Caulophyllum thalictroides
Imeandikwa na:
Dkt. Benjamin L, MD
1 Agosti 2021 17:55:31
Utangulizi
Caulophyllum thalictroides ni mmea poli wenye uwezo wa kitiba na una asili ya Amerika kaskazini. Mmea huu hufahamika kama dawa ya kuimarisha misuli ya kizazi. na hufahamika kwa jina jingine la ‘blue cohosh’
Sifa za mmea Caulophyllum thalictroides
Caulophyllum thalictroides ni mmea asili wenye asili ya pwani ya mashariki ya Amerika kaskazini. Mmea huu hukua mwaka mzima. Caulophyllum thalictroides umekuwa ukitumiwa kwa miaka mingi na Wahindi kuwaponya wanawake waliotoka kujifungua na kuongeza uchungu. Mmea huu umekuwa na matumizi kwa wanawake ingawa unaweza kutibu maumivu ya maungio kutokana na michomo kinga (athraitiz).
Uwezo wa Caulophyllum thalictroides kitiba
Mmea huu unafahamika kutumiwa na wanawake wa Kihindi kuharakisha kujifungua kwa kuongeza uchungu. Ulitumika pia kurekebisha mzunguko wa hedhi, kuondoa hedhi nyingi na kupunguza maumivu ya hedhi.
Mizizi ya Caulophyllum thalictroides huweza kufanya kazi kama dawa za uzazi wa mpango.
Matumizi katika tiba ya kisasa
Wataalamu wa tiba asilia India wanafahamu uwezo wa matunda ya Caulophyllum thalictroides na wamekuwa wakitumia kama dawa ya kuongeza uchungu, kupunguza maumivu kutokana na hedhi au ovari.
Matumizi mengine ya Caulophyllum thalictroides kama dawa asili
• Kupunguza maumivu ya tumbo kutokana na mijongeo ya misuli laini
• Kupunguza vichomi vya tumbo
• Kupunguza haja ngumu
• Kutibu kwikwi
• Kutibu baridi yabisi
• Dalili kali kabla ya hedhi
• Kutibu koo linalouma
Matumizi ya Caulophyllum thalictroides katika tiba
Dikoksheni hutibu maumivu ya hedhi na maumivu ya maungio ya mwili kutokana na michomo kinga
Tinkcha ya dawa hutolewa kwa mama mwenye uchugnu ili kuharakisha kuzaa kwa kuongeza mjongeo wa misuli ya kizazi na pia hutumika kupunguza maumivu ya uzazi
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.
Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.
KUMBUKA:
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Agosti 2021 17:55:31
Rejea za mada hii;
1. Dugoua JJ, et al. "Safety and efficacy of blue cohosh (Caulophyllum thalictroides) during pregnancy and lactation." Can J Clin Pharmacol. 2008 Winter;15(1):e66-73.
2. Lee Y, et al. "Anti-Inflammatory Effect of Triterpene Saponins Isolated from Blue Cohosh (Caulophyllum thalictroides)." Evid Based Complement Alternat Med. 2012;2012:798192.
3. Wu M, et al. "Teratogenic effects of blue cohosh (Caulophyllum thalictroides) in Japanese medaka (Oryzias latipes) are probably mediated through GATA2/EDN1 signaling pathway." Chem Res Toxicol. 2010 Aug 16;23(8):1405-16.
4. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
5. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
6. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
7. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
8. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
9. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
10. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021