Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
11 Aprili 2020 16:55:11
Adalimumab
Ni dawa kwenye kundi la saitokini moduleta, dawa zingine katika kundi hili ni, Infliximab na golimumab. Dawa hizi zimetengenezwa kutoka kwenye antibodi za monokrono, antibodi hizi hufanya kazi za kuzuia saitokani za inflamesheni na tyuma necrosis facta alfa. Dawa hii inatakiwa kutumika chini ya uangalizi maalumu kutoka kwa mtaalamu mbobezi wa dawa.
Dawa huuzwa kwa jina la humira na hupatikana katika mfumo wa maji ambayo hutolewa kwa kuchomwa sindano.
Jinsi Adalimumab inavyofanya kazi
Dawa hii hushambulia Tyuma Nekrosisi Fakta alfa (TNF). TNF huzalishwa na mfumo wa kinga mwilini na kazi yake kuu ni kusababisha inflamesheni na uharibifu wa maungio ya mwili(jointi)
Dawa hii haipo kwenye makundi ya dawa za maumivu lakini inauwezo wa kupunguza maumivu ya jointi mwilini.
Dawa hii hutolewa kwa kuchomwa sindano na inatumika mara moja kwa mwezi, wagonjwa huweza kuelekezwa na daktarin ili kujidunga dawa wakiwa nyumbani.
Mwingiliano na chakula
Haina madhara yeyote ya muingiliano na chakula
Kazi za dawa ya Adalimumab
Hutumika kwa wagonjwa wa Ryumatoid arthraitizi- huu ni ugonjwa unaoshambulia jointi
Hutumika kwa wagonjwa wa psoriatiki arthraitizi - Ni aina ya arthraitizi ambayo huathiri watu wenye magonjwa ya ngozi
Hutumika kwa wagonjwa wenye aksho spondailoarthraitizi ,hii ni aina ya arthraitizi ambayo dalili moja kuu ya wagonjwa hawa ni maumivu kwenye mgongo
Hutumika kwa wagonjwa wa ankailozing spondilaitizi -hii ni aina ya arthraitizi ambayo huathiri zaidi uti wa mgongo na jointi kubwa za mwili
Hutumika kwa wagonjwa wa juvinaili idiopathiki arthraitizi ,hii ni aina ya arthraitizi ambayo hupelekea kuvimba kwa jointi zaidi ya moja hasa hasa huathiri wadada katika umri wa shuleni
Hutumika kwa wagonjwa wa asaletivu kolaitisi
Hutumika kutibu plagi ya soriasisi
Hutumika kwa mgonjwa wa Crohns
Hutumika kutibu Hidradenitisi Suppurativa ambao ni ugonjwa ambao husabisha uvimbe kwenye sehemu za siri na kwapani
Hutumika kutibu ugonjwa wa uveitis ambao ni uvimbe kwenye macho
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Adalimumab
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo :
Chanjo ya anthrax
Chanjo mfu ya hepataitiz A
Chanko ya hepataitiz A
Chanjo ya hpv
Chanjo ya kirusi cha influenza
Chanjo ya pneumococcal
Chanjo ya kichaa cha mbwa
Chanjo ya rubella
Chanjo ya hai tetekuwanga
Chanjo ya taifodi
Chanjo hai ya taifodi
Chanjo hai ya kirusi cha varicella
Chanjo ya kirusi cha manjano
Chanjo hai ya kirusi cha herpes zoster
Chanjo ya rubella na surua
Abatacept
Alefacept
Anakinra
Antithymocyte
Azathioprine
Baricitinib
Basiliximab
Chanjo hai ya bcg
Canakinumab
Certolizumab pegol
Cyclosporine
Chanjo ya dpt
Etanercept
Everolimus
Glatiramer
Golimumab
Hydroxychloroquine sulfate
Leflunomide
Infliximab
Muromonab cd3
Mycophenolate
Tacrolimus
Temsirolimus
Tocilizumab
Tongkat ali
Ustekinumab
Vedolizumab
Tahadhari ya Adalimumab kwa wagonjwa wafuatao;
Huweza kuongeza hatari ya kupata Maambukizi zaidi sababu hupunguza kinga ya mwili
Huweza kupelekea hatari ya moyo kuferi
Hupunguza chembechembe nyeupe za danu
Kama mgonjwa atapata hali ya lupus dawa hizi zinaoaswa kusimamishwa ,hali hii ni uvimbe ambao hutokea endapo seli za kinga ya mwili zitashambulia seli zake zenyewe
Huweza kupelekea shida kwenye ini
Matumizi ya Adalimumab Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii haipaswi kutumika kwa mama mjamzito na mama anayenyonyesha
Pia haitumiki kwa wagonjwa wenye Maambukizi ya VVU, saratani, multiple sclerosis, Kifua kikuu, Hepatitis B na magonjwa ya moyo
Maudhi ya Adalimumab
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :
Maumivu kwenye alipochomwa sindano
Maambukizi ya juu ya mfumo wa upumuaji
Increased creatine phosphokinase
Maumivu ya kichwa
Kutokwa na vipele
Sinusaitizi
Kichefuchefu
Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Tumbo kuuma
Homa kama ya mafua
Kuwa na mafuta kwa wingi mwilini
Maumivu ya mgongo
Kolestro kuwa kwa wingi
Kukojoa damu
Shinikizo la damu kuwa juu
Kuongezeka kwa vimeng’enya ini vya alkaline phosphatase
Je endapo umesahau dozi ya Adalimumab ufanyeje?
Endapo mgonjwa atasahau kutumia hii dozi anapaswa kuwasiliana na daktari aliyemuandikia dawa hii
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:51:13
Rejea za mada hii:-