Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Charles W, MD
Dkt. Benjamin L, MD
21 Novemba 2021 07:05:22
Kupiga miayo mingi
Kupiga mwayo ni kitendo kisicho cha hiari cha kufungua kinywa na kuvuta pumzi kwa kina ili kujaza hewa safi kwenye mapafu. Hutokea kama jambo la asili kwa binadamu na huamshwa mara nyingi na uchovu wa mwili au kukosa usingizi.
Baadhi ya miayo hudumu kwa sekunde chache kabla ya kufungua mdomo na kutoa hewa iliyovutwa wakati wa mwayo
Dalili
Dalili mbalimbali zinaweza kuambatana na miayo ambazo ni;
Kujinyoosha mwili
Macho kutoa machozi
n.k
Hata hivyo tafiti mbalimbali hazijapata uhakika kwanini watu wanapiga miayo, lakini viamsha miayo vinafahamika kama vile uchovu wa mwili na kuboreka. Unaweza pia kupiga mwayo endapo ukiongeleakuhusu mwayo au kuona mtu anaiga mwayo.
Ni nini faida za kupiga miayo?
Tafiti zinaonyesha kupima miayo husaidia,
​
Kupooza ubongo
Kupunguza shinikizo la hewa ndnai ya sikio
Kudumisha mawasiliano asilia kwenye jamii
Kupiga miayo mara nyingi kuliko kawaida hutokea pale endapo unapiga miayo zaidi ya mmoja kwa dakika, hali hii inaweza kusababishwa na magonjwa au uchovu na kukosa usingizi.
Kuna baadhi ya hali na magonjwa huweza kuamsha rifleksi za mshipa wa vagasi na kupelekea mtu kupiga miayo inayoambatana na kushuka kwa mapigo ya moyo na shinikizo la damu.
Visababishi ni nini?
​
Visababishi halisi vya kupiga miayo mara kwa mara huwa havijulikani, hata hivyo huweza kuchangiwa na;
Kusinzia, kuchoka au uchovu mkali wa mwili
Madhaifu ya kulala kama vile apnia na nakolepsi, angzayati
Maudhi ya dawa aina Fulani yanayotumika kutibu sononeko, ang’zayati
Kuvilia damu maeneo ya kuzunguka moyo ambayo huweza kuambatana na dalili za kuishiwa pumzi, kifua kuwa kizito,maumivu sehemu ya juu ya mwili, kichefuchefu, kuhisi kichwa chepesi.
Matumizi ya dawa kama za SSRI, baadhi ya dawa za maumivu, dawaza antihistamine n.k
Visababishi vingine
Kwa mara chache sana sababu zingine zinaweza kuwa;
Saratani ndani ya ubongo huambatana na dalili za maumivu ya kichwa, kupoteza kumbukumbu, kuhisi ganzi, mwili kuchomachoma, kutoona vema, kupooza mwili
Mshituko wa moyo
Kiharusi- huambatana na kupooza kwa mwili maeneo ya uso au upande mmoja wa mwili
Kifafa
Sclerosisi ya kusambaa
Upungufu wa vichocheo vya tezi thyroid
Mwili kushindwa dhibiti joto lake
Kupotea kwa uwiano wa madini mwilini
Kufeli kwa ini- huweza kuambatana na kukosa hamu ya kula, kichefuchefu, kuharisha,kuchanganyikiwa, kuchoka sana wakati wa mchana, kuvimba tumbo
Ongea na daktari wako ili kujua kisababishi cha kupiga kwako miayo, daktari wako tu anaweza kutambua kisababishi
Vipimo
Utaulizwa maswali mbalimbali kabla ya kufanyiwa vipimo, haswa maswali kuhusu tabia yako ya kulala ili kutambua kama unapata usingizi wa kutosha na endapo tatizo lako linahusiana na kukosa usingizi. Vipimo unavyoweza kufanyiwa ni;
Kipmo cha kuangalia tabia ya umeme wa ubongo- ECG. Kipimo hiki huweza kutambua matatizo ya degedege
Kipimo cha MRI- huweza kutambua uvimbe kwenye ubongo na matipo slerosisi, pia huweza kuangalia utendaji kazi wa moyo na kutambua matatio ya moyo.
Matibabu
Matibabu ya kupiga miayo mara kwa mara
Matibabu yatategemea kisababishi, kama kitakuwa dawa unazotumia, daktari atakushauri uache kutumia dawa na kukupa mbadala. Inategemewa utakapoacha dawa hizo miayo itaisha ndani ya siku chache.
Kama kisababishi ni kukosa usingizi au madhaifu ya usingizi, daktari atakupa dawa au mbinu za namna ya kupata usingizi na kupumzisha mwili wako zinazohusisha;
Kutumia vifaa vya kupumulia kama unakosa hewa wakati wa kulala
Kufanya mazoezi ya mwili ili kupunguza msongo mwilini
Kuzingatia tabia ya kulala enye mpangilio
Kama kisababishi cha kupiga miayo ni kwa sababu ya ugonjwa mwilini, kisababishi hicho kinatakiw akutibiwa haraka iwezekanavyo.
​
Namna ya kuacha kupiga miayo mingi
Njia zifuatazo zinaweza kukusaidia kuacha kupiga miayo mingi
Vuta hewa kwa kina
Kama unahisi unapiga miayo mingi, jaribu kufanyazoezi la kuvuta hewa kwa kina kupitia pua. Hii ni kwa sababu unapopiga miayo mingi maanake mwili wako unahitaji hewa safi kwa wingi. Tafiti pia zimeonyesha kufanya hivi hupunguza kupiga miayo ya kuambukizwa.
Pumzika
Kama una majukumu mengi yanayokuletea uchovu, kuboreka na msongo mwilini unahatari ya kupata miayo mingi zaidi. Matumizi ya kahawa au kuongea sana pia husababisha kupiga miayo. Unapaswa kupata muda wa kupumzika, jipange na majukumu nayo ili kupata muda wa kupumzika
Pooza mwili wako
Unaweza kupooza mwili kwa kutembea maeneo yenye upepo mfano kwenye ufukwe wa bahari, mlimani au barabara yenye upepo mwingi. Kunywa kinywaji cha chenye ubaridi pia ( maji au juisi asili) ni njia mojawapo ya kupooza mwili. Kufanya hivi hupunguza joto mwilini na kitendo cha kupiga miayo mingi.​
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
21 Novemba 2021 07:41:13
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Why do you yawn when you’re not sleepy?. psychologytoday.com/blog/brain-sense/201111/why-do-you-yawn-when-youre-not-sleepy. Imechukuliwa 07.07.2020
2. A case of excessive yawning with citalopram. ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2708013/. Imechukuliwa 07.07.2020
3. Yawning. https://www.medicalnewstoday.com/articles/324401#treatment. Imechukuliwa 07.07.2020
4. Yawning. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3678674/. Imechukuliwa 07.07.2020
5. health grades. yawning excessively. https://www.healthgrades.com/right-care/symptoms-and-conditions/yawning-excessively. Imechukuliwa 07.07.2020