Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
ULY CLINIC
14 Septemba 2023, 04:02:02
Nyama puani
Nyama puani kwa jina jingine Nazo polipsi ni vinyama laini, visivyo na maumivu na si saratani vinavyoota kwenye kuta laini za ndani ya matundu ya pua au sainazi kutokana na michomo sugu. Vinyama hivi huwa na mwonekano wa zabibu zilizoning’inia kwenye kikonyo chake na huota kwenye kuta zinazozalisha majimaji ya puani.
Endapo vinyama vilivyoota si vikubwa, mtu anaweza asipate dalili zozote zile, vinavyama jinsi vinavyokuwa dalili hutokea au kuongezeka na mwisho wa siku vinyama vinaweza kukua na kusababisha shida katika upumuaji na hivyo mtu kuanza kupumulia mdomo, kupoteza uwezo wa kunusa kwa muda na maambukizi ya mara kwa mara puani.
Umri wa kupata tatizo hili
Tatizo hili linaweza mpata kila mtu kwa umri wowote ule, hata hivyo hutokea sana kwa vijana wadogo na umri wa kati.
Dalili
Dalili hutokea mara nyingi kutokanana michomo na kuvimba kwenye kuta za pua au sainazi kwa zaidi ya wiki 12. Vinyama vinapokuwa vikubwa huziba njia za hewa na hivyo kupata dalili shida wakati upumua pamoja na;
Kutokwa na makamasi
Matundu ya pua kukauka kw ndani
Kuchuruzika kwa makamasi mepesi
Kutoweza nusa au kupungua uwezo wa kunusa
Kupoteza hisia za ladha ya chakula
Maumivu ya uso au kichwa
Maumivu kwenye meno ya juu
Kuhisi mgandamizo mbele ya kichwa na usoni
Kukoroma
Kutokwa na damu puani mara kwa mara
Unapopatwa na dalili hizi ni vema ukawasiliana na daktari wako haraka
Endapo dalili hizi zimedumu zaidi ya siku 10
Unashindwa kupumua vema
Dalili kuwa kali ghafla
Kuona mawenge au kupoteza uwezo wa kuona
Kuvimba maeneo ya kuzunguka macho
Maumivu ya kichwa makalai au kuongezeka kwa maumivu ya kichwa
Visababishi
Mpaka sasa haifahamiki kinaghaubaga ni nini kisababishi halisi cha nyama puani, na kwanini baadhi ya watu wanapata tatizo hili kwa muda mrefu na kwanini uvimbe na michomo inasababisha kuvimba kwa vinyama puani kwa baadhi ya watu tu.
Vihatarishi vya kupata tatizo
Hali yoyote ile inayoweza kuamsha michomo au uvimbe puani au kwenye sainazi, kama vile maambukizi ya bakteria virusi au fangasi, aleji hukuweka hatarini kupata vinyama puani. Hali ambazo zinaonekana kuambatana na vinyama puani huwa pamoja na;
Pumu ya kifua(asthma)
Aleji na aspirini
Sinusaitizi ya aleji dhidi ya fangasi
Faibrosisi ya sistiki
Sindromu ya churg-strauss
Upungufu wa vidamin D
Vipimo
Mara nyingi daktari atatambua tatizo lako kwa kukuuliza maswali kuhusu dalili zako, kisha atakumulika kwa kifaa cha mwanga puani ili kuangalia kama kuna vinyama. Baadhi ya vipimo pia vinavyoweza kufanyika ili kumsaidia daktari kutofautisha tatizo hili na menginehuwa pamoja na;
Kipimo cha endoskopu ya pua
Kipimo cha CT scan ya kichwa
Kipimo cha damu kutambua kiwango cha vidamin D
Kipimo cha kutambua sistiki fibrosisi
Kipimo cha aleji kwenye ngozi
Matibabu
Matibabu ya tatizo hili mpaka liishe huwa na changamoto zake, utatakiwa shirikiana na daktari wako ili kupata matibabu yanayokufaa wewe ya kudhibiti dalili na kutibu visababishi vinavyoamsha tatizo lako kama vile aleji
Madhumuni halisi ya matibabu ni kupunguza viuvimbe vya puani na kuviondoa kabisa.
Matumizi ya dawa huwa ni chaguo la kwanza ingawa upasuaji unaweza ukahitajika kwa baadhi ya nyakati hata hivyo hauwezi kutoa suluhisho la mwisho kabisa kwa sababu vinyama vinaweza kujirudia tena.
Matibabu dawa
Dawa hizi huwa na malengo ya kupunguza na kuondoa vimbe za polipsi puani, vimbe zinaweza kuwa ni ndogo au kubwa. Dawa zinazotumika ni pamoja na;
Corticosteroid ya kunyunyiza puani- hupunguza uvimbe na michomo zipo aina kadhaa za dawa kwenye kundi hili kama vile Budesonide, mometasone , triamcinolone, beclomethasone , Redihaler, na ciclesonide . Wasiliana na daktari wako kwa ushauri zaidi
Dawa jamii ya corticosteroids za kuchoma au kunywa- hutumika endapo dawa za kunyunyiza zimeshindwa kufikia malengo, dawa hizi utaandikiwa na daktari wako, zinaweza kutumika pamoja na dawa za kunyunyiza puani. Fuata ushauri wa daktari
Dawa za kutibu naso polipsi na sinusaitizi sugu- daktari wako atakupatia dawa za kutibu sinusaitizi sugu na naso polipsi yenye jina la dupilumab
Dawa zingine za kupunguza aleji
Matibabu upasuaji
Kama dawa hazijafanya kazi licha ya kuzitumia kwa muda wa kutosha, daktari anaweza amua kukupa matibabu ya upasuaji wa kutumia kamera ndogo inayopita puani ili kutoa vinyama puani.
Upasuaji huu huwa unaweza fanyiwa na kwenda nyumbani siku hiyohiyo au siku inayofuata, utapatiwa dawa za corticosteroid za kunyunyizia puani ili kuzuia kujirudia kwa vinyama hivyo. Na pia unaweza pewa maji ya chumvi kunyunyizia puani ili kuharakisha kupona.
Madhara
Madhara yanayoweza jitokeza ni kuziba kwa matundu ya pua na sainazi kutokana na kuota kwa vinyama. Madhara ya kuziba huku hupelekea;
Kushindwa kupumua usiku- mtu husimama kupumua na kuanza kupumua tena wakati amelala. Hali hii huwa si nzuri kwani huleta madhara ndani ya mwili katika mifumo mbalimbali
Kuamka kwa asthma-kwa mtu mwenye asthma, asthma huamka kutokana na kuziba kwa njia ya hewa
Maambukizi kwenye sainazi
Kujikinga
Unaweza kupunguza uwezekano wa kupata au kujirudia kwa vinyama puani kwa kufanya yafuatayo;
Dhibiti aleji na asthma kwa kufuata ushauri wa daktari na matibabu aliyokupa. Endapo dalili hazijaisha rejea kwa daktari wako kukubadilishia mpango wa matibabu.
Zuia vichokoza pua- zuia kwa jinsi unavyoweza vitu vyoyote vinavyochokoza pua kama vile uchafu wkenye hewa unaoletwa na vumbi, moshi wa sigara, mvuke wa kemikali, pafyumu, mavi ya wanyama na uchafu mdodo mdogo kwenye hewa.
Kuwa msafi- nawa mikono yako kwa maji safi na sababuni mara unapotoka kwenye mikusanyiko, hii itakusaidia kupunguza idadi ya bakteria na virusi mikononi mwako kabla ya kushika maeneo ya pua.
Ongeza unyevu wa hewa nyumbani kwako- tumia vifaa maalumu kama air conditioner au humidifier ili kuongeza unyevunyevu kwenye hewa ndani ya nyumba yako. Hakikisha unasafisha humifier ili kuondoa bakteria na virusi kila siku
Fasisha ndani ya pua yako kwa kutumia maji maalumu ya chumvi (saline), hii inaweza kufungua sainazi za pua na kufanya majimaji yatoke kirahisi na kuondoa viamsha aleji puani
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
14 Septemba 2023, 04:49:31
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
Nasal polyps. American Academy of Allergy, Asthma & Immunology. https://www.aaaai.org/conditions-and-treatments/library/allergy-library/nasal-polyps. Imechukuliwa 9.10.2020.
Clinical presentation, diagnosis, and treatment of nasal obstruction. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 9.10.2020
Safe ritual nasal rinsing. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/parasites/naegleria/ritual-ablution.html. Imechukuliwa 9.10.2020
Chronic rhinosinusitis: Clinical manifestations, pathophysiology and diagnosis. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 9.10.2020
Mayo clinic. Nasal polyps. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/nasal-polyps/symptoms-causes/syc-20351888. Imechukuliwa 9.10.2020