Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
7 Machi 2021 14:22:49
Michirizi ya kuvimba mishipa ya damu chini ya ngozi
Telangiectasia ni nini?
Telangiectasia ni dalili ya mwonekano wa mistari yenye rangi ya pinki au nyekundu inayopotea kwa muda mfupi endapo itagandamizwa.
Telangiectasia huwa ni ishara ya kuvimba au kupasuka kwa mishipa ya damu chini kidogo na karibu na sura ya ngozi, hali hii inaweza kutokea kwenye ngozi ya nje au ngozi laini katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwa pamoja na macho, kiwiliwili, pua, ubongo au ndani ya kuta za mfumo wa chakula n.k.
Mishipa mingi ya damu iliyovimba inaweza kutukana na kufanya eneo lililoathiriwa kuwa na baka lenye rangi ya pinki au nyekundu. Hali hii huweza kumwathiri mtu wa umri wowote ule na wakati mwingine huhusiana sana na tatizo la ‘varicose vein’ linalotokana na kuongezeka kwa shinikizo la damu kwenye moyo au kuziba kwa mishipa ya damu inayorejesha damu kwenye moyo
Je tatizo la telangiectasia ni hatari?
Mara nyingi visababishi vya tatizo hili huwa ni vya kawaida na visivyoleta madhara yoyote au kuhitaji matibabu. Madhara kwa watu wengi huwa ni yale ya kimwonekano tu, yaani watu wenye tatizo hili hujiona na mwonekano w akutofauti wakijifananisha na wenzao. Licha ya kuwa telangiectasia husababiswha na hali zisizo za hatari, kuna baadhi ya visababishi vinaweza kuwa vya hatari zaidi na hivyo mtu atahitaji uchunguzi ili kufahamu shida yake ni nini kabla ya kusema tatizo lakeni la kawaida au la.
Hali na magonjwa gani yanayosababisha tatizo la telangiectasia?
Mtu mwenye Telangiectases anapaswa kufanyiwa uchunguzi ili kutofautisha hali ya kawaida au magonjwa mengine ambayo yanaweza kuonekana na ishara hii ya telangiectasia. Baadhi ya magonjwa yanayoonekana na ishara ya telangiectasia ni;
Saratani ya mishipa ya damu
Infantile Hemangioma
Madhaifu ya uumbaji wa mishipa ya capillary au vein
Varicose vein
Aneurism
Aina
Kuna makundi mawili ya telangiectasia, kundi la telangiectasia ya kurithi na telangiectasia ya kupata ukubwani.
Visababishi
Hakuna kisababishi cha kueleweka kinachofahamika kusababisha telangiectasia, hata hivyo baadhi ya visababishi vinavyofahamika katika makundi mbalimbali ambayo ni ;
Telangiectasia ya kurithi
Telangiectasia ya ukubwani
Telangiectasia kutokana na majeraha kwenye ngozi
Telangiectasia kutokana na saratani
Telangiectasia kutokana dawa
Telangiectasia ya kurithi
Visababishi mbalimbali vya telangiectasia ya kurithi ni pamoja na;
Telangiectasia ya kuvuja damu ya kurithi
Telangiectasia ya kurithi isiyo na madhara
Telangiectasia ya mwili mzima isiyo na madhara
Telangiectasia ya upande mmoja aina ya naevoid
Angioma serpiginosum
Syndrome ya Rothmund Thompson
Ataxia-telangiectasia
Syndrome ya Bloom
Syndrome ya Cockayne
Cutis marmorata telangiectatica congenita
Syndrome ya Goltz
Syndrome ya Kindler
Telangiectasia ya ukubwani
Visababishi vya telangiectasia ya ukubwani ni pamoja na;
Uogonjwa wa Rosacea
Telangiectasia ya kuchomwa na mwanga wa jua
Telangiectasia ya kuzeeka kwa ngozi haswa kwa watu wanaovuta sigara
Spider telangiectasis
Poikiloderma ya Civatte kutokana na kuchomwa na mwanga wa jua shingoni
Telangiectasia ya ujauzito
Telangiectasia kutokana na magonjwa ya ini yanayohusiana na unywaji pombe oamoja na maambukizi ya virusi
Syndrome ya Cushing
Sclerosis ya kudhuru viungo vya mwili
Cutaneous lupus erythematosus
Magonjwa ya tishu zinazounga tishu na tishu
Ugonjwa wa Dermatomyositis
Ugonjwa wa Mastocytosis
Syndrome ya Carcinoid
Necrobiosis lipoidica
Telangiectasia kutokana na majeraha kwenye ngozi
Telangiectasia kutokana na majeraha kwenye ngozi kama vile;
Makovu ya keloid au yasiyo ya keloid
Kupigwa na muonzi ya jua au miongiz aina nyingine
Telangiectasia kutokana na saratani
Telangiectasia kutokana na saratani inaweza kusababishwa na saratani kama;
Sebaceous hyperplasia
Saratani ya basal cell
Saratani ya cel za Merkel
Saratani ya Kaposi
Lymphoma ya T-seli kwenye za ngozi
Lymphoma B-seli za Intravascular
Telangiectasia in skin tumours
Telangiectasia kutokana dawa
Baadhi ya dawa zinazoweza kupelekea tatizo la telangiectasia ni;
Matumizi ya muda mrefu ya dawa jamii ya corticosterois kwa njia ya kunywa au kuchoma kwenye mishipa
Matumizi ya dawa za kutanua mishioa na jamii ya calcium channel bloka
Kuchoma sindano ya triamcinolone
Certain medications may give rise to telangiectasia.
Dalili
Dalili za telengiestasia hutegemea kisababishi
Dalili kwa ujumla huwa ni
Maumivu endapo kutakuwana mgandamizo kwenye mishipa inayoonekana
Muasho
Mwonekano wa alama kama michirizi ya mishipa ya damu chini kidogo ya ngozi yenye rangi nyekundu au pinki
Dalili za telangiectasia ya kurithi inayoambatana na kuvuja damu huwa pamoja na;
Kutokwa damu puani mara kwa mara
Kutokwa na haja kubwa nyeusi au nyekundu
Kuishiwa pumzi
Degedege
Kupata kiharusi
Kuzaliwa na alama za kuzaliwa kama mabaka ya port-wine
Vihatarishi
Vihatarishi vinavyoweza kupelekea kupata telangiectasia ni
Kuwa na ndugu wa damu moja mwenye tatizo hili(baba, mama au mtoto)
Kuwa mjamzito
Kupigwa jua au na upepo
Kutumia dawa zinazotanuamishipa ya damu
Kunywa pombe kupita kiasi
Kupata majeraha kwenye ngozi
Kufanyiwa upasuaji
Chunusi
Matumizi ya muda mrefu ya dawa jamii ya corticosteroid kwa kupata au kunywa
Wakati gani wa kumwona daktari?
Mara nyingi watu huwa hawahitaji kuonana na daktari endapo wana tatizo hili, lakini endapo una tatizo hili la telangiactisia pamoja na dalili zifuatazo unapaswa kuonana na daktari wako kwa uchunguzi na tiba;
Maumivukwenye mishipa ya damu iliyovimba
Muasho mkali
Kutokwa damu puani mara kwa mara
Kutokwa na haja kubwa nyeusi au nyekundu
Kuishiwa pumzi
Degedege
Kupata kiharusi
Kuzaliwa na alama za kuzaliwa kama mabaka ya port-wine
Vipimo
Tatizo la telangiectasia hutambuliwa kwa mwonekano wake na kutoka kwenye historia ambayo atakuuliza daktari wako. Mbali na hivyo daktari anaweza kukuandikia vipimo ili kuthibitisha alichodhani kuwa ni kisababishi kwako. Daktari wako anaweza kukuandikia kipimo kati ya hivi hapa chini;
Kipimo cha damu kama FBP
Kipimo cha Liver function test
Kipimo cha mionzi kama CT scan na Xray
Kipimo cha MRI
Matibabu
Mara nyingi, telangiectasia huwa haina madhara yoyote. Matibabu yanaweza kufikiriwa kufanyika endapo mtu anatokwa damu au kutopenda mwonekano wa mishipa ya damu. Mara baada ya kufanyiwa vipimo, daktari atatibu kisababushi kilichosababisha kuonekana kwa tatizo lako.
Licha ya kuwepo kwa matibabu ya kuondoa dalili ya mwonekano wa mishipa iliyovimba, hakuna tiba ya moja kwa moja kuondoa tatizo hili.
Matibabu mbalimbali yapo ambayo yanahusisha;
Tiba ya upasuaji wa kisu cha umeme kuondoa ishipa ya damu iliyovimba
Tiba dawa kutibu kisababishi, mfano endapo sababu ni maambukizi utapewa dawa kuondoa maambukizi hayo.
Tiba ya mwanga wa laser kuziba mishipa ya damu iliypasuka
Tiba ya sclerotherapy kwa mishipa ya damu iliyokuwa mikubwa zaidi
Matibabu ya nyumbani
Jikande na maji ya baridi au barafu kwenye eneo la mishipa iliyovimba baada ya kupigwa na mwanga wa jua au baada ya kutoka juani. Usitumie maji ya moto kuepuka kujeruhi mishipa ya damu.
Paka mafuta ya arnica au ya mmea witch hazel au vinegar ya tufaa kwa kutumia pamba kila siku au mara mbili kwa siku. Hii itafanya ngozi ishikamane vema na kuzuia mwonekano wa mishioa ya damu iliyovimba
Tumia mafuta au majimaji ya alovera kila siku kwenye eneo lenye shida ya mwonekano wa mishipa ya damu iliyovimba. Tafiti zinaonyesha mafuta au majimaji haya hufanya ngozi ishikamane vema hivyo huweza saidia kupunguza wekundu kwenye ngozi
Tumia vitamin C endapo utashauriwa na daktari wako. Vitamin C hufanya kazi ya kutibu majeraha na mishipa ya damu iliyo na shida pamoja na kuifanya iwe na afya njema. Matumizi ya vitamin C yatafanya wekundu na mishipa ya damu iliyovimba kupotea. Tumia endapo utashauriwa na daktari wako.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 19:54:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. Telangiectasia. https://dermnetnz.org/topics/telangiectasia/. Imechukuliwa 7.03.2021
2. Giulietta Maria Riboldi et al. Ataxia Telangiectasia. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK519542/. Imechukuliwa 7.03.2021
3. Cynthia Rothblum-Oviatt, et al. Ataxia telangiectasia: a review. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5123280/. Imechukuliwa 7.03.2021
4. Hereditary Hemorrhagic Telangiectasia (Osler-Weber-Rendu Syndrome).https://www.merckmanuals.com/professional/hematology-and-oncology/bleeding-due-to-abnormal-blood-vessels/hereditary-hemorrhagic-telangiectasia. Imechukuliwa 7.03.2021
5. Hereditary hemorrhagic telangiectasia. https://medlineplus.gov/genetics/condition/hereditary-hemorrhagic-telangiectasia/.Imechukuliwa 7.03.2021
6. Bloom syndrome. https://medlineplus.gov/genetics/condition/bloom-syndrome/. Imechukuliwa
7.03.20217. Rachel Farley-Loftus, et al. Poikilodermatous mycosis fungoides. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/21163159/. Imechukuliwa 7.03.2021