top of page

Euphorbia hirta

Imeandikwa na:

Dkt. Benjamin L, MD

3 Agosti 2021 17:44:13

Utangulizi

Euphorbia hirta ni mmea unaofahamika duniani kote kutokana na uwezo wake mkubwa katika tiba asilia, haswa kutibu matatizo ya wanawake, magonjwa ya mfumo wa upumuaji, minyoo, amibiasis, kisonono n.k.

Sifa za mmea Euphorbia hirta

• Ni moja ya magugu poli
• Huweza kustawi kwenye hali ya hewa ya ujoto pembezoni mwa barabara
• Huwa mwembamba wenye shina
• Hustawi vipindi fulani katika mwakana huwa na vinyweleo na matawi mengi kuanzia kwenye shina mpaka kwenye kilele
• Hukua kufikia urefu wa sentimita 40
• Huwa na rangi nyekundu au zambarau
• Majani yake huwa na rangi kijanimkolezo kwa juu na iliyopauka kwa chini na urefu wa sentimita 1 hadi 2.5
• Matunda yake huwa na rangi ya njano
• Mbegu zake huwa zimekunjamana

Uwezo wa kitiba Euphorbia hirta

Mmea huu una kemikali za alkanes, triterpenes, phytosterols, tannins, polyphenols na flavonoids na umekuwa ukitumika katika tiba asili Afrika na India kutibu magonjwa yafuatayo;

• Magonjwa ya wanawake
• Kikohozi
• Bronkaitiz
• Pumu ya kifua
• Minyoo kwa watoto
• Kuhara damu
• Manjano
• Chunuzi
• Kisonono
• Matatizo ya mfumo wa chakula
• Uvimbe

Uwezo wake mwingine ni;

• Kushusha shinikizo la damu
• Kuondoa hofu na wasiwasi
• Hushusha homa
• Huondoa maumivu
• Hupunguza maumivu kutokana na michomo kinga
• Hutibu vipele vya macho
• Hutibu malenge lenge ya moto au msuguano
• Kuua vimelea vya maradhi Escherichia coli, Staphylococcus aureus, Pseudomonas aeruginosa, na Bacillus subtili
• Kutibu malaria
• Kutibu fangasi

Maudhi ya Euphorbia hirta

• Hupunguza uwezo wa manii kujongea( hupunguza uwezo wa mwanaume kutungisha mimba wakati wa matumizi)
• Kuchefuchefu
• Kutapika

Tahadhari kwa watumiaji Euphorbia hirta

Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa wajawazito na wanaonyonyesha kwa kuwa inaweza kusababisha madhara ambayo hayajulikani.

Kuna ushahidi kwamba kunywa dawa hii wakati wa ujauzito kwa kuwa inaweza sababaisha ongezeko la mjongeo wa misuli ya kizazi, huweza kutoa mimba.

Matumizi ya Euphorbia hirta kama dawa

Kwa kunywa gramu 100 za dikoksheni ya mmea kwa muda wa siku tatu, hutibu amibiasis au kuharisha damu.

Kwa kunywa gramu 100 za dikoksheni ya mmea huondoa kushikwa na pumu ya kifua kwa kutanua kipenyo cha njia ya hewa.

Ustahimilivu wa matumizi ya dawa hii ni mkubwa kwa wagonjwa wengi.

Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea

​

Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia

​

Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.

​

Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.

​

Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia

​

Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.

​

Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.

​

Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.

​

Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.

 

Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa

 

Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.

​

Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa

 

Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.

​

Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa

 

Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika.  Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.

 

Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika

​

Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol  au maji.

 

Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.

​

Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa

 

Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.

​​

KUMBUKA:

 

Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.

 

Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano

​

Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Agosti 2021 17:44:13

Rejea za mada hii;

1. Euphorbia hirta. https://plants.ces.ncsu.edu/plants/euphorbia-hirta/. Imechukuliwa 03.08.2021

2. Sunil Kumar, et al. Euphorbia hirta: Its chemistry, traditional and medicinal uses, and pharmacological activities. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3249903/. Imechukuliwa 03.08.2021

3. Prajapati ND, et al. Agarbios; 2003. Handbook of Medicinal Plants.

4. Kirtikar KR, et al. Dehradun, India: Oriental Enterprises; 2003. Indian medicinal plants with illustrations.

5. Nadkarni KM. 4th. Bombay, India: Popular prakashan; 1976. Indian Materia Medica.

6. Sood SK, et al. India: Scientific Publishers; 2005. Ethnic Indian Plants in cure of diabetes.

7. Singh P, et al. Inhibition of aflatoxin production on some agricultural commodities through aqueous plant extracts. J Indian Bot Soc. 1986;65:30–2.

8. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021

9. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021

10. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021

11. Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021

12. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021

13. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021

14. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021

bottom of page