Cajanus cajan
Imeandikwa na:
ULY CLINIC
8 Julai 2021, 18:22:33


Utangulizi
Mmea Cajanus cajan umekuwa ukitumika kama tiba asili kutibu kuharisha, ambao una asili ya India, na Afrika. Cajanus cajan kwa sasa unapatikana maeneo mengi duniani katika ukanda wa tropiki na hufahamika Kiswahili kama Mbaazi.
Sifa za mmea Cajanus cajan
Mbaazi huweza kurefuka na kufikia urefu wa mita tatu kwenda juu, maua yake huwa ya njano na yenye ukijivu . Matunda yake kwa ndani huwa na mbegu kadhaa ambazo zimefunikwa na podo nyoofu.
Uwezo Cajanus cajan kitiba
Mbaazi huwa na kampaundi ya tannins ambayo ndo kiini cha dawa kinachofanya kazi ya kuzuia kuharisha
Tafiti zinaonyesha kuwa, chembe nyekundu za damu zenye umbo la mundu ( kutokana na ugonjwa wa seli mundu) huweza kurejeshwa kwenye umbo lake la awali endapo mgonjwa atatumia dawa iliyotokana na mbegu zake.
Juisi ya majani yake hutumika kudhibiti sukari kwenye damu kwa wagonjwa wa kisukari
Unga wa mbegu zake hutia nguvu mwili
Majani yake hutibu sumu ya chakula, maumivu ya tumbo na haja ngumu
Majani, mbegu na shina bichi hutibu maambukizi ya fizi, mipasuko kwenye midomo na kusafisha kinywa
Uji wa majani yake hutumika kutibu vidonda midomoni na michomo ya kinga za mwili
Matumizi ya cajanus cajan kama dawa
Tiba ya kuharisha
Tengeneza dikoksheni ya miligramu 15 za majani kwenye lita moja ya maji na kunywa kwa siku
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.
Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.
KUMBUKA:
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
8 Julai 2021, 19:13:04
Rejea za mada hii;
1. Dilipkumar Pal, et al. Biological activities and medicinal properties of Cajanus cajan (L) Millsp. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3255353/#. Imechukuliwa 08.07.2021
2. Pal D, Sarkar A, et al. CNS depressant activities of Coccos nucifera in mice. Acta Pol Pharm. 2011;68:249–54.
3. Pal DK, et al. Antibacterial activity of Cuscuta reflexa stem and Corchorus olitorius seed. Fitoterapia. 2006;77:589–91.
4. Pal DK, et al. AK. Evaluation of CNS activities of aerial parts of Jasminum multiflorum Andr. Asian J Chem. 2007;19:4452–8.
5. Pal DK, et al. Analgesic and anticonvulsant effects of saponin isolated from the leaves of Clerodendrum infortunatum Linn. In mice. Indian J Exp Biol. 2009;47:743–7.
6. Pal DK, et al. Analgesic and anticonvulsant effects of saponin isolated from the stems of Opuntia vulgaris Mill in mice. Euro Bull Drug Res. 2005;13:91–7.
7. Mohammed R, et al. An ethnobotanical survey and pharmacological evaluation of medicinal plants used by the Garo tribal community living in netrakona district Bangladesh. Adv Nat Appl Sci. 2009;3:402–18.
8. Luo QF, Sun L, Si JY, Chen DH. Hypocholesterolemic effect of stilbenes containing extract fraction from Cajanus cajan on diet induced hypercholesterolemia in mice. Phytomed. 2008;15:932–9.
9. Ezike AC, Akah PA, Okoli CC, Okpala CB. Experimental evidence for the antidiabetic activity of Cajanus cajan leaves in rats. J Basic and Clinical Pharm. 2010;1:25–30
10. Nicholson RA, David LS, Pan RL, Xin Min Liu. Pinostrobin from Cajanus cajan (L.) Millsp. Inhibits sodium channel-activated depolarization of mouse brain synaptoneurosomes. Fitoterapia. 2010;81:826–9.
11. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
12. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
13. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
14. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
15. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
16. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
17. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021