021, 09:26:48
Maumivu wakati wa hedhi (Dysmenorrhea)
Dismenorrhea ni maumivu ya tumbo wakati wa hedhi, huathiri zaidi ya asilimia 50 ya wanawake walio kwenye kipindi cha kuona hedhi.
Maumivu haya huweza kuja na kuondoka, kuwa butu au ya kuchoma kama mshale. Mara nyingi huambatana na maumivu makali ya kunyonga au kubana yanayosambaa kuelekea kwenye njia ya haja kubwa au mapajani, na huweza kutangulia kabla ya kuona damu au wakati damu inatoka.
Visababishi
Adenomysosis
Kusinyaa kwa tundu la shingo ya kizazi
Endometriosis(kutungishwa cha chembe za endometria nje ya mfuko wa kizazi)
Magonjwa ya michomo kwenye nyonga (PID)
sindromu ya komahedhi
Maumivu yasiyokuwa nasababu za awali
Fibraoid ndani ya mfuko wa kizazi
Matumizi ya vipandikizi vinavyowekwa ndani ya kizazi
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
7 Februari 2022, 19:30:16
Rejea za mada hii