Mwandishi:
Dkt. Benjamin L, MD
Mhariri:
Dkt. Adolf S, MD
Dawa ya jipu ukeni
18 Juni 2021, 19:38:43

Jipu ukeni katika makala hii imetumika kumaanisha uvimbe maji au uvimbe wa usaha kwenye mirija ya batholin, soma zaidi kwa uelewa wa ziada kuhusu uvimbe wa batholin kwenye makala ya ‘jipu tundu la uke’ au ‘uvimbe wa batholin’.
Dawa ya kutibu jipu tundu la uke
Dawa zinazotumika kutibu uvimbe wa batholini ni unaojumuisha uvimbe wa maji au usaha zinaweza kuwa dawa za kupaka au kunywa. dawa hizo ni;
Trimethoprim-sulfamethoxazole
Amoxicillin-clavulanate
Clindamycin
Cefixime
Clindamycin
Kumbuka
Dawa zilizoorodheshwa hapo juu huwa zinatumika kwa mchanganyiko na hutegemea aina ya bakteria ambao wametengeneza uvimbe huo na mwitikio wao kwenye dawa. Wasiliana na mtaalamu daktari wako dawa gani na dozi gani utumie na kwa siku ngapi, endapo pia una ujauzito utashauriwa endapo haina madhara kwenye ujauzito
Matibabu ya jipu linalojirudia kweney mashavu ya uke ni yapi?
Endapo uvimbe wa batholin unajirudia rudia, unabidi kuonana na daktari kwa matibabu mengine ya dawa au upasuaji. Upasuaji hufanyika ndani ya siku moja na unawez akurejea nyumbani siku hiyo hiyo.
Unapata wapi taarifa zaidi kuhusu jipu tundu la uke?
Kupata taarifa zaidi kuhusu jipu tundu la uke ingia kwenye makala kwa kubofya linki hii