Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Adolf S, M.D
31 Machi 2020 18:39:21
Kuoza meno
Ni matatizo yanayojumuisha inflamesheni za tishu zinazozunguka jino, kupoteza jino na maambukizi ya jini.
Pia ni kuharibika kwa meno kutokana na shughuli za bakteria ambao hushambulia mabaki ya sukari kwenye jino na kuzalisha asidi ambayo huharibu madini ya jino.
Bakteria huharibu tishu ngumu ya meno (za enemali, dentini na simentamu) kwa kutengeneza asidi kutoka kwenye mabaki ya chakula yaliyo kwenye sehemu ya jino.
Ikiwa uharibifu wa madini ya jino ni mkubwa kuliko ujenzi kutoka kwa vyanzo kama vile mate, matokeo ni kuoza kwa meno.
Tatizo hili hutokea kwa watu wa lika zote (watoto, vijana na wazee).
Kuoza meno limekua ni tatizo kubwa duniani kwa asilimia 36 ya idadi ya watu. Pia huhusishwa na umaskini, usafishaji wa kinywa na vyakula.
Bakteria wanaosababisha meno kuoza
Streptococcus mutans
Lactobacillus
Actinomyces
Visababishi
Vijidudu kwenye meno mfani;bakteria
Uchafu kwenye meno
Kuzalishwa kwa mate kidogo mdomoni
Kula sana vyakula vyenye wanga na sukari
Umbile baya la jino
Kuwa na mapengo kati ya jino na jino
Dalili
Zifuatazo ni dalili za meno kuoza
Jino kubadilika rangi
Kutokwa kwa vishimo kwenye jino
Maumivu wakati wa kula chakula au kunywa maji baridi au moto.
Jino kupata ganzi
Fizi kuvimba
Kupata homa
Matatizo yatokanayo na meno kuoza
Infenksheni ya fofota
Fofota/kufa
Majipu kwenye tishu
Kupata jipu kwenye mapafu
Infenksheni ya mifupa ya taya
Matibabu
Matibabu yanaweza kuhusisha
Kutumia dawa ya kupunguza maumivu mfano; NSAIDs
Kuziba jino. Hii hufanyika kwa jino lililotoboka/ lenye shimo
Kung'oa jino
Kutumia antibayotiki. Hii husaidia kupunguza kuenea kwa wadudu kwenye meno ya pembeni mfano; Amoxylline
Knga
Kupunguza matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi
Kusafisha meno (kupiga mswaki kwa kutumia dawa ya meno angalau mara 3 kwa siku) mara kwa mara.
Kupunguza matumizi ya floraidi. Hii hupatikana kwenye maji, chumvi, au dawa ya meno.
Kufanya uchunguzi wa kinywa (kumwona daktari wa meno) mara kwa mara ili kupata ushauri.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:03:53
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1.MOHSW.(2005).Oral surgery and pathology.A Manual for Dental Therapist.DRAFT. Dar es salaam,Tanzania: ministry of health and social welfare
2.Laudenbanch, JM; Simon,Z(November 2014) Common Dental and Periodontal Disease: Evaluation and Management. The medical clinic of North America.