top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

21 Aprili 2020 09:57:03

Captopril

Captopril

Captopril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la jina la Capoten


Rangi ya Captopril


Rangi ya Captopril huweza kuwa nyeupe au rangi ya maziwa, lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotenegenza

Dozi na matumizi ya Captopril


Dawa hii inashauriwa kutumia lisaa limoja kabla ya kula chakula kama utakavyoshauriwa na daktari wako. Tumia dawa hii na maji ya kutosha. Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa. Baada ya wiki mbili au zaidi tangu ulipoanza kutumia dawa hii shinikizo la damu litashuka na kuwa la kawaida. Shinikizo la damu likiwa la kawaida usahilishe matumizi ya dawa hii ili uendelee kuwa na afya njema.


Captopril hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,



  • 12.5mg

  • 25mg na

  • 50mg


Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.


  • Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na captopril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu

  • Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa Bradykinin. Kutanuka kwa mishipa husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.

  • Hupinga kazi za homoni ya angiotensini II kwenye mishipa ya fahamu ya simpathetiki.

  • Huongeza uwezo wa figo kupoteza madini ya sodiamu na maji kwa njia ya mkojo kwa kupinga uzalishaji wa homoni ya aldosterone inayochochewa kuzalishwa Zaidi na homoni ya angiotensin II. Homoni ya aldosterone kazi yake ni kutunza maji na madini hayo mwilini.

  • Huzuia kutokea kwa mabadiliko ya kuta za moyo na mishipa ya damu kutokana na shinikizo la damu, kuferi kwa moyo na infaksheni ya mayokadia.


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (kundi la ACEIs) na dawa hii ni;


  • Benazepril

  • Enalapril

  • Fosinopril

  • Lisinopril

  • Moexipril

  • Perindopril

  • Quinapril

  • Ramipril


Kazi ya dawa:


  • Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu

  • Hutumika kwenye matibabu ya moyo ulioferi

  • Hutumika kwa kupunguza athari za magonjwa ya figo(dayabetiki neohropathi) kwa wagonjwa wenye kisukari


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


  • Venetoclax

  • Valsartan

  • Topotecan

  • Tolmetin

  • Telmisartan

  • Sulindac

  • Salsalate

  • Sacubitril/valsartan

  • Sacubitril/valsartan

  • Pregabalin

  • Piroxicam

  • Oxaprozin

  • Olmesartan

  • Naproxen

  • Nabumetone

  • Meloxicam

  • Mefenamic acid

  • Meclofenamate

  • Losartan

  • Lofexidine

  • Lanthanum carbonate

  • Ketorolac

  • Ketoprofen

  • Irbesartan

  • Indomethacin

  • Ibuprofen iv

  • Ibuprofen

  • Flurbiprofen

  • Fenoprofen

  • Etodolac

  • Eprosartan

  • Diflunisal

  • Diclofenac

  • Dextran yenye madini chuma

  • Dawa ya mishipa ya Sodium phosphates

  • Dacomitinib

  • Choline magnesium trisalicylate

  • Celecoxib

  • Candesartan

  • Azilsartan

  • Aspirin rectal

  • Aspirin

  • Allopurinol

  • Aliskiren

  • Aliskiren


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za ACEIs


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


Wagonjwa wenye anyuria (figo Kutozalisha mkojo)


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


  • Dawa hii ipo kwenye kundi C na D ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito

  • Haipaswi kutumika kwa mamam mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni. Madhara hayo kwa mtoto ni haipotension, haipoplezia ya fuvu, anyuria, kuferi wa figo na kifo.

  • Haishauriwi kutumika kwa mama anayenyonyesha kwa sababu huingia kwenye maziwa ya mama.


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


  • Kikohozi kikavu

  • Maumivu ya kifua

  • Kupoteza ladha ya chakula

  • Ganzi kwenye miguu na miguu kuchoma choma

  • Kukojoa protini

  • Vipele kwenye ngozi

  • Haipotensheni

  • Haipakalemia

  • Vipele kiasi na kuwashwa kwa ngozi


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:48:21

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.captopril.https://www.drugs.com/captopril.html. Imechukuliwa 20/4/2020

2.Medscape.captopril.https://reference.medscape.com/drug/capoten-captoril-captopril-342315. Imechukuliwa 20/4/2020

3.WebMd.captopril.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-964/captopril-oral/details. Imechukuliwa 20/4/2020

4.MedicinePlus.captopril.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682823.html. Imechukuliwa 20/4/2020
5. A Textbook of Clinical Pharmacology and Therapeutics FIFTH EDITION JAMES M RITTER ,LIONEL D LEWIS ,TIMOTHY GK MANT ,ALBERT FERRO. ISBN 978-0-340-90046-8. Ukurasa wa 187-188

6. Cardiovascular Pharmacology Concepts ACEIs. https://cvpharmacology.com/vasodilator/ACE. Imechukuliwa 20/4/2020
bottom of page