top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Adolf S, M.D

12 Aprili 2020 17:30:46

Saratani ya ziwa
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Saratani ya ziwa

Saratani ni mkusanyiko wa magonjwa unaohusisha uzalishwaji wa seli zisizo rasmi na usiozuilika sehemu yeyote katika mwili wa binadamu.


Mara nyingi uzalishwaji wa seli za saratani huwa hauna mwisho na huwa endelevu. Uundwaji hovyo wa seli husababisha uvimbe katika mwili wa binadamu ambao hukua na kupelekea kubanwa kwa mishipa ya damu, ubongo, mifupa, neva, ini na ogani nyingine nyingi.


Saratani husababisha kifo baada ya kupitia kipindi cha maumivu makali.


Kuna saratani zinazosababishwa na virusi mfano saratani ya shingo ya kizazi na saratani ambazo hazifahamiki visababishi.


Saratani ya ziwa ni uundwaji usio rasmi na usiozuilika wa seli za ziwa/titi na mara nyingi huanza katika seli za mirija inayotengeneza maziwa. Saratani ya ziwa hutokea kwa wanawake mara nyingi zaidi ya wanaume.


Saratani ya ziwa inaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili kupitia kwenye mishipa ya damu na mishipa ya limfuna kuathiri sehemu nyingine za mwili. Wakati mwingine saratani inaposafiri na kujishikiza sehemu nyingine ya mwili, hukua pale na kuleta madhara.


Vihatarishi


Vilivyoorodheshwa hapa chini ni vihatarishi vya kupata saratani kutokana na tafiti zilizofanyika, sio lazima kila mwenye kihatarishi anaweza kupata saratani, kuna baadhi ya watu huwa hawana vihatarishi lakini wanapata saratani ya ziwa.


 • Kuwa mwanamke -mara nyingi wanawake ndio wanaathirika sana kuliko wanaume

 • Kurithi- hii hutokana na kurithi vinasaba vya ugonjwa kutoka kwa wazazi

 • Familia kuwa na historia ya saratani ya ziwa- kama kuna mwanafamilia aliyewahi kupata saratani ya ziwa basi kunauwezekano mkubwa wa kupata saratani hiyo

 • Umri mkubwa- athari za kupata saratani ya ziwa huongezeka zaidi kadiri umri unavyozidi kuongezeka

 • Kupata mtoto ukiwa na zaidi ya miaka 35

 • Uzito mkubwa

 • Kutokufanya mazoezi

 • Mwanamke ambaye hajawahi kupata ujauzito ana hatari kubwa ya kupata saratani ya ziwa kuliko Yule aliyewahi kupata ujauzito.

 • Uvutaji sigara na

 • Matumizi ya pombe


Dalili


 • Uvimbe au ngozi ngumu ndani au karibu na titi au chini ya kwapa

 • Mabadiliko ya umbo au ukubwa wa titi moja au yote mawili

 • Mabadiliko ya rangi au umbo la chuchu

 • Ngozi ya titi kujikunja au kuwa na makunyanzi

 • Chuchu ya titi kudidimia ndani au kuingia kwa ndani

 • Kutokwa na majimaji, usaha au damu kwenye chuchu

 • Ngozi ya titi kuwa nyekundu na kuwa na magamba (kama ganda la chungwa)

 • Maumivu ya titi au chuchu

 • Kuwashwa kwa chuchu

 • Kuhisi uvimbe ndani ya ziwa

 • Kuwashwa kwa titi

 • Kuhisi titi kuwa gumu, kuuma au kuwa na joto sana ukishika

 • Kuongezeka ukubwa kwa uvimbe ndani ya chuchu

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

19 Julai 2023 20:03:53

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1)Definition of cancer at https:// www.medinenet.com/cancer/article.htm# what is cancer. Imechukuliwa 9/4/2020

2)CDC. Breast cancer definition at https://www.cdc.gov/cancer/breast/basic_info/index.htm . Imechukuliwa 9/04/2020

3)Mayo clinic. Breast cancer. https://www.mayoclinic.org/disease-conditins/breast-cance/symptoms-causes/syc-20352470. Imechukuliwa 09/04/2020


4)Cancer treatment centre for America. Breast cancer symptoms. https://www.cancercenter.com/cancer-types/breast-cancer/symptoms. Imechukuliwa 9/04/2020

bottom of page