Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Utangulizi
​
UKIMWI ni ugonjwa sugu, unaotishia Maisha na husababishwa na Kirusi cha ukimwi (VVU)
Kirusi huyu huvamia kinga zamwili na kusababisha mwonekano wa dalili mbalimbali zinazoitwa UKIMWI. Hivyo Tukisema UKIMWi tunamaanisha mwonekano wa dalili mbalimbali kwa mtu mwenye maambukizi ya ukimwi.
Matumizi ya dawa za VVU huweza kuzuia mwendelezo wa mgonjwa kupata dalili za UKIMWI
Dawa hizi kwa sasa Tanzania hutolewa Bure na muda wowote ule mara unapopata maambukizi ya ukimwi
Dalili za awali za maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi ni pamoja na
Kuonyesha dalili za kuwa na mafua ndani ya wiki mbili toka umepata maambukizi
​
Dalili hii inaweza kudumu kwa wiki kadhaa na kuondoka
-
Homa
-
Maumivu ya kichwa
-
Maumivu ya misuli
-
Maumivu ya maungio ya mwili(jointi)
-
Harara
-
Koo kuwa kavu
-
Vidonda mdomoni vinavyouma
-
Kuvimba mitoki, haswa ya shingoni
-
Kuharisha
-
Kupoteza uzito(kupungua uzito)
-
Kikohozi(kukohoa)
-
Kutokwa jasho wakati wa usiku
​
Dalili hizi zinaweza kuwa za wastani na mtu anaweza asizishitukie
Dalili za kuendelea kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni pamoja na;
Jinsi VVU vinavyozidi kuharibu mfumo wa kinga wa mwili, mwili utaanza kuonyesha dalili za UKIMWI ambazo huwa sugu kama vile;
​
-
Homa
-
Mwili kuchoka
-
Kuvimba mitoki- kama dalili ya kwanza ya maambukizi
-
Kuharisha
-
Kupungua uzito
-
Maambukizi ya fangasi kooni
-
Mkanda wa jeshi
-
Nimonia(pneumonia)
Dalili za Mtu anayeelekea kupata UKIMWI au za mtu mwenye UKIMWI ni;
Dalili za UKIMWI mara nyingi huwa hazitokei kwa watu Wenye maambukizi ya VVU na tayari wamesha anza dawa mapema toka walipogundulika. Endapo mtu hajapata dawa huchukua takribani wastani wa miaka 8 hadi 10 kupata dalili za UKIMWI. UKIMWI unapompata mtu Kinga za mwili huwa chini kiasi cha kutosha na hivyo mtu huweza kuambukizwa magonjwa mbalimbali na kuonyesha dalili za UKIMWI.
Dalili za UKIMWI ni pamoja na
​
-
Kutokwa jasho
-
Kutetemeka mwili(homa)
-
Homa za kujirudia
-
Tatizo sugu la kuharisha
-
Kuvimba mitoki na tezi
-
Tatizo sugu la Ulimi kuwa mweupe na fangasi wa kinywani
-
Kuchoka mwili kusikoelezeka na kusipokuwa na sababu ya msingi
-
Mwili kuwa dhaifu
-
Kupoteza uzito
-
Vipele na harara kwenye Ngozi
Soma zaidi kuhusu UKIMWI kwa kubonyeza hapa
​
Kumbuka wasiliana na daktari wako siku zote endapo umeona kuwa unadalili zilizotajwa hapa na umekuwa na kihatarishi
​
​
Imeboreshwa 05.06.2020
​