Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
28 Oktoba 2021 05:48:41
Vipele mgongoni
Mwonekano wa vipele au uvimbe mgongoni unaweza kutokana na kuchomoza kwa tishu za kawaida kama vile misuli, tishu unganishi, ngozi na mifupa na mishipa ya fahamu, licha ya kuweza changiwa pia na magonjwa mengine ya ngozi. Dalili na sifa za vipele hutumiwa na daktari ili kutambuakama ni kipele cha kawaida au la.
Ni nini husababisha vipele mgongoni?
Magonjwa yaliyoorodheshwa hapa chini husababisha vipele mgongoni na wakati mwingine huweza kusababisha uvimbe mkubwa badala ya kipele kidogo.
Visababishi vikuu
Visababishi vikuu ambavyo maelezo yake yapo hapa chini ni;
Maelezo ya ziada kuhusu visababishi yanapatikana kwenye aya zinazofuata.
Maumbile ya kawaida ya mgongo
Uvimbe au kuchimoza kwa misuli, mishipa ya fahamu, mafuta chini ya ngozi, tezi limfu, au shina la nywele linaweza kusababisha hisia au mwonekano wa kipele mgongoni ambavyo ni vya kawaida na huweza kuonekana kwa kila mtu.
Madhaifu ya mishipa ya fahamu na mifupa
Mifupa na mishipa ya fahamu inaweza kupata uvimbe wa aina yoyote ile kutokana na madhaifu katika ukuaji wa tishu hizi, matokeo yake ni kuonekana kwa uvimbe unaoweza kuwa wa kawaida au saratani. Unapoona ishara ya uvimbe haswa unaoambatana na daily zingine kama maumivu unapaswa kuonana na daktari kwa uchunguzi.
Magonjwa ya ngozi
Magonjwa ya ngozi yanaweza kutokea kwenye tishu mbalimbali zilizotengeneza mgongo kama vile saratani ya melanoma n.k
Tezi limfu
Tezi limfu zinapopata maambukizi huvimba na kutengeneza kipele kidogo au uvimbe mkubwa mgongoni. Dalili zingine za homa au maumivu huweza kuambatana na uvimbe wa tezi limfu.
Saratani
Inaweza kuwa saratani iliyoanzia kwenye tishu mbalimbali kama mifupa ngozi n.k au saratani iliyosambaa mgongoni kutoka kwenye maeneo mengine ya mwili. Mfano wa saratani zinazoweza kutokea kwenye mgongo ni saratani ya basal seli, melanoma n,k
Sisti yenye maji
Sisti ni uvimbe uliotengenezwa na kwa kuta za epithelia na hukaliwa na maji, hewa, mafuta au vitu vingine ndani yake. Siti ya maji ni kifuko kilichojazwa na maji ambacho huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili ikiwa pamoja na mgongo.
Lipoma
Lipoma ni uvimbe wa mafuta na huwa si saratani. Uvimbe huu hukaa kati ya ngozi na misul na hutokea sana baada ya kuvuka umwi wa miaka 40.
Lipoma huwa na sifa ya kutembea unapoguswa na hauna maumivu isipokuwa kama umeota karibu na mshipa wa fahamu. Na huweza tokea maeneo yoyote ikiwa pamoja na mgongo.
Jipu la ngozi
NI kifuko kinachofanyika chini ya ngozi na hujazwa na usaha na husababishwa na maambukizi ya bakteria chini ya ngozi yanayoingia baada ya kujitoboa, kujikata au kujikwangua.
Dalili huwa pamoja na kukua umbile, rangi nyekundu pembezoni, maumivu na homa wakati mwingine. Kama jipu lisipotibiwa hukua na kuweza sambaa maeneo ya pembeni.
Sunzua
Sunzua huweza kuwa mithili ya upele mdogo namrefu au uliosambaa kama uyoga na huota kwenye usawa wa juu ya ngozi.
Huweza kutokea kama mmoja au kwenye kundi na husababishwa na maambukizi ya kirusi cha human papillomavirus (HPV). Kirusi HPV huambukizwa kwa kugusa majimaji ya kidonda au kwa njia ya kufanya ngono.
Forunko
Forunko ni maambukizi ya bakteria kwenye shina la nywele yanayoweza kutokea sehemu yoyote ya mwili. Maambukizi hutokea kutokana na msuguano kati ya mgongo na kitu chochote kinachoweza kusababisha mpasuko kwenye ngozi ya mgongo na hivyo kupelekea bakteria kuingia.
Hutokea sana kwa watu wenye mfumo dhaifu wa kinga ya mwili kama vile wenye kisukari na magonjwa mengine sugu.
Dalili huwa pamoja na kuvimba au kipele, kilicho na rangi nyekundu, kinachouma na chenye usaha kama kikitumbuliwa.
Chunusi
Chunusi huwa ni vipele vidogo vinavyotokea sehemu ambapo kuna tezi za mafuta. Chunusi kwa ndani huwa zimejazwa namafuta, uchafu, bakteria au ngozi mfu.
Huweza kuonekana baada ya kubarehe kutokana na homon kuhamasisha ngozi kuzalisha mafuta na hivyo kuweza pelekea kuziba kwa vitundu vya mafuta na kutengeneza chunusi.
Dalili zake huwa pamoja na mwonekano wa kipele kilichoinuka kutoka chini ya ngozi, chenye kichwa cheupe au cheusi
Angioma ndogo
Angioma ni vipele vidogo vyenye rangi nyekundu visivyo na madhara vinavyotokea sana kuanzia umri wa miaka 40 na kuendeea. Kipele hiku huanzia kwenye kuta za mishipa ya damu.
Vipele mshikizo
Vipele mshikizo ni vipele vidogo vinavyoning’inia juu ya ngozi na huwa havina shida yoyote. Hutokea sana kwenye maeneo ya shingo, kufua, mgongo na kwapani. Soma zaidi kuhusu vipele mshikizo sehemu nyingine katika tovuti hi.
Matibabu
Matibabu ya vipele vya mgongoni hutegemea kisababishi, onana na daktari wako kwa uchuguzi ili kupata matibabu kulingana na kisababishi.
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Imeboreshwa,
19 Julai 2023 20:02:12
Soma dalili zingine Zaidi kwa kubonyeza herufi ya mwanzo hapa chini
​
[A] [B] [C] [D] [E] [F] [G] [H] [I] [J] [K] [L] [M] [N] [O] [P] [Q] [R] [S] [T] [U] [V] [W] [X] [Y] [Z] [Z] [#]
Rejea za mada
1. NCBI. Skin tag. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK547724/. Imechukuliwa 28.10.2021
2. NCBI. Detecting melanoma. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK321126/. Imechukuliwa 28.10.2021
3. NCBI. Acne Vulgaris. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK459173/. Imechukuliwa 28.10.2021
4. NCBI. Malignant Melanoma. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470409/.Imechukuliwa 28.10.2021
5. NCBI. Epidermoid Cyst. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK499974/. Imechukuliwa 28.10.2021
6. NCBI. Lipoma. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK507906/. Imechukuliwa 28.10.2021
7. NCBI. Cherry Hemangioma. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK563207/. Imechukuliwa 28.10.2021
8. NCBI. Boils and carbuncles: Overview. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK513141/. Imechukuliwa 28.10.2021
9. NCBI. Warts. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK279586/. Imechukuliwa 28.10.2021