Majani na magamba au magome mti wa Acacia nilotica hutibu maumivu ya jino, matunda yake huwa na kiasi kikubwa cha tannins inayotibu ugonjwa wa kuhara damu na kubadilisha rangi ya ngozi kuwa nyeusi zaidi endapo itapakwa kwenye ngozi.
Achillea millefolium ni mmea ambao una asili ya Ulaya, uwezo wake wa kutibu maradhi unafahamika kwa muda mrefu sana na umekuwa ukiwasaidia askari wakati wa vita kutibu na kukata damu inayotoka kwenye majeraha mbalimbali.
Mmea wa Acorus calamus hufanya kazi ya kutuliza mfumo wa fahamu, kutubu magonjwa mbalimbali yanayohusiana na mmeng'enyo wa chakula, harara na uvimbe wa yutikaria.
Adansonia digitate ni jina la kisanyansi la mbuyu, lichaya kutumika kama chakula toka enzi, sehemu mbalimbali za mbuyu zimekuwa zikitumika kama tiba ya kuharisha, kuondoa michomo na kuzuia au kutibu matege
Mmea huu hutoa harufu unapo fikitwa, hii huelezea uwezo wake wa kichawi na kitiba na matibabu ya magonjwa ya akili. Hutumika pia kwenya matibabu ya magonjwa ya macho, majeraha ya kuungua na nimonia kwa kupaka kifuani