top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

8 Novemba 2021 08:01:05

Jipu
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Jipu

Jipu ni kijifuko kilichojazwa na usaha. Huweza kutokea sehemu yoyote ile ya mwili, mahali ambapo pamepata maambukizi ya , haswa chini ya ngozi ama kwenye misuli ya mwili. Ingawa jipu huweza tokea sehemu yoyote ile hata ndani ya tumbo.

Nini husababisha Jipu

Maambukizi haya yanaweza kusababishwa na bakteria, virusi, fangasi n.k lakini kwa asilimia kubwa huwa ni bakteria.

Namna gani jipu hutokea baada ya maambukizi ya vimelea?

Kwa kawaida maambukizi yanapotokea chini ya ngozi ama ndani ya misuli, chembe chembe nyeupe za damu zinazopambana na magonjwa huvamia maambukizi hayo ili kupambana nayo. Wakati wa mapambano hayo vimelea wa magonjwa hufa na na pia baadhi ya chembe zamwili hufa, majimaji pia husukanyika kutokana na michomo ya kwenye chembe chembe hai na hivo kutengeneza mkusanyiko wa majimaji na vimelea waliokufa, ambo huitwa jipu. Jipu hujitokeza kutokana na kuvimba kwenye sehemu husika lilipotokea na kwenye ngozi huwa rahisi kutambua kwa kuwa huonekana kwa nje.

Mara nyingi jipu huwa jekundu(kwa watu weupe), hunyanyuka juu ya usawa wa ngozi, na huuma. Jipu ndani ya mwili huwa halionekani na huzalisha dalili kutegemea lipo sehemu gani ya mwili. Mfano likiwa kichwani mtu anaweza kupata maumivu ya kichwa na anaweza pata kiharusi ama degedege, kukosa hisia sehemu Fulani ya mwili n.k

Matibabu


Matibabu ya jipu ni kutumbua na dawa zinazolenga kutibu kisababishi.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Novemba 2021 08:13:32

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. Wolters Kluwer Health/Lippincott Williams & Wilkins. p. 373.

2. Marx, John A. Marx (2014). "Skin and Soft Tissue Infections". Rosen's emergency medicine : concepts and clinical practice (8th ed.)

bottom of page