Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Aprili 2020 16:12:09
Chlorthalidone
Chlorthalidone ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu pamoja na uvimbe wa mwili kutokana na magonjwa ya moyo Ini au figo. Dawa hii iliyo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Thiazide Diuretiksi, huwa maarafu kwa majina ya Hygroton,Thalitone na Chlorthalid.
Rangi ya Chlorthalidone
Rangi ya dawa huwa ni nyeupe, hata hivyo hutegemea rangi iliyochaguliwa na kiwanda.
Kunywa dawa hii baada ya kulak ama vile ulivyoelekezwa na daktari wako. Usinywe dawa masaa kabla ya kulala ili kuzuia kuamka mara kwa mara kukojoa. Kwa sababu dawah ii hutumika mara moja kwa siku ni vema ukachagua muda mwingine mbali na muda wa karibia kulala.
Licha ya hivyo dawa hii hupunguza hatari ya kupata kiharusi, infaksheni ya mayokadia, kuferi kwa moyo na madhara yanayotokana na shinikizo la juu la damu.
Chlorthalidone hupatikana katika mfumo wa kidonge wenye uzito wa Milligram zifuatazo
15mg
25mg
50mg
100mg
Namna dawa inavyofanya kazi
Hufanya kazi kwa kuongeza fugo kupotezaji madini ya kloraidi na sodiamu kwenye mkojo. Madini haya yanapopotea kwenye mkojo huambatana na maji, shinikizo la damu hupungua kutokana nakupungua kwa maji kwenye mishipa ya damu.
Madini haya pia yanapopotea kwenye mkojo Pamoja na maji hurusu maji yaliyotuwama kwenye mwili kupungua pia, ndo maana dawa hii ikitumiwa na watu waliovimba kutokana na kutuwama kwa maji kwenye miguu na sehemu zingine, uvimbe huo hupotea.
Madini ya sodiamu yanapopungua kwenye mishipa ya damu, husababisha kutanuka kwa mishipa ya dam una kushuka kwa shinikizo la damu.
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na Thiazide Diuretiks ni;
Bendroflumethiazide
Chlorothiazide
Methyclothiazide
Polythiazide
Hydrochlorothiazide
Metolazone
Indapamide
Kazi ya dawa;
Hutumika kutibu uvimbe wa mwili unaotokana na magonjwa ya moyo kuferi, magonjwa ya ini na figo.
Hutumika kutibu shinikizo la juu la damu.
Hutumika kutibu shinikizo la damu kwa mgonjwa mwenye moyo ulioferi
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Aminolevulinic acid ya kunywa
Isocarboxazid
Lofexidine
Methyl aminolevulinate
Squill
Tretinoin
Tahadhari ya dawa;
Itumike kwa tahadhari kwa wagonjwa wa kisukari, wenye upungufu wa elekrolaiti, wenye madini ya kalisimau kwa wingi kwenye damu na shinikizo la chini la damu.
Hupaswa kutumika kwa Tahadhari kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo na ini
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Wagonjwa Wenye matatizo ya kutoa mkojo(kukojoa)
Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Dawa hii ipo kwenye kundi C ya usalama wa dawa kipindi cha ujauzito
Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito na mama anayenyonyesha
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ni;
Kushuka kwa shinikizo la damu
Arizimia
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Kuchoka
Kukosa hamu ya kula
Kichefuchefu
Kutapika
Kukojoa sana
Kutokuona vizuri
Elekrolaiti kupungua
Vipele
Konstipesheni
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?
Endapo umesahau kunywa dozi yako, kunywa mara moja utakapokumbuka isipokuwa muda wa dozi ingine umekaribia. Wasiliana na daktari endapo unahitaji maelezo Zaidi.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:48:53
Rejea za mada hii:-