top of page

Carica Papaya

Imeandikwa na:

@ ULY CLINIC

30 Juni 2021 20:34:26

Utangulizi

Ni mti ambao asili yake ni Amerika ya kati, kwa sasa unalimwa na kustawi vema maeneo mbalimbali Afrika. Matumizi ya mpapai ni mengi na imeandikwa kwenye kumbukumbu kwamba mazao yote ya mpapai yana uwezo kitiba wa kitibu njano, utomvu wake hutibu minyoo, mizizi na majani yake huwa na uwezo wa kupunguza maji mwilini.

Kwa matibabu ya manjano baadhi ya nchi zimekuwa zikichemsha tunda lake ambalo halijaiva na kuongezea na kuku pamoja na majani ya Tinospora bakis kama kiongeza hamu ya kula.

Sifa za mme wa carica papaya

Mpapai huweza kuwa na kufikia urefu wa mita 2 hadi 10, na kuwa na majani sehemu yake ya juu ambapo.

Mpapai huwa na utomvu karibia sehemu zote kuanzia majani, shina na tunda lake. Matunda yake ni matamu na yenye rangi mbalimbali kwa ndani mfano njano, nyekundu n.k

Uwezo wa carica papaya kitiba

Magamba ya mpapai hutumika katika matibabu ya manjano, tafiti nyingi zimeshafanyika kuhusu uwezo wake huu na kutambua uwezo wake mkubwa.

Kimeng’enya cha papain kilicho kwenye mmea huu, kina uwezo wa kuua minyoo sindano, minyoo mviringo na trikephale na ndio maana huwa na uwezo wa kutumika kwenye matibabu ya minyoo.

Majani ya mpapai huwa na uwezo wa kutibu ugonjwa wa malaria

Matumizi ya carica papaya kama tiba asili

Kwa matibabu ya manjano

Chukua papai bichi au gramu 10 za mizizi ya iliyosagwa kisha changanya na kitu chochote kama kuku ili ili utengeneze mlo wako wa dawa.

Matibabu ya minyoo

Ili kutibu minyoo sindano na mviringo

Lina gramu 4 hadi 8 za utomvu wa papai bichi kwa kunywa mtoto gramu 8 hadi 12 kwa mtu mzima.

Baada ya kutumia utomvu, unapaswa kutumia dawa za kulegeza matumbo (dawa za kufanya uendeshe) ili kufanya minyoo waliokufa kutoka kwenye utumbo.

Majina mengine ya dawa asili ya carica papaya

Dawa hii hufahamika kwa carica papaya majina mengine kama;

• Dawa asili ya minyoo
• Dawa asili ya manjano
• Dawa asili ya malaria

Kazi zingine za carica papaya

Huweza kutibu tatizo la choo kigumu kwa kula matunda yaliyoiva.

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2021 10:33:54

Rejea za mada hii;

1. L O Onaku, et al. Antagonistic antimalarial properties of pawpaw leaf aqueous extract in combination with artesunic acid in Plasmodium berghei-infected mice. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/21715732/#. Imechukuliwa 30.06.2021

2. Kalimuthu Kovendan,et al. Antimalarial activity of Carica papaya (Family: Caricaceae) leaf extract against Plasmodium falciparum. https://www.researchgate.net/publication/233778301_Antimalarial_activity_of_Carica_papaya_Family_Caricaceae_leaf_extract_against_Plasmodium_falciparum. Imechukuliwa 30.06.2021

3. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021

4. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021

5. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021

6. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021

7. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021

8. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021

9. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021

bottom of page