Griffonia Simplicifolia
Imeandikwa na:
Dkt. Benjamin L, MD
2 Agosti 2021 19:04:41
Sifa za mmea Griffonia simplicifolia
Griffonia simplicifolia ni mmea poli jamii ya kunde unaotambaa kwenye mimea mingine katika ukanda wa savanna na mapoli ya Afrika Magharibi. Urefu wake huweza kufikia mita 3, hutoa maua ya kijani na huzalisha mbegu zilizofunikwa kwa podo jeusi.
Mizizi, majani, maua, matunda na mbegu zake hutumiwa na wataalamu wa tiba asili kama dawa ya magonjwa mbalimbali yanayohusiana na mfumo wa kati wa fahamu, hata hivyo kiwango kikubwa cha kemikali ya 5-HTP hupatikana kwenye mbegu zake.
Magonjwa yanayotibiwa na Griffonia simplicifolia
Mbegu za Griffonia simplicifolia huwa na uwezo wa kutibu;
• Msongo wa mawazo
• Kujidharau
• Kula sana
• Maumivu ya misuli
• Kuzuia uzee wa haraka
• Homa ya mjongeo
• Obeziti
• Kukosa usingizi
• Sonona
• Hofu kuu
• Maumivu ya kichwa
• Matatizo ya tumbo
• Kutibu vidonda
Namna Griffonia simplicifolia unavyofanya kazi ya kutibu
Mbegu za Griffonia simplicifolia huwa na kemikali yenye jina la 5-HTP inayofahamika kufanya kazi kwenye mfumo wa kati wa fahamu kwa kuuchochea uzalishe homon serotonin.
Serotonin ni homon muhimu inayorekebisha usingizi, hamu ya chakula, maumivu na hali ya moyo hivyo ni kiini muhimu kwenye magonjwa ya sonona, kukosa usingizi na obeziti.
Matumizi ya Griffonia simplicifolia kama dawa
• Griffonia simplicifolia hupatikana kwenye fomu ya kidonge au unga kwenye maduka ya dawa asili na virutubisho. Hutumika katika dozi kati ya miligramu 50 hadi 100 za kiini cha dawa kutibu matatizo yaliyotajwa hapo awali na mara nyingi dozi 1 hadi 4.
• Hupendelewa kutumika nyakati za usiku ili kuzuia hali ya kusinzia mchana
• Madhara ya dawa kwenye damu yanaweza kudumu kwa muda wa mwezi mmoja hadi mitatu, hivyo kwa tiba ya kudumu unapswa kuwasiliana na daktari wako.
Maudhi ya Griffonia simplicifolia
Matumizi ya dawa kwa kunywa Griffonia simplicifolia ni salama endapo itatumika hadi wiki nane. Usalama wa matumizi ya muda mrefu bado haufahamiki. Baadhi ya watu wanaotumia Griffonia simplicifolia hupata maudhi ya;
• Kuharisha
• Maumivu ya tumbo
Maudhi mengine hutegemea kiwasi cha dawa uliyotumia na yanaweza kuhusisha;
• Mapigo ya moyo kwenda mbio
• Mzio wa ngozi
• Usingizi
• Maumivu ya kichwa
• Madhaifu ya misuli
• Kichefuchefu na kutapika
• kuharisha
Tahadhari ya matumizi ya Griffonia simplicifolia
Tahadhari inapaswa kuchukuliwa kwa wajawazito na wanaonyonyesha kwa sababu hakuna tafiti zilizoangalia madhara ya matumizi ya mmea huu katika kipindi hiki.
Namna ya kuandaa aina mbalimbali za dawa kutoka kwenye mmea
​
Namna ya kuandaa infusheni ya dawa asilia
​
Infusheni huandaliwa kwa kuzamisha sehemu ya mmea unayotaka kutumia kama dawa kwenye kiasi cha maji yaliyochemka. Baada ya kuzamisha kwenye maji yaliyochemka, maji hayo huchujwa baada ya dakika 15. Dozi ya dawa inayotakiwa kuandaliwa kwa wastani huwa ni gramu 1 kwa kila mililita 10 za maji.
​
Kuna dawa nyingi asilia zimeshatengenezwa na kufungwa kwenye vifungashio vya karatasi ambapo unaweza kutumia kirahisi kama majani ya chai ya kuchovywa. Dawa kwenye fomu hiyo zitapunguza muda wa kuandaa.
​
Namna ya kuandaa dikokshen ya dawa asilia
​
Dikokshen hutumika kuvuna kiini cha dawa ambacho hakiathiriwi na joto.
​
Ili kuandaa dikokshen ya dawa, chemsha magome au mizizi ya mmea kwa muda wa dakika 15 hadi 60 (hutegemea aina ya mmea au kiini cha dawa), kisha pooza na ongeza maji ya baridi ili kutengeneza kiasi cha dawa na wingi wa kiini unachohitaji.
​
Endapo dawa inatakiwa kuchemka kwa muda mrefu, unatakiwa ongezea kiasi cha maji yaliyopotea ili dawa isiungue.
​
Dozi ya dikoksheni ni sawa na infusheni yaani gramu moja ya mmea kwa mililita 10 za maji isipokuwa endapo dawa ina uteute mwingi, gramu moja inatakiwa kuchanganywa na mililita 20 za maji.
Namna ya kuandaa mmengenyo wa dawa
Kuandaa mmeng’enyo wa dawa kwa njia hii unatakiwa weka dawa yako kwenye chombo kisha ongeza maji yenye joto linalotakiwa, mara nyingi joto linatakiwa kuwa kati ya nyuzi za sentigrade 35 hadi 40 ikitegemea aina ya dawa. Lengo kuu la kuzingatia joto ni kutoharibu kiini cha dawa ambacho kinategemea joto.
​
Namna ya kuandaa masalesheni ya dawa
Ili kuandaa masalesheni ya dawa, saga au katakata dawa kwenye vipande vidodo vidogo sana kisha weka kwenye jaa ya kioo yenye kimiminika cha kufyonza dawa. Funika mchanganyiko na acha kwa muda wa siku tatu au zaidi kwenye joto la ndani ya nyumba.Baada ya kutimia kwa siku tatu, tikisa kwa nguvu mara nyingi ili dawa iingie kwenye kimiminika. Baada ya hapo chuja dawa na kamua unga au vipande ili dawa yote itoke. Baada ya hapo unaweza kuchuja dawa kwa ajili ya matumizi au kuifanyia dekatensheni ili kupata kiini safi cha dawa.
​
Namna ya kuandaa pakolesheni ya dawa
Hii ni njia maarufu ya kuandaa tinkcha ya dawa au kufyonza dawa kutoka kwenye kimiminika. Njia hii inahitaji chombo maalumu chenye jina la pakoleta na unatakiwa kuwa mtaalamu zaidi kuandaa dawa kwa njia hii. Soma zaidi maelezo kwa kutumia linki chini ya tovuti hii.
Namna ya kuandaa dawa ya kufyonza kwa kimiminika
​
Njia hii huandaa dawa kutoka kwenye kimiminika chenye dawa au tishu za mnyama kwa kufyonzwa dawa hiyo kwa kutumia kimiminika kingine haswa pombe aina ya ehthanol au maji.
Kiasi cha pombe na maji yanayowekwa hutegemea aina ya dawa. Njia hii inahitaji uwe mtaalamu wa kuandaa dawa, unaweza kujifunza zaidi namna ya kuandaa dawa kwa njia hii kupitia linki chini ya tovuti hii au tumia dawa ambazo tayari zimekwisha andaliwa.
​
Namna ya kuandaa tinkcha ya dawa
Tinkcha ya dawa huandaliwa kwa kufanya masalesheni au pakolesheni ya dawa kwa kutumia kimiminika cha pombe tu. Njia hii ni nzuri ya kuvuna kiwango cha kiini unachotaka kutoka kwenye mimea au mnyama. Soma zaidi kuhusu njia hii kupitia rejea chini ya Makala hii.
​​
KUMBUKA:
Kama kuna haja ya kuchemsha dawa, hakikisha unatumia chomo kilichotengenezwa na udongo au sufuria za stainless steel na usifunike wakati wa kuchemsha ili kutoa sumu na kutobadili kiini cha dawa.
Usitumie dawa zaidi moja na kutibu tatizo moja au mawili tofauti ili kuepuka madhara na mwingiliano
​
Endapo unatumia dawa za hospitali, wasilina na daktari wako kukushauri ili kuepuka mwingiliano wa dawa na madhara yanayoweza kutokea.
ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute msaada kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba kupitia kitufe cha 'Pata tiba' au 'Mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
2 Agosti 2021 19:09:39
Rejea za mada hii;
1. Carnevale G et al. Griffonia simplicifolia negatively affects sexual behavior in female rats. Phytomedicine. 2010;17(12):987-991.
2. Chae H. Set al. 5-hydroxytryptophan acts on the mitogen-activated protein kinase extracellular-signal regulated protein kinase pathway to modulate cyclooxygenase-2 and inducible nitric oxide synthase expression in RAW 264.7 cells. Biol Pharm Bull 2009;32(4):553-557.
3. Iovieno N, et al. Second-tier natural antidepressants: review and critique. J Affect.Disord. 2011;130(3):343-357.
4. Pranzatelli M, et al. Neuropharmacology of progressive myoclonus epilepsy: response to 5- hydroxy-L-tryptophan. Epilepsia 1995;36(8):783-791
5. Wyatt R, et al. Behavioral changes of chronic schizophrenic patients given L-5- hydroxytryptophan. Science 9-22-1972;177(54):1124-1126
6. Angst J, et al. The treatment of depression with L-5-hydroxytryptophan versus imipramine. Results of two open and one double-blind study. Arch Psychiatr Nervenkr 1977;224:175-86
7. Birdsall TC. 5-Hydroxytryptophan: A Clinically-Effective Serotonin Precursor. Altern Med Rev 1998;3:271-80.
8. Cangiano C, et al. Effects of 5-hydroxytryptophan on eating behavior and adherence to dietary prescriptions in obese adult subjects. Adv Exp Med Biol 1991;294:591-3
9. Cangiano C, et al. Eating behavior and adherence to dietary prescriptions in obese adult subjects treated with 5-hydroxytryptophan. Am J Clin Nutr 1992;56:863-7.
10. Carnevale G, et al. Influence of Griffonia simplicifolia on male sexual behavior in rats: behavioral and neurochemical study. Phytomedicine 2011;18(11):947-52
11. Carnevale G, et al. Anxiolytic-like effect of Griffonia simplicifolia Baill. seed extract in rats. Phytomedicine 2011;18(10):848-51
12. Johnson KL, et al. Presence of peak X and related compounds: the reported contaminant in case related 5-hydroxy-L-tryptophan associated with eosinophilia-myalgia syndrome. J Rheumatol 1999;26:2714-7
13. Preshaw RM, et al.The dietary supplement 5-hydroxytryptophan and urinary 5-hydroxyindole acetic acid. CMAJ 2008;178:993
14. Rondanelli M, et al. Satiety and amino-acid profile in overweight women after a new treatment using a natural plant extract sublingual spray formulation. Int J Obes (Lond) 2009;33:1174-1182
15. Singhal AB,et al. Cerebral vasoconstriction and stroke after use of serotonergic drugs. Neurology 2002;58:130-3
16. Titus F,et al.5-Hydroxytryptophan versus methysergide in the prophylaxis of migraine. Randomized clinical trial. Eur Neurol 1986;25:327-9.
17. van Hiele LJ. l-5-Hydroxytryptophan in depression: the first substitution therapy in psychiatry? The treatment of 99 out-patients with 'therapy-resistant' depressions. Neuropsychobiology 1980;6:230-40
18. Wang XZ, et al. A new ß-carboline alkaloid from the seeds of Griffonia simplicifolia. Chin J Nat Med 2013;11(4):401-5
19. Infusion methods. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/infusion/#. Imechukuliwa 27.06.2021
20. Decoction extraction. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/decoction/. Imechukuliwa 27.06.2021
21. Extraction methods digestion. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/digestion/. Imechukuliwa 27.06.2021
22.Fluid extract. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/fluid-extract/. Imechukuliwa 27.06.2021
23. Tincture. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extracts/tincture/. Imechukuliwa 27.06.2021
24. Perolation. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/percolation/. Imechukuliwa 27.06.2021
25. Maceration. https://www.medicinalplants-pharmacognosy.com/pharmacognosy-s-topics/extraction-methods/maceration/. Imechukuliwa 27.06.2021