top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

30 Juni 2021 18:47:19

Hedhi baada ya kutoa mimba
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Hedhi baada ya kutoa mimba

Hedhi baada ya kutoa mimba katika Makala hii inaamaanisha sifa za damu ya hedhi ya kwanza na ya pili baada ya mimba kutoka yenyewe au kutoa kwa njia ya dawa au kusafisha kizazi.


Ni lini damu ya hedhi hureje baada ya kutoa mimba?


Baada ya kutoa mimba, baadhi ya wanawake hedhi yao hurejea mara baada ya kusafishwa kizazi au baada ya wiki chache toka mimba imetoka.


Kwa kawaida inachukua wiki 4 hadi 6 kwa hedhi kurejea, hata hivyo kurejea kwake hutegemea kiwango cha homoni za ujauzito ambazo hutofautiana kati ya mwanamke mmoja na hutegemea umri wa ujauzito.

Endapo homoni za ujauzito zitaendelea kuwepo kwenye damu baada ya kutoa mimba, hedhi ya kwanza itachelewa kutokea.


Itakapopita wiki zaidi ya sita bila kuona hedhi, unapaswa kupima ujauzito ili kuhakikisha kama unao kabla ya kuonana na daktari wako kwa uchunguzi.


Muda wa hedhi kudumu baada ya kutoa mimba


Hedhi ya kwanza baada ya kutoa mimba huweza kuwa fupi kuliko kawaida yako baadaya kutoa mimba kwa njia ya kusafishwa kizazina huwa ndefu endapo mimba imetolewa kwa dawa. Utofauti ni kutokana na mabadiliko ya homoni lakini mzunguko wa hedhi utarejea kama kawaida baada ya muda kupita.


Sifa za hedhi ya kwanza baada ya kutoa mimba


Hedhi ya kwanza inayotokea baada ya kutoa mimba huweza kuwa na damu ningi na nzito kuliko kawaida haswa kwa waliotoa mimba kwa njia ya dawa ukifanannisha na njia ya kusafishwa kizazi, hii ni kwa sababu mji wako wa uzazi unatoa tishu zote za mimba zilizo ndani ya kizazi na taratibu, na baaadhi ya wakati huambatana na kupitisha mabonge ya damu iliyoganda.


Hedhi ya baada ya upasuaji huwa nyepesi mwanzoni na hurejea kawaida baada ya miezi michache.


Aina za ute unaotoka ukeni baada ya kutoa mimba


Ni kawaida baada ya mimba kutoka kutokwa na ute wa rangi nyekundu ukifuatiwa na na pinki na baadaye njano au ute wa rangi ya maji n.k. licha ya kuwa na rangi tofauti na kawaida wiki kadhaa baada ya kutoa mimba, ute unaotoka haupaswi kuwa na harufu mbaya kama ya samaki kwani harufu hiyo huashiria maambukizi.


Dalili za hedhi ya kwanza baada ya kutoa mimba


Dalili za hedhi huwa kama za kawaida lakini wiki za kwanza huambatana na maumivu ya kunyonga ya tumbo la chini yanayoendelea kupungua kwa ukali siku zinavyoenda. Dalili zingine zinazoweza kutokea ni;


  • Tumbo kujaa gesi

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya titi yakiguswa

  • Maumivu ya misuli

  • Kupoteza mudi nzuri

  • Uchovu


Matumizi ya pedi baada ya kutoa mimba


Unaruhusiwa kuvaa pedi gani?

Unaruhusiwa kuvaa pedi za kinamama waliojifungu na kuepuka pedi za kuchomeka ndani ya uke baada ya mimba kutoka au kutoa mimba.


Lini nitarejea kuanza vaa pedi za kawaida?

Baafa ya wiki mbili kupita toka mimba imetoka au baada ya damu kukatika, unaweza anza vaa pedi za kawaida ambazo ulikuwa unatumia.


Hedhi ya pili baada ya kutoa mimba


Wanawake wengi hupata hedhi ya pili ya kawaida baada ya kutoa mimba, hata hivyo wengi wao wanaweza kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka kwa miezi michache. Mzunguko unaweza kuwa mrefu au mfupi na damu inaweza kuwa kidogo au nyingi ikitegemea njia ambayo ulitumia kutoa mimba. Wakati wa hedhi ya pili, unaruhusiwa kutumia pedi ya aina yoyote kama ulizokuwa unatumia awali


Mambo ya kufanya baada ya kutoa mimba


Unapaswa kufahamu kwamba, baada ya kutoa mimba kuna uweekano mkubwa sana wa kupata mimba utakaposhiriki ngono, ni vema wakati huu ukatumia kinga au ukaacha kushiriki kabisa mpaka mzunguko wako wa hedhi utakapokuwa vema. Unaweza kutumia njia za uzazi wa mpango pia, lakini hizi hazitakukinga kupata maambukizi ya magonjwa ya zinaa.


Unashauriwa kuacha shiriki ngono kwa wiki kadhaa mpaka mzunguko wako wa kawiada utakaporejea kwa sababu kipindi baada ya kutoa mimba mlango wa kizazi huwa wazi na hupelekea uwezekano mkubwa wa kuruhusu maambukizi kupenya na kuingia ndani ya mji wa uzazi haswa endapo damu bado zinatoka.


Kipindi gani salama kujamiana baada ya kutoa mimba?


Inashauriwa kitaalamu kukaa kwa muda wa angalau wiki mbili au zaidi bila kujamiana baada ya kutoa mimba.


Hata hivyo WHO na baadhi ya madaktari na wanashauri usubirie mpaka pale damu itakapokata ndipo ushiriki ngono, hii ni kwa sababu utapunguza hatari ya kupata maambukizi kwenye mfuko wa uzazi. Damu inapokuwa inaendelea kutoka, hii inamaanisha mlango wa uzazi upo wazi, hivyo maambukizi yanaweza ingizwa ndani ya kizazi wakati huu endapo utajamiana. Maambukizi yanaweza kuwa ya vimelea vya magonjwa ya zinaa au yasiyo ya zinaa.


Wakati gani unapaswa kuonana na daktari haraka?


Unapaswa kuonana na daktari haraka endapo unapata dalili zifuatazo za hatari baada ya kutoa mimba;


  • Unajaza pedi kubwa zaidi ya mbili kwa kila saa

  • Unatokwa na mabonge makubwa ya damu mithiri ya limao

  • Una maumivu makali sana ya tumbo au mgongo

  • Maumivu ya tumbo hayaishi na dawa ulizopewa

  • Unapata homa zaidi ya nyuzijoto 38 za selishazi

  • Unatetemeka

  • Unatokwa na uchafu unaonuka ukeni

  • Unatokwa na uchavu wa njano au kijani ukeni

  • Endapo hedhi yako haijarejea kwa zaidi ya wiki nane toka mimba imetoka

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021 04:52:32

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Abortion and bleeding. healthcentre.org.uk/abortion/abortion-bleeding.html. Imechukuliwa 30.06.2021

2. After an abortion. soc.ucsb.edu/sexinfo/article/after-abortion. Imechukuliwa 30.06.2021

3. After an abortion. bpas.org/abortion-care/after-an-abortion/. Imechukuliwa 30.06.2021

4. Mayo Clinic Staff. (2018). Medical abortion. mayoclinic.org/tests-procedures/medical-abortion/about/pac-20394687. Imechukuliwa 30.06.2021

5. NHS. When is it safe to have sex after an abortion?. https://www.nhs.uk/common-health-questions/sexual-health/when-is-it-safe-to-have-sex-after-an-abortion/. Imechukuliwa 30.06.2021

6. Counselling for Maternal and Newborn Health Care: A Handbook for Building Skills.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK304195/. Imechukuliwa 30.06.2021

bottom of page