top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

25 Machi 2021 17:30:03

Msinyao wa urethra
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Msinyao wa urethra

Msinyao wa urethra kitiba ikifahamika kama ‘urethral stricture’ ni ugonjwa unaosababishwa na makovu au uvimbe katika kuta za mrija wa mkojo wenye jina la urethra. Kusinyaa huko husababisha mrija kuwa mwembamba hivyo kuleta dalili mbalimbali kama vile mkojo kushindwa kutoka, kutumia nguvu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, hisia za kutokojo mkojo wote na dalili zingine.



Tatizo hili hutokea sana kwa wanaume zaidi ya wanawake duniani na humpata mtu yeyote katika umri wowote ule


Dalili


Dalili kuu za msinyao wa urethra ni pamoja na;


  • Kupungua kwa mkondo wa mkojo

  • Hisia za mkojo kubaki kwenye kibofu muda mfupi baada ya kukojoa

  • Mkojo kutoka mithiri ya maji ya bomba la mvua

  • Kushindwa kutoa mkojo kirahisi

  • Kukenya wakati wa kukojoa ili kusukuma mkojo utoke

  • Maumivu wakati wa kukojoa

  • Kukojoa mara kwa mara

  • Maambukizi ya UTI / na UTI ya kujirudia rudia haswa inayosababishwa na bakteria Escherichia coli, maambukizi ya kichocho, TB, haya husababisha michomo kwenye mrija wamkojo

  • Ugonjwa wa michomo kama vile Lichen sclerosis (LS)


Visababishi


Visababishi vya ugonjwa huu vimegawanyika katika makundi makuu manne ambayo ni,


  • Sababu zisizofahamika

  • Majeraha njia ya mkojo

  • Michomo njia ya mkojo

  • Madhara ya kitiba


Maelezo yanayofuata yanazungumzia visababishi mbalimbali ambavyo vipo kwenye makundi yaliyotajwa hapo juu


Visababishi


  • Kuingiziwa kifaa chochote kupitia njia ya mkojo wakati wa matibabu kama vile kamera kuchunguza ndani ya kibofu cha mkojo au wakati wa upasuaji wa tezi dume

  • Matumizi ya catheter kwenye njia ya mkojo kwa muda mfupi au muda mrefu

  • Majeraha kwenye mrija wa mkojo au via vilivyomo ndani ya nyonga

  • Kukua kwa tezi dume

  • Upasuaji wa kupunguza au kuondoa tezi dume

  • Saratani ya mrija wa urethra

  • Maambukizi ya magonjwa ya zinaa

  • Madhara ya tiba mionzi


Namna gani tatizo hili hutambuliwa hospitali?


Tatizo hili hutambuliwa kwa kutumia historia ya tatizo, dalili pamoja na vipimo mbalimbali.

Baadhi ya vipimo vinalenga kutambua kisababishi na vingine vinalenga kufahamu shida ni nini.


Vipimo


  • Kipimo cha kuingiza kamera kwenye mrija ili kuona sehemu iliyoziba kinachoitwa Urethroscopy

  • Kipimo cha Cystourethrogram. Hiki hufanyika kwa kuwekewa kemikali maalumu kwenye kibofu kisha kupigwa picha ya Xray ili kuangalia ni sehemu gani ya njia ya mkojo imeziba. Kipimo hiki huchukua muda mrefu na ni muhimu sana kufanyika


Matibabu


Matibabu yanayofanyika hutegemea na hatua au ukubwa wa kovu. Matibabu hayo huhusisha


  • Upasuaji wa kovu dogo

  • Upasuaji kovu Kubwa


Matibabu ya kovu dogo

Kovu dogo hutibiwa kwa kuingiziwa kitu ili kutanua njia ya mkojo, baada ya kutanua kuna hatari ya kujirudia kwa kovu hivyo utapewa dawa za kuzuia makovu na pia kukaa na mrija wa mkojo kwa miezi michache kabla ya kutolewa na kuwa huru.


Matibabu ya kovu kubwa

Makovu haya huhitaji matibabu ya upasuaji wa hatua, utafanyiwa upasuaji wa kufungua njia ya mkojo kutoa kovu kisha kuunga miiishio ya kuta za mrija, kitiba upasuaji huu hufahamika kama urethroplasty.


Endapo upasuaji huu si sahihi kwako haswa kwa kovu kubwa, utafanyiwa upasuaji wa hatua ili kutoa kovu, na kutengeneza mrija mpya wa urethral eneo lililotolewa kovu. Kuta za mrija mpya utavunwa kwenye ngozi ndani ya mashavu yako au ngozi ya pumbu.


Baada ya kufanyiwa upasuaji, daktari atashauri ukae na mpira wa mkojo (catheter) kabla ya kupona.


Ufanisi wa matibabu ya msinyao wa urethra

Mara nyingi matibabu hufanikiwa na wagonjwa hurejea kwenye maisha ya kawaida kama zamani. Hata hivyo tatizo hili linaweza kujirudia, hivyo endapo umeandikiwa kuonwa na daktari baada ya upasuaji, unatakiwa usikose kwenda kliniki yako kwa ajili ya kufuatiliwa maendeleo mpaka pale daktari atakajiridhisha hakuna uhaja wa kuhudhuria.


Kinga


Ni kweli huwezi kukinga magonjwa yote lakini unaweza kujikinga na vihatarishi vya makovu kwenye mrija wako wa mkojo kwa


  • Kupata matibabu ya magonjwa ya njia ya mkojo kwa wakati

  • Kuepuka vihatarishi vinavyoweza kuleta majeraha kwenye via ndani ya nyonga au njia ya mkojo

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021 04:53:26

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1. UPTODATE. Peterson A. Urethral strictures in men. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 25.03.2021

2. AUA guideline. American Urological Association Male urethral stricture:. https://www.auanet.org/guidelines/male-urethral-stricture-(2016). Imechukuliwa 25.03.2021

3. Tritschler S, et al. Urethral stricture: Etiology, investigation and treatments. Deutsches Ärzteblatt International. 2013;110:220.

4. Luman N, Oosterlimck W, Hoebeke P. Urethral reconstruction using buccal mucosa or penile skin grafts: systematic review and meta-analysis. Urol Int 2012;89:387-394. Imechukuliwa 25.03.2021

5. Bashar M. Abdeen, et al .Urethral Strictures. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK564297/. Imechukuliwa 25.03.2021

6. Mathur R, et al. Comprehensive analysis of etiology on the prognosis of urethral strictures. Int Braz J Urol. 2011 May-Jun;37(3):362-9; discussion 369-70.

7. Smith TG. Current management of urethral stricture disease. Indian J Urol. 2016 Jan-Mar;32(1):27-33.

8. Hampson LA, et al. Male urethral strictures and their management. Nat Rev Urol. 2014 Jan;11(1):43-50.

9. Waterloos M, et al. Female Urethroplasty: A Practical Guide Emphasizing Diagnosis and Surgical Treatment of Female Urethral Stricture Disease. Biomed Res Int. 2019;2019:6715257. [PMC free article] [PubMed]

10. Latini JM, et al. SIU/ICUD Consultation On Urethral Strictures: Epidemiology, etiology, anatomy, and nomenclature of urethral stenoses, strictures, and pelvic fracture urethral disruption injuries. Urology.
2014 Mar;83(3 Suppl):S1-7.

11. Stefan Tritschler, et al. Urethral Stricture: Etiology, Investigation and Treatments. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3627163/. Imechukuliwa 25.03.2021

bottom of page