top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, MD

18 Novemba 2020 10:56:49

Hisia za uvimbe ndani ya koo
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Hisia za uvimbe ndani ya koo

Hisia za uvimbe ndani ya koo


Ni hisia zinazotokea pale mtu anapohisi kuwa kuna uvimbe ndani ya koo haswa wakati anameza mate wakati kiuhalisia hakuna uvimbe wowote ule ndani ya koo. Hali hii huwa haizuii mtu kula chakula wala kunywa maji na huweza kutokea kwa mtu wa jinsi na umri wowote ule, hata hivyo watu wa umri wa kati (miaka 50 na kuendelea) huathiriwa Zaidi


Kisababishi halisi cha tatizo hili hakifahamiki, mwathirika wa tatizo hili huweza kufanyiwa vipimo mbalimbali ili kujihakikishia kwamba hana shida nyingine ambayo ni ya hatari ndani ya mwili, endapo hakuna shida yoyote ile mgonjwa hupewa tumaini kuwa tatizo haliwezi kumdhuru na haliwezi kusababisha tatizo jingine lolote mwilini.


Kisababishi

Kisababishi halisi hakifahamii, hata hivyo baadhi ya mambo ambayo yanasemekana kuchangia ni;


  • Madhaifu ya mijongeo ya misuli ya koo

  • Kucheua tindikali (GERD)

  • Msongo wa mawazo

  • Kumeza mara kwa mara au kukausha koo


Madhaifu ya mijongeo ya misuli ya koo

Inasemekana kuwa kuna shida kwenye mijongeo ya misuli ya koo inayohusika na umezaji. Misuli hii huwa haisinyai na kutanuka kwa mpangilio asili ili kuruhusu umezaji wa chakula na maji. Tatizo huonekana sana pale mtu anapomeza mate kwa sababu baadhi ya misuli huwa haifanyi kazi katika mpangilio mzuri, na wakati wa kumeza chakula misuli mingi ya koo huamshwa na ubongo hivyo ni mara chache sana mtu akahisi kuwa kuna kitu kwenye koo kwakuwa hufanya kazi katika mpangilio mzuri.


Kucheua tindikali (GERD)

Kucheua tindikali kutoka tumboni pia huchangia kupata hisia za kuhisi uvimbe kwenye koo wakati wa kumeza mate. Tindikali hizi huchoma na kusababisha misuli ya koo kushindwa kuwa na mpangilio katika ufanyaji kazi wake.


Msongo wa mawazo

Msongo wa mawazo husababisha tatizo hili au kufanya liwe na hali mbaya Zaidi


Kuchuruzika kwa majimaji nyuma ya koo

Kuchuruzika kwa majimaji nyuma ya koo kutoka puani pia kunaweza kusababisha tatizo hili likawa na dalili mbaya Zaidi


Kumeza mara kwa mara au kukausha koo

Magonjwa ambayo yanafanana na tatizo hili ama yanaweza kuchanganywa na tatizo hili ni;


  • Cricopharyngeal webs

  • Myasthenia gravis

  • Myotonia dystrophica

  • Achalasia

  • autoimmune myositis

  • Pharyngitis

  • Tonsilitis

  • Sinusitis

  • Uvimbe kwenye mediastinum unaosababisha mgandamizo kwenye esophagus


Dalili


Dalili mara nyingi hutokea na kupotea.


  • Mara nyingi mgonjwa huhisi hisia za kuwa na uvimbe ndani ya koo, mbele ya shingo na anaweza kusema kwamba unatembea kwenda juu au chini ya shingo;

  • Uwezo wa mtu huweza kumeza na kunywa huwa ni kama kawaida

  • Dalili mara zote hupoa mtu akila chakula au kunywa maji

  • Mara zote hakuna dalili za hisia ya maumivu ya koo wakati wa kumeza

  • Dalili huonekana zaidi wakati wa kumeza mate


Kumbuka

Hisia za uvimbe kwenye koo wakati haupo huwa si dalili ya saratani wala haina hatari ya kuwa saratani kwa mbeleni. Tatizo hili hutofautiana na tatizo la shida wakati wa kumeza chakula likijulikana kama disfagia(dysphagia)


Viashiria


Viashiria hatari vinavyokufanya utafute tiba kutoka kwa daktari ni;


  • Maumivu ya koo au shingo

  • Kupoteza uzito

  • Tatizo kuanza ghafla

  • Maumivu, kupaliwa au kushindwa kumeza

  • Kucheua chakula au kutapika

  • Madhaifu ya misuli

  • Kuonekana kwa uvimbe

  • Dalili kuzidi kuwa mbaya zaidi jinsi siku zinavyokwenda


Onana na daktari wako haraka endapo uanapata viashiria vya hatari kwa uchunguzi zaidi.


Vipimo


Vipimo vitafanyika vikitegemea historia ya tatizo na dalili zilizoonekana, hata hivyo mara nyingi vipimo huwa havihitajiki lakini endapo vitahitajika ni kwa sababu tu ya kutofautisha tatizo hili na mengine ambayo yanaleta dalili kama hii.


Endapo una tatizo hili pia unaweza kupelekwa kwa mtaalamu wa kinywa pua na koo- ENT ili kufanyiwa uchunguzi zaidi na tiba.


Matibabu


Matibabu hutegemea kisababishi kilichofahamika, hata hivyo huhusisha;


  • Tiba ya mazoezi ya misuli ya kioo

  • Kutibu tatizo la ya kuchuruzika kwa majimaji nyuma ya koo kutoka puani

  • Tiba ya kucheua tindikali kwa dawa za kuzuia uzalishaji wa tindikali

  • Kuacha kuvuta sigara

  • Kutibu msongo wa mawazo kwa kutumia tiba ya kujitambua (soma zaidi kuhusu tiba hii katika ya ULY CLINIC

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 19:54:47

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Patient. Globus Sensation. https://patient.info/digestive-health/difficulty-swallowing-dysphagia/globus-sensation.Imechukuliwa 18.11.2020

2. MSD manual. Lump in Throat. Jonathan Gotfried , MD etal .www.msdmanuals.com/en-in/professional/gastrointestinal-disorders/symptoms-of-gastrointestinal-disorders/lump-in-throat#.Imechukuliwa 18.11.2020

3. Lump In Throat (Throat Fullness, Globus Syndrome, Globus Sensation, Globus Hystericus, Globus Pharyngeus). https://medicine.uiowa.edu/iowaprotocols/lump-throat-throat-fullness-globus-syndrome-globus-sensation-globus-hystericus-globus-pharyngeus. Imechukuliwa 18.11.2020

bottom of page