Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, MD
3 Desemba 2020 20:17:34
Kukauka kwa uke
Kukauka kwa uke(kuwa na uke mkavu) ni tatizo linalofahamika sana na linaloweza kuwapata wanawake katika umri wowote ule, hata hivyo hutokea sana kwa wanawake wenye umri mkubwa(miaka kati ya 50-60) haswa katika kipindi cha komahedhi.
Katika makala hii utajifunza kuhusu maana, dalili, visababishi na matibabu ya uke mkavu kwa ujumla na wakati wa ngono au kujamiana
Maji ya ya uke huzalishwa wapi?
Kwa kawaida wakati hufanyi ngono ute wa uke huzalishwa na tezi zilizo kwenye shingo ya kizazi, ute huu huwa na hali ya utindikali ili kuua vimelea vya maradhi vilivyo ukeni, ute hutoka kwenye eneo hili la shingo ya kizazi na kuonekana nje ya uke. Ute unaozalishwa huwa ni mweupe na huupa uke harufu ya kawaida tunayoifahamu.
Wakati wa shughuli za ngono au kujamiana pia, kuna tezi ambazo hufanya kazi ya kuzalisha ute ute mwingi kwenye uke ili kufanya tendo hilo liwe rahisi bila maumivu, tezi hizo ni tezi za batholin. Tezi za batholin huwa ni mbili kila upande wa katika mlango wa kuingia kwenye uke. Robo ya wanawake walio kwenye umri wa komahedhi hupata ukavu wa uke wakati wa tendon na wengine shida hii huambatana na maumivu
Kutokana na maelezo ya hapo juu, tatizo la uke kuwa mkavu limegawanyika katika sehemu mbili, uke mkavu kabla ya komahedhi na wakati wa komahedhi
Dalili
Dalili zinazoweza ambatana na uke mkavu ni;
Maumivu wakati wa ngono
Kusinyaa kwa kuta zauke
Kutokwa na damu wakati wa tendo
Kupoteza hamu ya tendo kutokana na maumivu
Maumivu ya uke wakati wa kufanya mazoezi kutembea, kukaa au kusimama
Kubadilika kwa mwonekano wa uke na mashavu ya uke
Kubadilika kwa tabia ya ute unaotoka ukeni
Kupata hisia za kuungua ukeni
Msongo wa mawazo na kuhisi mabadiliko makubwa mwilini mwako
Uke mkavu kabla ya komahedhi
Hutokea kwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 18- 50. Dalili ya uke mkavu hutokea wakati wa kujamiana na husababishwa na;
Kutosisimuliwa vya kutosha kabla ya ngono
Msongo wa mawazo
Kuwa kwenye mahusiano yasiyo na maelewano
Kufanyiwa ukatili wa kijinsia au kubakwa
Kutumia sabuni, dawa za kusafisha uke na kemikali zingine zinazoingia ukeni
Kuogelea kwenye maji
Kuoga kwenye sinki la maji moto
Matumizi ya dawa za kuzuia aleji na kutibu homa ya baridi
Matumizi ya dawa za kuzuia msongo wa mawazo
Uke mkavu wakati wa komahedhi
Wanawake wanaofika katika kipindi cha miaka 50 na kuendelea huingia katika kipindi cha hedhi kukoma kuonekana, kipinid hiki huitwa kipindi cha komahedhi. Katika kipinid hiki wanawake hupata uke mkavu kwa sababu ya kushuka endelevu kwa kiwango cha homoni estrogen kwenye damu ambayo huzalishwa na kiwanda cha mayai yaani ovary.
Sababu zingine za uke kuwa mkavu
Visababishi
Vipo visababishi mbalimbali vinavyoweza kupelekea uke kuwa mkavu ambavyo vinafahamika ambavyo ni;
Kupungua kwa kiwango cha homoni estrogen kwenye damu
Hali na mambo yanayoweza kupelekekea kushuka kwa homoni hii ni;
Kunyonyesha kwa wakati huu
Kutoka kujifungua
Kuvuta sigara
Kutibiwa kwa dawa za saratani kwenye ovary
Madhaifu ya kinga z amwili
Komahedhi
Kukaribia kipinid cha koma hedhi
Kufanyiwa upasuaji wa kutolewa ovary
Kutumia dawa za kuzuia uzalishaji wa estrogen
Kusafisha ndani ya uke kwa maji na sabuni zenye kemikali
Sindrome ya sjogren’s
Matumizi za kuzuia aleji na homa baridi
Matibabu
Kabla ya kufanyiwa matibabu daktari wako atakuuliza maswali mbalimbali yanayohusiana na visabaishi na kukufanyia vipimo ili kufahamu ni nini kisababishi kwako. Mpe ushirikiano daktari wako ili ajue tatizo lako. Mtibabu hulenga kutibu kisababishi kilichofahamika, inaweza kuwa matibabu dawa au tiba ya saikolojia.
Matibabu ya nyumbani
Fanya mambo yafuatayo ili kujitibu nyumbani dhidi ya uke mkavu
Tumia vilainisha uke ambavyo vinapatikana kwenye maduka ya dawa, paka vilainishi hivi kwenye mashavu ya uke na ndani ya uke kabla ya kujamiana
Tumia vitia unyevu ukeni ambavyo utaandikiwa na daktari wako, tumia mara tatu kwa wiki
Kwa wanawake walio kwenye komahedhi na wale wenye homoni ya chini ya estrogen, matumizi ya vidonge vya estrogen vinavyowekwa ukeni husaidia kuondoa tatizo hilo
Matumizi ya dawa zenye homoni ya dehydroepiandrosterone mara moja kwa siku
Kujikinga kutumia pafyumu za kuweka ukeni
Usiumie krimu zinazochokoza uke wako
Tumia muda mrefu zaidi kwenye maandalizi kabla ya kufanya tendo ili kuzipa muda tezi batholin kuzalisha ute wa kutosha
Wakati gani wa kumwona daktari wa matibabu?
Endapo unapata tatizo hili na licha ya kufanya juhudi zozote, hakikisha unaonana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba.
Wanawake wengi huwa wanakaa kimya na tatizo hili bila kumshirikisha mtu yeyote na kutafuta matibabu, kwa baadhi ya nyakati ni kwa sababu ya kuona aibu kuongea kuhusu tatizo hili. Unapopatwa na tatizo hili fahamu kuwa haupo peke yako, wapo watu wanaopata tatizo hili na matibabu yapo. Hakikisha unawasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi na matibabu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako wakati wote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:47
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Bachmann G, et al. Clinical manifestations and diagnosis of genitourinary syndrome of menopause (vulvovaginal atrophy). https://www.uptodate.com/contents/search . Imechukuliwa 2.12.2020
2. Casper RF. Clinical manifestations and diagnosis of menopause. https://www.uptodate.com/contents/search . Imechukuliwa 2.12.2020
3. Baer AN. Treatment of dry mouth and other non-ocular sicca symptoms in Sjogren's syndrome. https://www.uptodate.com/contents/search . Imechukuliwa 2.12.2020
4. Frequently asked questions. Women's health FAQ072. Your sexual health . American College of Obstetricians and Gynecologists. https://www.acog.org/Patients/FAQs/Your-Sexual-Health. Imechukuliwa 2.12.2020
5. Frequently asked questions. Gynecologic problems FAQ028. Vaginitis. American College of Obstetricians and Gynecologists. https://www.acog.org/Patients/FAQs/Vaginitis. Imechukuliwa 2.12.2020
6. Vaginal dryness. https://www.womens-health-concern.org/help-and-advice/factsheets/vaginal-dryness/#. Imechukuliwa 2.12.2020
7. Vaginal dryness. https://www.healthdirect.gov.au/vaginal-dryness. Imechukuliwa 2.12.2020
8. 5 Reasons Your Vagina Is Going Dry. https://www.womenshealthmag.com/health/a19890829/vaginal-dryness/. Imechukuliwa 2.12.2020