Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
18 Aprili 2020, 18:17:28
Amlodipine
Ni aina ya dawa iliyo kwenye kundi la dawa za kushusha shinikizo la juu la damu linaloitwa kalisimau chaneli bloka, hutumika katika matibabu ya shinikizo la juu la damu(haipatensheni) na anjaina. Dawa hii huuzwa mara nyingi kwa jina la Norvasc, rangi yake mara nyingi ni nyeupe hata hivyo hutegemea rangi pendekezwa ya kiwanda.
Dawa zilizo kundi moja na Amlodipine
Felodipine
Isradipine
Nicardipine
Nifedipine
Jinsi Amlodipine inavyofanya kazi
Amlodipine hufanya kazi kwenye mishipa ya damu ya pembeni na huwa husababisha maudhi kidogo sana ya kushusha mapigo ya moyo na utendaji wa umeme ndani ya moyo ukilinganisha na dawa zingine kwenye kundi lake. Hata hivyo hutumika kidonge kimoja kwa siku na hivyo kuifanya ipendwe san ana wagonjwa.
Dawa hii huwa na antioksandi ya naitriki oksaidi ambayo hufanya mishipa ya damu ya pembeni ipanuke na hivyo kupungua kwa shinikizo la dam na kutibu anjaina.
Kazi za dawa ya amlodipine ni;
Hutumika kutibu shinikizo la juu la damu
Hutumika kutibu anjaina
Dawa zilizo kundi moja na amlodipine
Diltiazem
Apalutamide
Lofexidine
Nefazodone
Idelalisib
Simvastatin
Ivosidenib
Dawa ya amlodipine haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye mzio na dawa hiyo
Tahadhari ya amlodipine kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye moyo ulioferi
Wagonjwa wenye Magonjwa ya Ngozi
Matumizi ya amlodipine Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Amlodipine haina shida endapo itatumika kwa mama mjamzito maana haina hatari yeyote kwa mtoto
Hakuna madhara yeyote kwa mtoto endapo itatumika kwa mama anayenyonyesha
Maudhi ya Amlodipine
Kizunguzungu
Kichefuchefu
Kuwashwa mwili
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Kupata vipele kwenye Ngozi
Misuli kukosa nguvu
Je endapo umesahau dozi ya Amlodipine ufanyeje?
Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, isipokuwa muda kama umekaribia wa dozi ingine ruka dozi uliyosahau na endelea na dozi kwa muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:51:38
Rejea za mada hii:-