top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Dkt. Helen L, MD

11 Juni 2023 09:23:52

Maumivu ya Mkono
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Maumivu ya Mkono

Utangulizi


Maumivu ya mkono ni maumivu yanayotokea kwenye eneo kati ya maungio ya kiganja cha mkono na bega ambayo huweza kutokea kama maumivu au uchungu, kuchoma au kutoboa yanayopelekea kuathiri utendaji kazi.


Dalili zingine zinaweza kuambatana na maumivu ya mkono ni kama vile maumivu, kukakamaa, uvimbe, na kutoweza kujongea bila kusababisha maumivu. Maumivu ya mkono yanaweza kuwa ya kudumu kwa muda mfupi au mrefu na yanaweza kuathiri mkono mzima au eneo fulani tu.


Visababishi vya maumivu ya mkono

Maumivu ya mkono mara nyingi husabaishwa na kuumia au kuanguka, hata hivyo visababishi pia vinaweza kutokea kwenye mkono au sehemu nyingine ya mwili.


Ikiwa maumivu yanatokana na sababu katika mkono huweza kutokana na uchovu wa misuli au tendoni kutokana na kufanya kazi kupita kiasi. Yanaweza pia kusababishwa na maumivu ya tendoni, kuvia kwa damu kutokana na kugonjwa, kuchanika kwa viungo vya maungio ya mkono na kuvunjika mfupa.


Mgandamizo kwenye mshipa wa fahamu

Mgandamizo kwenye mshia wa fahamu unaweza kusababisha mshipa huo usifanye kazi vema ya kusafirisha taarifa katika mfumo wa umeme na hivyo kupelekea maumivu makali, ganzi, kuchomachoma, au misuli kuwa dhaifu.

Mgandamizo unawez akusabaishwa na:

  • Mifupa

  • Misuli

  • Tendoni

  • Uvimbe


Kuchanika kwa tishu unganishi katika maungio ya mkono

Tishu unganishi hujumuisha ligamenti na tendoni ambazo zikichanika au kunyumbulika hupelekea kusabaisha maumivu katika maungio. Kuchanika ama kunyumbulika kwa tishu unganishi kunaweza kutokana jeraha kwenye maungio ya mkono na matibabu yake yanaweza kufanyika nyumbani au kuhitaji upasuaji kutegemea na ukubwa wa uharibifu wa tishu unganishi.


Dalili zake huwa pamoja na:

  • Kuvimba

  • Kuvia kwa damu

  • Kiungo kushindwa jongea kwenye baadhi ya uelekeo

  • Ungio kutokuwa imara


Kuvunjika kwa mifupa

Kuvunjika mfupa husababisha maumivu makali, ya kuchoma kama mshale katika mkono. Ukiwa umevunjika mkono utasikia sauti ya mifupa kusagana endapo utajongesha kiungo hiko. Dalili zingine zinajumuisha

  • Kuvimba kwa mkono

  • Kuvia kwa damu

  • Mauivu makali

  • Kubadilika kwa umbile la mkono

  • Kushindwa kujongesha mkono uelekeo wa kwenda mbele na nyuma


Visabaishi vingine

Visababishi vingine vinajumuisha:

  • Anjaina

  • Mshituko wa moyo

  • Baridi yabisi


Utambuzi

Visababishi vya maumivu ya mkono vinaweza kutambuliwa kwa kufanya uchunguzi wa mwili na vipimo, Baadhi ya vipimo ni pamoja na:

  • MRI

  • EMG

  • Utrasound

  • Vipimo vya damu


Matibabu ya maumivu ya mkono

Matibabu ya maumivu ya mkono hutegemea kisababishi na ukubwa wa tatizo. Yanaweza kuwa ya nyumbani au hospitali.


Matibabu yanaweza kuhusisha

  • Dawa za maumivu

  • Dawa za ganzi

  • Tiba mazoezi

  • Upasuaji


Matibabu ya nyumbani ya maumivu ya mkono

  • Pata mapumziko kiasi nyumbani

  • Kanda kwa kutumia mfuko wa barafu iliyoganda kwenye eneo linaloouma kwa dakika 15 hadi 20 mara tatu kwa siku

  • Funga mkanda wa mgandamizo kupunguza uvimbe

  • Weka mkono wako usawa wa juu ya mwili kupunguza maumivu. Unaweza kutumia mto au kitu chochote.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

11 Juni 2023 09:23:52

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

​

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. https://journals.lww.com/spinejournal/Abstract/2003/09010/Impact_of_Neck_and_Arm_Pain_on_Overall_Health.23.aspx. Imechukuliwa 10.06.2023

2. https://pediatrics.aappublications.org/content/117/2/412.short. Imechukuliwa 10.06.2023

3. https://onlinelibrary.wiley.com/doi/full/10.1002/art.23580. Imechukuliwa 10.06.2023

4. Seller RH, et al. Pain in the upper extremity. In: Differential Diagnosis of Common Complaints. 7th ed. Elsevier; 2018. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 10.06.2023

5.Ferri FF. N — Differential diagnosis. In: Ferri's Clinical Advisor 2023. Elsevier; 2023. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 10.06.2023
Imechukuliwa 10.06.2023

6. Goldman L, et al., eds. Bursitis, tendinitis, and other periarticular disorders and sports medicine. In: Goldman-Cecil Medicine. 26th ed. Elsevier; 2020. https://www.clinicalkey.com. Accessed Jan. 26, 2023.

7. Heart attack symptoms, risk, and recovery. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/heartdisease/heart_attack.htm. Imechukuliwa 10.06.2023

8. LaDou J, et al., eds. Shoulder, elbow, & hand injuries. In: Current Diagnosis & Treatment: Occupational & Environmental Medicine. 6th ed. McGraw Hill; 2021. https://www.clinicalkey.com. Accessed Jan. 26, 2023.

9. Stelter J, et al. The emergent evaluation and treatment of shoulder, clavicle and humerus injuries. Emergency Medicine Clinics of North America. 2020; doi:10.1016/j.emc.2019.09.006.

bottom of page