top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

24 Juni 2020 09:27:20

Vipele machoni
shahawa-zenye-damu-ulyclinic-compressor.

Vipele machoni

Vipele ndani ya kope za macho ni vipele vinavyotokea kutokana na kuziba kwa mirija inayopitisha mafuta. Kope za macho zimetengenezwa na ngozi pamoja na tezi zinazozalisha mafuta ili kufanya ngozi hiyo isikauke. Mirija hii inapoziba husababisha mafuta kushindwa kutoka na hivyo kuleta maambukizi ya bakteria kwenye mrija hiyo iliyoziba hatimaye uvimbe kuongezeka na kuambatana na dalili mbalimbali kama zilivyoorodheshwa katika Makala hii.


Unaweza kupata kipele kimoja au vingi au kwenye macho yote mawili.Kumbuka: Vipele hivi vinaweza kutokea nje au ndani ya kope za macho.


Visababishi


Kisababishi kikubwa ni kuziba kwa mirija inayopitisha mafuta katika ngozi ya kope


Visababishi vingine

 • Ugonjwa wa xanthelasma- husababisha kipele chenye mwinuko mdogo ndani ya kope vinavyotokea kwa kadri mtu anavyongezeka umri. Vipele hivi si hatari igawa vinaweza kuashiria kuongezeka Zaidi kwa kolestro mwilini.

 • Vipele vya papiloma- ni vipele vyenye rangi ya pinki, huwa havina shida yoyote na huweza kukua taratibu na kuathiri kuona kwako na wakati mwingine huweza kuota nje ya kope ya jicho. Huweza kundolewa kwa njia ya upasuaji mdogo.

 • Vifuko vya maji- Hivi huwa ni vijifuko vy amaji vinavyoota kwenye macho


Dalili


 • Kuhisi macho yana mchanga au yanakwaruza

 • Macho kuongeza hisia dhidi ya mwanga(hivyo kuathiriwa na mwanga na kutoa machozi)

 • Kutoa machozi

 • Maumivu ya jicho yakishindwa au kufikitwa


Vihatarishi


Vihatarishi vinavyoweza kusababisha kupata tatizo hili ni;


 • Kushika macho bila kunawa

 • Kutumia lenzi za kuvaa machoni

 • Kuacha mekup kwenye macho wakati w akulala

 • Kutumia mafuta au vipodozi vilivyoisha muda wa matumizi

 • Ugonjwa wa blepharitis

 • Kuwana ugonjwa wa rosacea


Matibabu


Mara nyingi vipele hivi huweza kuisha vyenyewe baada ya muda wa wiki kadhaa, hata hivyo isipoisha tafuta matibabu kutoka kwa daktari wako.


Matibabu ya nyumbani

 • Tumia maji ya uvuguvugu kwenye jicho lenye shida, kanda kwa dakika 10 fanya hivi mara 4 kwa siku

 • Usitumie vipodozi au mafuta yaliyokwisha muda wake wa matumizi

 • Tibiwa ugonjwa wa blepharitis au rosacea kama unao

 • Usijaribu kukamua au kutoboa vipele hivi mwenyewe ukiwa nyumbani, acha viondoke vyenyewe au wasiliana na daktari wako

 • Usitumie lensi za kuvaa ndani ya kope za macho mpaka vipele vipone

 • Onana na daktari wako kwa ushauri Zaidi


Dawa

Daktari anaweza kukupa antibayotiki kama anahisi unamaambukizi yanayoambatana na vipele hivyo. Hata hivyo mara nyingi vipele hivi huwa haviondoki kwa tiba ya dawa za antibayotiki. Endapo tiba ya dawa imeshindikana au havijaondoka vyenyewe ni vema kubadili tiba.


Tiba ya upasuaji

Daktari atakufanyia upasuaji mdogo wa kuondoa vipele hivi. Vipele hivi vinaweza kujirusia baada ya miezi kadhaa kupita, hata hivyo huweza kujirudia sehemu ileile, sehemu nyingine au jicho jingine


Kujikinga


Nawa mikono yako izuri kabla ya kushika macho yako. Kama unapata sana vipele hivi, ni vema ukawa unaondoa mafuta yaliyozidi kwa umakini katika pembe za kope zako. Tumia mafuta ya samaki katika chakula, mafuta haya huzuia hatari ya kupata aina hii ya vipele. Unaweza kuyapata kwa kula samaki aina ya sangara.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Imeboreshwa, 

8 Oktoba 2021 04:53:54

Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini

[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]

Rejea za mada

1.Chalazion and hordeolum. Merck Manual Professional Edition. http://www.merckmanuals.com/professional/eye-disorders/eyelid-and-lacrimal-disorders/chalazion-and-hordeolum-stye. Imechukuliwa 24.06.2020

2.Eye cosmetic safety. U.S. Food and Drug Administration.http://www.fda.gov/Cosmetics/ProductsIngredients/Products/ucm137241.htm. Imechukuliwa 24.06.2020

3.Lindsley K, et al. Interventions for acute internal hordeolum. Cochrane Database of Systematic Reviews. http://onlinelibrary.wiley.com/doi/10.1002/14651858.CD007742.pub3/abstract. Imechukuliwa 24.06.2020

4.Wash your hands. Centers for Disease Control and Prevention. http://www.cdc.gov/Features/HandWashing. Imechukuliwa 24.06.2020

5.Using eye makeup. American Academy of Ophthalmology. http://www.geteyesmart.org/eyesmart/living/eye-makeup.cfm. Imechukuliwa 24.06.2020

6.Dupre AA, Wightman JM. Red and painful eye. In: Walls RM, Hockberger RS, Gausche-Hill M, eds. Rosen's Emergency Medicine: Concepts and Clinical Practice. 9th ed. Philadelphia, PA: Elsevier; 2018:sura ya 19.
7.Yanoff M, Cameron JD. Diseases of the visual system. In: Goldman L, Schafer AI, eds. Goldman-Cecil Medicine. 25th ed. Philadelphia, PA: Elsevier Saunders; 2016:sura ya 423.

bottom of page