top of page

Imeandikwa na ULY CLINIC

20 Septemba 2021 16:37:58

Urethraitiz

Urethraitiz

Urethritiz hutokana na michomo kwenye mrija wa urethra kama matokeo ya shambulio la kinga ya mwili kwenye vimelea wa maradhi walio kwenye mrija huo haswa wale wanaosababisha magonjwa ya zinaa.


Dalili zake ni;


  • Kutokwa na uchafu mwembamba na msafi kama kamasi au

  • Kutokwa na uchafu mzito kama usaha


Dalili zignine ni

  • Kusita kukojoa

  • Kushindwa kuzuia mkojo

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Maumivu wakati wa kukojoa

  • Muwasho kwenye tundu la mkojo

  • Hisia za kuungua kwenye tundu la mkojo


Kisababishi kikuu cha urethraitiz ni maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwenye mrija urethra. Bakteria hao ni kama vile;


  • Chlamydia trachomatis

  • Neisseria gonorrhoeae


Vimelea weingine wanaoweza kuchangia lakini kwa asilimia chache ni;


  • Mycoplasma genitalium

  • Trichomonas vaginalis

  • Herpes Simplex virus

  • Treponema pallidum

  • Neisseria meningitides

  • Ureaplasma urealyticum

  • Ureaplasma parvum

  • Candida species


Visababishi


Kuna visababishi vingine ambavyo havihusiani na maambukizi pia vinaweza kupelekea tatizo la urethraitiz kama vile;


Uharibifu kwenye njia ya mkojo kutokana na kuwekewa mpira au kifaa tiba kwenye njia ya mkojo au sababu zingine


Uchokozi kwenye njia ya mkojo kutokana na

  • Kuingiziwa mpira wa mkojo na kukaa muda mrefu

  • Msuguano kwenye njia ya mkojo kutokana na kuvaa nguo za kubana au shinikizo wakati wa kujamiana

  • Kufanya kazi za kuongeza shinikizo kwenye njia ya mkojo kama vile kuendesha baiskeli

  • Matumizi ya sabuni, poda na viuaji manii vyenye uchokozi kwenye ngozi na mrija wa mkojo

  • Kuingia koma hedhi na kutokuwa na kiwango cha estrogen ya kutosha ( kwa wazee)

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba kupitia namba za simu au kwa kubonyeza 'Pata tiba' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

7 Februari 2022 19:16:21

Rejea za mada hii

NHS. Overview. Non-gonococcal urethritis. https://www.nhs.uk/conditions/non-gonococcal-urethritis/. Imechukuliwa 20/09/2021

JOHN R. BRILL, MD, MPH. Diagnosis and Treatment of Urethritis in Men. https://www.aafp.org/afp/2010/0401/p873.html. Imechukuliwa 20/09/2021

NCBI. Urethritis. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537282/. Imechukuliwa 20/09/2021

Young A, Toncar A, Wray AA. Urethritis. 2021 Jul 29. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing; 2021 Jan–. PMID: 30725967.

bottom of page